KIVULI NDANI YA MWILI { SEHEMU YA TANO}

 Siku ya kwanza ya kuanza kazi ya kuwapangia wezi wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani kwenda kuiba pikipiki ndipo Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani akawaambia wezi wote kuwa wanapoenda katika kazi wasiwaue wanaowaibia pikipiki ili waendelee kununua pikipiki, waibe tena kampuni ikue. Wezi wote walielewa lakini rafiki yake mpelelezi ambaye alikuwa dereva bodaboda mwenzake Segerea aliemleta mpelelezi katika kitengo hicho, alichukia sana huku akiamini ushauri huo wa mpelelezi lakini akuwa na jinsi lazima akubali, bosi ameshasema. Walizingatia walichoambiwa na mpelelezi aliwafundisha jinsi ya kuwapiga ili kuwazimisha bila kuwajeruhi na siraha yeyote.


          Baada ya miezi miwili kupita, Scorpion anapigiwa simu na mtu ambae anamwita mheshimiwa.

"Amefikia wapi mpaka sasa?"

"Mheshimiwa si ulisema mpaka tuwajue wote wanaokijua hichi kitengo ili tupate kuwamaliza wote"

"ndio!"

"Ndio! maana mimi nilikuwa kimya bila kukupa taarifa zozote"

"OK! kwa sasa aina maana tena kuwajua wote, hao walioingia wachukuliwe hatua haraka iwezekanavyo ili kupoteza ushahidi wote"

"Sawa! nitalifanyia kazi"

          Walikubaliana hivyo! Mheshimiwa anakata simu. Mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani anabaki njia panda asijue nini cha kufanya. Mpelelezi  na Muona awakuyajua waliopangiwa wao waliendelea na kazi ya kuwapangia wezi sehemu za kwenda kuiba pikipiki. Wakiwa hapo ofisini walipata nafasi kubwa sana ya kupitia mafaili mbalimbali na kufanikiwa kuona faili lenye majina ya wezi wote, picha za sura zao pamoja na namba zao za simu. 

         Awakuishia hapo walichunguza sehemu tofauti tofauti wanagundua stoo zinazoifadhiwa mabaki ya pikipiki zinazochenguliwa yasiokuwa na kazi na preti namba za pikipiki zinazoibwa mitaani. Baada ya kugundua hayo, walitumia simu ya Muona kupiga picha hizo picha za wezi wote, kupiga picha majina na namba zao za simu, walipiga picha hayo mabaki ya pikipiki stoo na rundo la preti namba na kuzituma kwa O.S.S mkuu wao kwa njia ya mtandao wa whatsApp. O.S.S mkuu wa upelelezi aliziona vitu vyote alivyotumiwa aliwapongeza kwa kazi nzuri. Alikwenda kuifadhi vitu vyote katika faili maalumu katika komputa hapo kituo cha polisi Tabata Shule. Siku hiyo hiyo baadaye, O.S.S alikutana na kiongozi wake ngazi ya juu ya upelelezi R.C.O alimfikishia taarifa hizo. R.C.O alifurahi sana kwa kazi nzuri wanayoifanya vijana wake.


"Hatua nzuri ya mafanikio ya upelelezi, nakuahidi ukifanikiwa hilo lazima upandishwe cheo"

"Nashukuru mkuu"

"Maana umefanya kazi kubwa wewe na vijana wako kuhakikisha unatokomeza uharifu nchini"

"Ni kweli kabisa kwa sababu wanaohathirika na kitengo hichi ni madereva bodaboda"

"Hakika!"

"Sasa lazima tukusanye nguvu kubwa ili kuwatia nguvuni wezi wote na kuteketeza kitengo chote cha uharifu"

"Vizuri sana!"

          Walipanga mambo mengi ya upelelezi ili kuvamia katika hicho kitengo ili kuwatia nguvuni wezi wote.

          Masaa matatu baadaye, tayari ilikuwa saa kumi jioni juu ya alama. Sauti ya adhana ilisikika katika misikiti mbali mbali kuingia katika nyumba za ibada ili kufanya ibada. Mpelelezi na Muona wakiwa hapo ofisini katika kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani walisikia simu ya ofisi inaita. Mpelelezi alinyanyuka kutoka mahali alipokaa na kuanza kutembea taratibu kuelekea mahali simu inapoita. Alipofika aliangalia simu iliyoingia ni namba ngeni, hakuwa na wasi wasi anapokea, aliepiga anamwambia mpelelezi apeleke gari ili akabebe pikipiki.

          Mpelelezi akupoteza muda alimuaga Muona na anachukua gari aina ya haisi ambayo wanaitumia kubeba mapikipiki baada ya kuiba anaelekea alipoelekezwa maeneo ya Buguruni Skita katika viwanja vya mpira. Dakika thelathini na moja baadaye, mpelelezi anafika eneo la Buguruni Skita alisimamisha gari katika jengo kubwa la golofa. Akiwa ndani ya gari alipepesa macho huku na huko bila kumuona mtu. Alishuka katika gari anapiga hatua kusogea katika hilo jengo mara anawekwa chini ya ulinzi kwa nyuma na watu wasiojulikana kumuamuru aelekea ndani ya hilo gorofa. Mpelelezi alitii kama walivyomuamuru hadi ndani ya hilo gorofa lisiloisha lililo maeneo hayo ya Skita karibu na minazi. 


