KIVULI NDANI YA MWILI { SEHEMU YA SITA }

   Walimpa kipigo zaidi ili aseme mengi juu ya pikipiki hiyo alioiba Segerea ndipo  akaanza kusema akuwa peke yake, alikuwa na wenzake baada ya kuiba hiyo pikipiki waliipeleka makao makuu. Lakini huko makao makuu  akujua aliuziwa nani maana wao kazi yao kuiba pikipiki na kuzifikisha makao makuu yao, maswala ya kuuza anajua bosi wao.

          O.S.S mkuu wa upelelezi alimuuliza huyo mwizi anapopatikana huyo mkuu wao. Mwizi alisema anapopatikana huyo mkuu wao. O.S.S anatoa hoda akamatwe mara moja, anamtumia Muona afanye hiyo kazi, Muona akupoteza muda anaenda. Muona kwakuwa Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki ni mpenzi wake alimpigia simu.


"Mwanaume upo wapi?'

"Nyumbani mwanamke"

"Ok! nakuja sasa hivi nimekumiss sana"

"Sawa! utanikuta"

         Muona alikata simu, anaambatana na askari wenzake wanaingia katika gari la polisi wanaelekea nyumbani kwa mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani. Safari ya kutoka kituo cha polisi hadi nyumbani kwa mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani, mwendo wa dakika ishirini wanafika nyumbani kwa mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki. Gari la polisi lilisimama mbali na hapo nyumbani kwa mkuu wa kitengo wizi wa pikipiki mitaani. 

          Muona aliingia ndani ya nyumba ya mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani na askari wengine wanaizunguruka nyumba yote. Chakushangaza Muona alipoingia ndani alikuta milango yote ipo wazi na nyumba imetawariwa na ukimya. Aliingiwa na wasi wasi na alijiandaa kukabiliana na hatari yeyote itakayotokea mbele yake lakini alipofika sebuleni.

"Haah! Mungu wangu!"

          Alishtuka baada ya kumuona Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani ameuliwa kinyama na ametobolewa macho. Alipiga simu kwa askari wenzake waliopo nje na kuwaita haraka ndani. Askari walifika haraka haraka huku wakiwa na taadhali kubwa, walishtushwa baada ya kumuona Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani ameuliwa kikatili sana. Hakuna aliyekuwa tayari kuamini kwamba, kweli Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani amekufa, wakati muda mfupi uliopita Muona ametoka kuongea nae, ilikuwa ni kama ndoto! Muona aliishiwa nguvu na kujiona mpumbavu, mpango wake wa kuanzisha mahusiano na Scorpion ili kumtia nguvuni umeferi.

Alijiona mpumbavu wa wapumbavu kwa kumkabidhi Scorpion mwili wake akauchambua kama karanga mwisho wa siku, Scorpion amekufa bila kutimiza lengo la kumkamata kwa mikono yake. Alijilaumu tena na tena na kujitoa thamani kama mwanamke yeyote duniani kote, aliamini kumpa penzi Scorpion ndio njia ya kumkamata na ndio ungekuwa mwisho wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani lakini sivyo alivyotarajia.


Scorpion amekufa, askari wanafanya uchunguzi eneo lote la nyumba ya Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani bila kupata ushahidi wowote. Taarifa ilifika kwa O.S.S na wanaibeba maiti ya mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani na kuifikisha hospitali ya Amana.

**********

          Msaidizi wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani akiwa makao makuu akiendelea na kuboa pikipiki na kutoa injini bila kujua kinachoendelea kama vijana wake wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani wamekamatwa na Scorpion mkuu wake ameuliwa kinyama na watu wasiojulikana. Simu yake ya mkononi inaita anaitoa mfukoni anaangalia ni namba 0764 07 07 97 ni namba ngeni katika simu yake, anapokea.

"Bila shaka assistance director Scorpion Gereji?"

"Ndio"

"Mimi ndio bosi wa injini za pikipiki hapo Scorpion Gereji sasa naomba tukutane kwa ajiri ya kufanya biashara za injini"

"Sawa! lakini vizuri zaidi ungekuja ofisini hapa"

"Nilitaka nije lakini nahofia foleni sasa naomba chukua pikipiki uje wewe Kurasini shimo la udongo"

"Sehemu gani?"

"Ukifika katika ofisi ya Camel Oil nijulishe nitakuelekeza kwa kuja"

"Sawa! bosi"

          Simu ilikatwa, msaidizi anampigia simu mkuu wake ili kumjulisha taarifa hiyo lakini simu ilikuwa inaita bila kupokelewa. Anatuma meseji kuwa anaenda kukutana na mnunuzi wa injini kwa ajiri ya kufanya mazungumzo ya biashara. Simu ilikuwa chini ya mikono ya askari, askari walipopata taarifa hiyo wanagundua kuwa huyo msaidizi anahusika katika kitengo cha wizi wa pikipiki na huyo bosi mnunuzi wa hizo injini za pikipiki ni muhimu kupatikana. Walituma meseji na kujifanya Scorpion na kumwambia kuwa anafika hapo makao makuu muda si mrefu.

          Msaidizi  baada ya kupokea taarifa hiyo kutoka katika simu ya bosi wake aliamua kusubiri hadi bosi wake afike. Akiwa anamsubiri bosi wake mara simu yake inaita, anatoa mfukoni anaangalia ni namba ya yule mnunuzi.


“Umefikia wapi mpaka muda huu?”

“Namsubiri bosi afike ili tuje wote maana nimeongea nae sasa hivi, amese...."

          Kabla ajamaliza kusema, simu ilikatwa. Msaidizi anashangaa kukatwa simu ghafla anampigia lakini simu aipatikani. Msaidizi anapiga simu katika simu ya bosi wake, lakini simu inaita bila kupokelewa. Muda huo huo anatumiwa ujumbe mfupi na simu ya bosi wake kuwa yupo njiani anaendesha gari. 

          Msaidizi baada ya kupokea ujumbe huo aliendelea kusubiri ghafla bila kutegemea, alishtukia askari wanaingia na kumuweka chini ya ulinzi. Msaidizi wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani alitii sheria bila shuruti ananyoosha mikono juu, wanampokonya simu na wanamkamata wanamtoa nje wanamuingiza katika gari, hawakupoteza muda eneo hilo wanawasha gari na kuondoka.

          Walipofika kituoni walimuingiza selo kiongozi msaidizi wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani. O.S.S aliangalia katika simu ya huyo msaidizi wa kitengo cha wizi wa pikipiki mtu wa mwisho kuongea nae ni nani? ndipo wanagundua ni private namba ilikuwa ngumu kumjua, walipiga hiyo namba lakini simu ilikuwa aipatikani. Walienda hadi selo wakamtoa msaidizi na kumuingiza chumba cha upelelezi na kuanza kumpa adhabu kali ili aseme aliekuwa anaongea nae nani na yupo wapi?. Lakini msaidizi akuweza kumjua kwa jina huyo aliekuwa anaongea nae zaidi aliwaambia kuwa alijitambulisha kama mnunuzi wa injini za pikipiki na alitaka wakutane waongee kuhusu ununuzi wa injini za pikipiki.

 O.S.S alitoa simu ya Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani na kupiga katika simu ya msaidizi wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani.

“Namba ya nani hiyo?”

Msaidizi anaangalia anaona namba ya bosi wake.

“Ni bosi wangu”

“Yupo wapi?”

“Aliniambia yupo njiani anakuja ofisini?”

          Mkuu wa upelelezi alitoa picha za maiti ya mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipki anamuonesha huyo msaidizi.

“Ndiyo huyu?”

Msaidizi anaangalia hiyo picha anashtuka baada ya kumuona ameuliwa kinyama.

"Ndiyo huyo?"

"Ndiyo!"

“Ameshauliwa na watu wasiojulikana kwa hiyo tunataka kufahamu yote kuhusu yeye”

          O.S.S baada ya kumwambia hivyo huyo kiongozi msaidizi wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani, anawaambia askari waletwe wale wezi waliohusika katika mauaji ya dereva pikipiki Segerea, askari walifanya kama walivyoambiwa, hao wezi waliletwa.

“Mnamfahamu huyu?"

Wezi walithibitisha wanamfahamu msaidizi wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani.

"Kama nani kwenu?”

“Kiongozi badala ya bosi hapo tulipokuwa tunafanya kazi”

Walijibu wote kwa pamoja.

“Vizuri! Hawa ndio waliohusika katika mauaji ya dereva pikipiki Tabata Segerea na kuiba pikipiki na hiyo pikipiki imehusika katika tukio lingine la mauaji Tabata Mawenzi na miongoni mmoja wapo aliokuwepo katika hilo tukio ni Imamu wa msikiti wa Almasjid Tidc Tabata Mawenzi kituo cha chama, sasa kama kiongozi wa genge lenu la wizi utakuwa unafahamu tukio hilo”

Kiongozi msaidizi wa kitengo cha wizi wa pikipiki alianza kukumbuka juu ya tukio hilo, anaanza kuelezea juu ya tukio ilo lilivyokuwa hadi kufika katika mauaji.

**********

          Wakati wa tukio hilo kabla ya kutokea msaidizi alikuwa na muda wa miaka mitatu katika kitengo hicho cha wizi wa pikipiki mitaani na biashara ya madawa ya kulevya ilikuwa haiendi vizuri kwa sababu mtu wa kusafirisha hakuwepo. Scorpion alilazimika kumshawishi Imamu Shafii wa msikiti wa Almasjid Tidc, amtumie katika biashara ya madawa ya kulevya kwa kutumia mwavuli wa dini. Imamu Shafii wa Almasjid Tidc alikataa. Scorpion akagundua njia nyingine ya kumwingiza katika biashara hiyo Imamu Shafii. alimtumia kijana mmoja kutokea Tbata Kimanga eneo la Mandela juu ambae alijukana kwa jina Yahaya Salumu almaarufu Albata Dickson. Scorpion alimchagua kijana huyo kutokana na uwezo wake wa kumshawishi mtu.

          Siku ya kwenda mitaani kuiba pikipiki, wezi wote walipangiwa kwa kwenda kuiba pikipiki lakini Albata akupangiwa aliambiwa kuna kazi nyingine anatakiwa apewe.  Albata alisubiri hiyo kazi aliokuwa anatakiwa kupewa na bosi wake.  Baada ya kusubiri kwa muda, aliitwa ofisini, alipofika ofisini alipewa kazi ya kwenda Tabata Mawenzi katika msikiti wa Almasjid Tidc kumshawishi Imamu ili wafanye nae miadhara mikoa mbalimbali na nje ya nchi.

          Albata alikubali kuifanya hiyo kazi na aliahidi kuikamilisha ndani ya muda mfupi kutokana na uwezo wake wa kushawishi na kwakuwa huyo Imamu Shafii anafahamiana nae sana. Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani alimuahidi donge nono la pesa endapo Imamu huyo akikubali. Alipewa pesa ya matumizi akiwa katika hiyo kazi ya kumshawishi Imamu Shafii na ile pikipiki ilioibiwa Tabata Segerea ilitolewa preti namba yake, ikawekwa preti namba nyingine akapewa Albata kama usafiri wakati wa  kwenda kumshawishi Imamu Shafii.

          Siku iliyofuata, Albata anafika Tabata Mawenzi katika msikiti wa Almasjid Tidc, mishale ya saa saba mchana aliungana na waumini wa kiisalmu katika ibada ya saa saba. Dakika kumi baadaye, wanamaliza ibada. Albata anamuona Imamu anatoka ndani ya msikiti anaondoka, alimuwai alimuomba kuongea nae. Imamu kwa jinsi alivyomuona Albata akuweza kumtiria mashaka kwakua alikuwa amevaa kanzu safi vazi la waumini wa kiume wa kisalamu, kibarakashia na sendo nzuri kwa haraka haraka vitu vyote alivyo vaa thamani yake kama laki  moja na nusu. 

          Imamu alijua Yahaya anataka kuoa, anatafuta shekhee wa kusimamia ndoa yake, bila kipingamizi anakubali kumsikiliza.Ndipo Yahaya alimwambia Imamu anataka kuambatana nae katika mikoa na nchi mbali mbali ili kufanya miadhara juu ya mafudisho ya dini ghalama zote kama usafiri, chakula na malazi atasimamia yeye. Imamu Shafii alikubali bila kipingamizi maana ndio jambo kila siku alikuwa anawaza juu ya kufanya muadhara kuhusu mafundisho ya dini ya kiislamu lakini tu pesa ndio ilikuwa tatizo.

          Walipanga siku ya kukutana tena ili wapange mambo mengine ya mafundisho na wapi wataanzia. Walipeana namba za simu na wanaagana Imamu Shafii anaondoka hapo msikitini akiwa mwenye furaha sana baada ya kusogezewa fursa ambayo alikuwa anaitaka kuifanya lakini alikosa pesa na wafadhiri. 

          Yahaya aliondoka hadi ofisini kwao Scorpion Gereji. Alipofika alikutana na Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki alimpa taarifa ya kuwa Imamu Shafii amekubali. Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani alifurahi sana, imani yake ilisadiki mpango wake unakwenda kufanikiwa na mradi wake utakuwa sawa muda wowote.

          Siku iliyofuata Yahaya alienda Almasjid Tidc, ndio siku waliopanga kukutana na Imamu Shafii, anakutana na Imamu Shafii, baada ya ibada ya saa kumi Imamu Shafii alimtambulisha Yahaya  kwa waumini wote na akawaeleza juu ya ujio wake. Waumini walifurahi sana na kumshukuru kwa kujitolea kusambaza dini na kutoa mafundisho ya neno la mungu. 

          Siku hiyo hiyo baadaye, Imamu Shafii aliwachukua baadhi ya waumini aliowaona watafaa katika hiyo kazi ya muadhara, walikaa pamoja na Yahaya walianza kupanga mambo mengi juu ya muadhara na kwa kuanzia muadhara.Dakika mia moja themanini, ziliwatosha kupanga mambo yote na kumaliza, Yahaya aliondoka, alirudi hadi ofisini na kukutana na mkuu wake na alimwambia maendeleo mazuri Imamu amewashirikisha baadhi ya waumini wake. Ilikuwa furaha ilioje kwa Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki aliamini kupiga hatua katika huo mradi wake maana Imamu Shafii akishirikiana na waumini wenzake ndio itakuwa vizuri atawatumia wote kuwabebesha madawa ya kulevya kutoka nchi zinazouza madawa ya kulevya na kusafirisha madawa ya kulevya wakiwa wanaenda katika hiyo miadhara.

          Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani alimpatia pesa Yahaya na alimwambia akawanunulie kanzu, kofia  ambazo watazitumia watakapoanza kazi ya miadhara na wakimaliza kununua hivyo vitu aende na huyo Imamu hadi hoteli ya Kilimanjaro ili wakale chakula cha mchana. Yote ni kumvuta Imamu Shafii katika kazi yao. Yahaya alifanya kama alivyoambiwa, alimpigia simu Imamu Shafii na kumwambia wakutane kariakoo, bila kipingamizi Imamu Shafii alikubali wito.

          Imamu Shafii alipanda gari kituo cha chama, alielekea kariakoo. Alitumia kama nusu saa kufika kariakoo alikutana na Yahaya. Yahaya alimuongoza Imamu Shafii katika duka wanalouza kanzu, kofia na vitu vingine vya aina hiyo na kuanza kununua. Imamu alifurahi sana na alimshukuru Yahaya. 

"Mungu akufanyie wepesi katika mambo yako ili ufanye makubwa zaidi ya haya"

"Inshallah!"

"Maana ni vijana wachache wenye nia kama yako, wengi wao pesa zao wanazitumia katika anasa'

"Ni kweli'

"Lakini wewe mungu amekupa ufahamu wa kufanya haya ni jambo kubwa sana, nakuombea maisha marefu ufanye makubwa"

"Inshallah!"

          Walimaliza kununua vitu vyote, walitumia usafiri wa gari aliokuja nayo Yahaya na walielekea hadi hotel mashuhuri hapo mjini inayojulikana kama HYAUPEGENCY DAR ES SALAAM THE KILIMANJARO. Kwa mara ya kwanza Imamu anaingia ndani ya hoteli hiyo kila kitu kwake kilikuwa kigeni. Yahaya alimuongoza hadi ndani ya hiyo hoteli hadi sehemu ya chakula lakini cha kushangaza Imamu aliwaona mashekhee wengi lakini wengi wao ni vijana wazee wachache. 

          Yahaya alimuelekeza sehemu ya kukaa Imamu Shafii baada ya hapo alienda kwa kila shekhee na kuanza kumsalimia na kumkaribisha. Imamu shafii alikuwa katika hali ya mshangao huku imani yake ilisadiki kuwa ni mtu mashuhuri na mwenye pesa ila ni muda gani ameanza kuwa na pesa kiasi hicho cha kuweza kuwapeleka watu wengi kiasi hicho hoteli hiyo kubwa kwa sababu anamfahamu Yahaya pamoja na familia yake.

          Yahaya alimaliza kumsalimia kila shekhee alirudi kukaa na kwa pamoja wakapata chakula na wageni wake wote. Walipomaliza kula kila shekhee alijitambulisha sehemu anayotoka, wengi walikuwa wanatoka mikoani. Walipata kufahamina mashekhee wote, Imamu Shafii peke yake ndio anatoka mkoa wa Dar es salaam. Baada ya utambulisho, Yahaya alijitambulisha kwa mashekhee wote na kuwaeleza kazi itakapoanzia ya miadhara na mafundisho ya dini. Kila shekhee alielewa na kuahidi kutoa elimu kubwa juu ya mafundisho ya dini sehemu zote.

          Dakika ishirini na tano baadaye, walifika watu walimpa kila shekhee bahasha yake, baada ya hapo kikao kiliisha na kila mmoja alipata nafasi ya kuondoka. Yahaya na Imamu Shafii waliingia ndani ya gari waliokuja nayo na kuondoka hotelini hapo, walielekea hadi Tabata Mawenzi msikiti wa Almasjid Tidc. Walipofika Imamu aliweka ndani hivyo vitu, baada ya kuhakikisha vipo sehemu salama aliingia ndani ya gari na Yahaya alimpeleka Imamu hadi nyumbani kwake, baada ya hapo Yahaya aliondoka zake.

          Siku hiyo hiyo jioni, Imamu alipata nafasi aliichukua ile bahasha aliopewa akaanza kuifungua, cha kwanza alikutana na kibunda cha pesa alishukuru mungu maana ni mwanzo mzuri wa mafanikio lakini alipofungua zaidi hiyo bahasha alikutana na barua. Taratibu aliifungua na kuanza kuisoma lakini hapo hapo muonekanao wake wa sura ulianza kubadirika baada ya kusoma kilichoandikwa ndani ya hiyo barua akutaka kuendelea kusoma hiyo barua aliikunja na kuirudisha ndani ya hiyo bahasha pamoja na zile pesa alizozikuta ndani ya hiyo bahasha. 

          Muda huo huo Imamu Shafii alitoka nyumbani kwake alienda hadi msikitini akaweka hiyo bahasha katika vitu alivyonunuliwa, baada ya hapo alimpigia simu Yahaya wakutane msikitini. Yahaya aliitikia wito, alifika msikitini alikutana na Imamu Shafii. Imamu Shafii cha kwanza alimkabidhi Yahaya vitu vyote alivyonunua kwa ajiri yake na waumini wengine.

"Aiwezekani, aitowezekana  na kama utaendelea  kuja hapa msikitini kwa ajiri ya ibada na si vinginevyo"

          Imamu akutaka hata jibu taratibu aliondoka na kumuacha Yahaya hapo eneo la msikitini. Yahaya alibaki katika mshangao kwa kile alichojibiwa na Imamu Shafii, kutokana na muonekano aliomuona nao Imamu, akutaka kumwita ili afahamu nini kimetokea mpaka amerudisha hivyo vitu, alipanga kurudi siku nyingine baada ya hasira zake kuisha hivyo alichukua hivyo vitu na kuondoaka.

          Njiani alijiuliza mengi juu ya uhamuzi aliochukua Imamu Shafii wa kukataa wakati kamwambia jambo zuri la miadhara juu ya mafundisho ya dini. Hadi anafika nyumbani kwake akuweza kutambua nini hasa Imamu Shafii kimembadilisha mawazo yake. Anafika nyumbani kwake alishusha huo mzigo wa vitu aliourudisha Imamu Shafii lakini akiwa ameubeba anapeleka ndani ghafla inaanguka bahasha chini anaiyokota anaingia ndani.

         Alipofika ndani aliweka hivyo vitu alikaa chini akaanza kufungua hiyo bahasha, alianza kukutana na pesa katika kibunda aliziesabu kwa haraka haraka aligundua ni taslimu laki tano. Alipoangalia vizuri ndipo alipoona karatasi nyeupe, aliitoa hiyo karatasi na kuanza kuisoma. Alichokisoma katika hiyo barua akutaka kundelea tena kusoma hata nguvu ya kuiweka hiyo barua katika bahasha yake alishindwa alijiraza hapo katika kochi mpaka usingizi ukampitia.

          Masaa mawili yalikatika mpaka kuja kuzinduka, ilikuwa ni saa sita na dakika ishirini, alichukua maji aliweka katika ndoo ya chooni aliingia bafuni na kuanza kuoga. Alitumia dakika tano kuoga alipomaliza alijiandaa kwa vazi lake la kanzu aliondoka hadi msikitini. Hadi anafika hapo msikitini muda wa ibada ulikuwa ushawaidia hivyo aliungana na waumini wa kiislamu waliingia katika ibada. Sala iliongozwa na Imamu Shafii mpaka anamaliza. Muda wa kutoka Yahaya alionana na Imamu Shafii, alimuomba kuongea nae. 

          Imamu Shafii akutaka kuongea wala kumsikiliza Yahaya, Yahaya alijitetea akuja na yale yale ila amekuja kwa kuhitaji msamaha kwa kile kilichotokea kwa sababu hata yeye alikuwa ajui. Imamu Shafii akuweza kumuelewa maana yeye ndie aliejitambulisha kama ndio kila kitu katika mpango huo wa kufanya miadhara mikoani na nje ya nchi na ghalama zote atazisimamia yeye mwenyewe sasa leo hii iweje aseme hata yeye alikua ajui.

          Yahaya alimuomba sana Imamu, akasababisha Imamu kuchukia na kuanza kongea kwa ukali akimsisitiza ataki kuongea nae, Imamu Shafii hasira zilimpanda hadi alitaka kumpiga Yahaya lakini  waumini waliokuwepo hapo msikitini walimzuia Imamu na kummtuliza. Wengine walimwambia Yahaya aondoke ili kuepusha matatizo. Yahaya alitii kauli ya waumini aliingia ndani ya gari aliondoka. Yahaya akupenda kwa kile kilichotokea maana huyo Imamu wanafahamiana sana na anamuheshimu sana. Njia nzima alisikitika sana kwa kumkosea bila kujua, alishindwa kujizuia machozi yalimtiririka na kuanza kulia kwa uchungu.

          Waumini walitaka kufahamu nini hasa mpaka wanakosana na Yahaya lakini Imamu akutaka kueleza chochote kilichotokea ila tu aliamua kuondoka msikitini hapo na kuelekea nyumbani kwake. Alipofika nyumbani kwake akuwa na furaha, mkewe aliigundua hali hiyo alimuuliza lakini Imamu akutaka hata kumueleza kilichotokea zaidi tu alimwambia mke wake kuna mtu wamekosana kikauli. Mke wa Imamu akutaka kufatiria sana.

          Safari yake Yahaya iliishia hadi nyumbani kwake. Alichukua ile bahasha na kuondoka hadi makao makuu ya kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani. Alipofika makao makuu moja kwa moja hadi ofisini kwa bosi wake alimkuta mkuu wake na msaidizi wake ambae ni fundi wa pikipiki katika hicho kitengo cha wizi wa pikipiki. Bila salamu aliaanza kumwambia ameshindwa kumshawishi Imamu. Mkuu wake alimuuliza sababu ya kushindwa kwake, Yahaya alitoa ile bahasha na kuibwaga mezani.

“Kama ningejua kuwa ni kumshawishi kwa ajiri ya kumtumia katika kufuata madawa ya kulevya na kusafirisha madawa ya kulevya, nisingethubutu kumwambia maana yule kama mzee wangu pia namuheshimu sana na yeye ananiheshimu ndiyo maana nilipomshawishi juu ya kufanya miadhara alikubali haraka”

“Sikiliza kama uliamua kuingia katika kazi ya wizi wa pikipiki tena unaua vipi unashangaa kusambaza madawa ya kulevya”

“Mkuu bora ingekuwa mimi lakini sio wale viongozi wa dini na kubwa zaidi ananijua mimi hadi familia yangu unafikiri itakuwaje kama akienda kutoa ripoti kituo cha polisi?”

“Hana ushahidi wala kidhibiti vizuri barua hii imerudi”

“Sawa! nimefanya kosa kubwa sana ila naomba asichukue hatua yeyote ila kwa sasa nimeshindwa tena hiyo kazi”

          Aliondoka na kumuacha mkuu na msaidizi wake humo ofisini kwake lakini kabla Yahaya ajatoka mlango mkubwa wa kutoka nje msaidizi alimuwai na kumsimamaisha.

“Bosi anakuhitaji ili muyamalize mjue mnafanya nini ili kuifanya siri ili lililotokea”

“Siitaji tena maana nimesababisha nimegombana na Imamu wa mtaani kwangu unafikiri uso wangu nauweka wapi?”

“Ndio maana anakwita ili mjue mnafanyaje kumaliza ili tatizo maana sio tatizo kwako hata kwake endapo huyo Imamu akitoa ripoti polisi itakuwaje?”

“Angekuwa analijua ilo angeniweka wazi juu ya huo mpango mapema lakini akaniambia kuwa nimshawishi ili tumtumie katika miadhara juu ya mafundisho ya dini ili kupata Baraka kutoka kwa mungu lakini kumbe sivyo kumbe anataka kumtumia kusafirisha madawa ya kulevya?”

“Yameshatokea mnatakiwa kuyamaliza”

“Nitalimaliza mwenyewe sio na yeye tena”

          Yahaya aliondoka, msaidizi anabaki kumuangalia mpaka anapotea machoni mwake, taratibu anarudi ndani alipofika kwa mkuu anamwambia amekataa.

“Tutajua cha kufanya kila kitu kitaenda sawa!”

**********

          Siku iliyofuata ilikuwa ni siku ambayo sherehe katika kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani, baada ya kila kijana kufanikiwa kurudi salama usalimini kutoka mitaani kuiba pikipiki na kufanikiwa kuiba pikipiki nyingi na kuzidi kuiingizia pesa kampuni hiyo ya Scorpion gereji.

Waliandaa tafrija fupi humo humo ndani ya kitengo chao cha wizi wa pikipiki mitaani, walikunywa na kufurahi, waliokoseana waliitumia siku hiyo kuombana msamaha na kuyasahau yote yaliopita. Yahaya ni miongoni aliekosana na bosi wake Scorpion. walitumia siku hiyo kuombana msamaha na kumaliza tofauti zao.

          Kwa pamoja walikunywa na kufurahi mpaka kila mmoja alilewa hasa hasa bosi ndio alikuwa amelewa sana hadi kushindwa kuendesha gari lake kurudi nyumbani kwake. Aliteuliwa Yahaya ampeleke bosi nyumbani kwake. Bila kipingamizi Yahaya alikubali, akachukua funguo ya gari ya bosi wake akawasha gari, bosi akapanda wakaanza safari ya kuelekea nyumbani kwa bosi wake Scorpion Kijichi.

          Muda wote wa safari bosi Scorpion alikuwa amelala siti ya nyuma katika gari, kutokana na pombe kumzidi sana bosi Scorpion alitapika ndani ya gari. Yahaya ikabidi asimamishe gari maeneo ya hospitali ya Mission. Bosi Scorpion alishuka ndani ya gari na kuanza kutapika, alitumia kama dakika tatu kutapika alipomaliza akaingia ndani ya gari na akamwambia Yahaya aendeshe gari.

          Yahaya akafanya kama alivyoamrishwa na bosi Scorpion lakini Yahaya kabla ajaweka gea ili kuruhusu gari kuondoka ghafla kilitua kitu kizito kichwani kwake kilichosababisha kupata mshtuko hadi anadondokea katika usukani wa gari. Muda huo huo alipata kizunguzungu na kuishiwa nguvu hata gari alishindwa kuendesha. Kutokana na maumivu makali aliyokuwa anayasikia alianza kukoloma kwa sauti huku akijitaidi kuinua kichwa hapo katika usukani wa gari lakini akuweza kutokana akuwa na nguvu kabisa.

          Hapo hapo bosi Scorpion aliinuka kutoka nyuma ya siti ya gari na kusogea hadi alipo Yahaya akavua tai yake na kumzingiriza shingoni na kuanza kumnyonga, aliona haitoshi tai peke yake kumaliza uhai wa Yahaya akatoa sindano ambayo ilikuwa na dawa kabisa kwa jinsi ilivyo ilikuwa imeandaliwa mapema na kumchoma ya shingo Yahaha mpaka kumkatisha uhai wake. Hapo ndio ulikuwa mwisho wa Yahaya wa maisha yake duniani. Bosi Scorpion baada ya kuhakikisha ameshammaliza Yahaya alitoa simu yake mfukoni alipiga.

“Nishamaliza kazi, kama dakika tano nitakuwa hapo”

          Alimtoa Yahaya mbele ya siti ya dereva alipokuwa akamuweka siti ya nyuma, hapo hapo aligeuza gari alirudi alipotoka. Kutokana ulikuwa muda wa usiku, mwendo wa dakika kumi alifika makao makuu ya Scorpion Gereji. Alikutana na msaidizi wake akiwa na watu watatu wenye miili minene waliovalia vazi la suti nyeusi. Haraka haraka waliishusha maiti ya Yahaya katika gari ya bosi Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani, waliingiza katika gari nyingine ndani ya gari hilo iliyowekwa maiti ya Yahaya kulikuwa na rundo la vitabu vya biblia.



          Siku hiyo hiyo saa kumi usiku, kiongozi msaidizi wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani na wavaa suti watatu walitoka hapo makao makuu ya kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani kwa kutumia gari lakini Gari waliyoitumia ilikuwa ndogo, awakuweza kutosha wote, msaidizi wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani aliamua kuitumia pikipiki aliokuwa anaitumia Yahaya kwenda msikitini kwa Imamu Shafii.

          Uzuri wa wa muda huo wa usiku kulikua hakuna foleni wala trafki, ikapelekea walitumia muda mchache kufika Tabata Mawenzi katika msikiti wa Almasjid Tidc, msikiti unaoongozwa na Imamu Shafii. Walipofika hapo msikitini kiongozi msaidizi wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani alibaki ndani ya gari. Walishuka hao wavaa suti watatu waliangalia mazingira ya eneo hilo la msikiti waliona usalama upo wa kutosha. Walishusha maiti ya Yahaya wakaibeba mkukumkuku na kuelekea ndani ya msikiti na mvaa suti mwingine alibeba rundo la vitabu alielekea ndani ya msikiti walipoelekea wenzake.

         

    *************ITAENDELEA IJUMAA IJAYO ************


MAWASILIANO ZAIDI TUCHEKI KUPITIA NAMBA HII KWA KUTUTUMIA HABARI +255682842818        

         

Chapisha Maoni

0 Maoni