          Baada ya kumfikisha ndani ya hilo gorofa walianza kumpiga mpaka anakua hoi hoi. Akiwa  katika hali mbaya kutokana na kipigo cha hao watu, alisikia sauti ikitoa amri waamue kabisa. Japo alikuwa katika hali mbaya lakini hiyo sauti alihisi sio ngeni masikioni kwake.Alijitaidi kuangalia inaposikika hiyo sauti kwa shida na tabu ili hakikishe anachokihisi ndipo anamuona mtu akiwa katika vazi la polisi lakini alishindwa kumjua ni nani anajitahidi kuangalia uenda anaweza kumjua lakini wapi! mboni za macho yake azikuweza kutoa taswira ya kuona vizuri kutoka alikuwa katika hali mbaya ya kipigo. Aliona msaada pekee wa kumjua mtu huyo ni kumbukumbu zake, alijitahidi kuvuta kumbukumbu alipowai kusikia sauti hiyo lakini pia alishindwa kutokana na hali aliokuwa nayo. Hao wapigaji baada ya kupewa ruhusa ya kuua waliendelea kumpiga mpelelezi hadi mpelelezi hadi pumzi zinakata.

"Ameshakufa tayari!"

          Huyo askari alietoa amri kuuliwa mpelelezi alisogea hadi sehemu walipo hao watu na mpelelezi. Alipofika alimkagua mapigo ya moyo mpelelezi kimya hakuna mdundo wowote wala hakuna pumzi anayosikia kutoka kwa mpelelezi. 

"Vizuri! kazi nzuri"

**********

          Msaidizi wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani akiwa hapo makao makuu ya kitengo cha wizi wa pikipiki akiendelea ya kubomoa pikipiki na kutoa injini mara simu yake iliita. Aliaacha kazi aliokuwa anaifanya anapokea simu. Mtu aliepiga simu alianza kutoa malalamiko muda mwingi amepiga simu katika simu ya ofisini ili gari ije kubeba pikipiki lakini simu inaita bila kupokelewa.

          Msaidizi wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani baada ya kupewa taaria hiyo alienda ilipo simu ya ofisi huku anaongea na huyo mtu lakini alipofika bila kumuona mpelelezi wala Muona. Alikata simu ya huyo mtu anapiga simu ya ofisini ambayo ipo kwa ajiri ya kupokea taarifa za kwenda kubeba pikipiki mitaani zilizoibiwa lakini anapiga mara nyingi bila simu kupokelewa. Alienda moja kwa moja hadi ofisini kwa mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani anamkuta akiwa na Muona.

"Mkuu napiga simu ya ofisi lakini bila kupokelewa sasa sijajua dereva yupo wapi maana vijana wanataka gari kubeba pikipiki"

"Kwani Job ametoka muda gani?"

Mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki alimuuliza Muona.

"Kama lisaa limoja na nusu baada ya kupigiwa simu akabebe pikipiki"

"Ajafika eneo la tukio lolote maana vijana wote wanapiga simu na kutuma meseji wanapiga simu ya ofisi ambayo anayo dereva wa gari lakini aipokelewi"

          Mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani na Muona wote walishangaa, Muona haraka haraka anapiga simu ya mpelelezi lakini inaita bila kupokelewa.

"Atakua wapi sasa"

"Kama apokei simu jaribu kutuma meseji yawezekana yupo sehemu mbaya ila hakikisha unatuma meseji ya kawaida"

"Vijana baada ya kupiga simu aipokelewi walituma meseji lakini hakuna meseji hata moja iliojibiwa"

Mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani alifikiria kama dakika mbili huku anachezea simu kama mtu anaepiga mahesabu.

"Fanya hivi wajulishe vijana wote kila mmoja afanye anavyoweza afike ofisini na hizo pikipiki na hakikisha unawaambia wasitume meseji wala kupiga simu tena katika simu ya ofisini aliokuwanayo Job"

"Sawa! mkuu"

          Msaidizi wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani alitoka humo ofisini kwa mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani aliondoka. Muona muda wote akuwa na amani wala furaha kutokana na mpelelezi, alifikiria nini kimemkuta mpaka apokei simu wala ajibu meseji. Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki aligundua hali hiyo kwa Muona.

"Muona"

Lakini Muona kimya akiwa katika mawazo mazito.

"Muona"

          Mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani alimwita huku akimshtua mkononi ndipo Muona anashtuka kama mtu alietoka usingizini na kuitikia.

"Vipi mbona mawazo mengi?"

"Job"

"Natumaini atakua sehemu salama,yawezekana apokei simu yupo sehemu mbaya si unajua kazi yenyewe hii"

"Bora hata ajibu meseji nipate tumaini"

"Usijari kila kitu kitakua sawa"

          Mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani alichukua simu yake anapiga katika simu ya ofisini aliokuwa nayo mpelelezi lakini simu ikawa aipatikani kabisa.

"Simu aipatikani kabisa"

"Mungu wangu"

Muona alitaka kulia lakini Mkuu wakitengo cha wizi wa pikipiki anamtuliza.

"Sijui kimemkuta nini Job wangu"

          Alichukua simu yake anapiga simu ya mpelelezi anapiga lakini nayo simu aipatikani kabisa, Muona alichanganyikiwa anainuka na kutoka ndani ya ofisi ya mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani. Mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani alimfuata nyuma anamuwai mlango wa kutoka nje.

"Muona unakwenda wapi?"

"Job nahitaji kujua alipo na nini kimemkuta"

"Wapi sasa?"

"I don't know"{Sijui}

Anapiga hatua anaondoka.

"Ni hatari kwako"

          Muona wala akujari alipiga hatua anaondoka na kutoka ndani ya jengo hilo la kitengo cha wizi wapikipiki mitaani. Jengo ilo kwa nje ukiliona unajua ni gereji lakini kumbe ndani inafanyika biashara chafu ya wizi.Mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki akutaka kumfuata tena Muona kuepusha kuvutana vutana mbele za watu. Muona akiwa njiani aliondoka kwa miguu ghafla inakuja gari na kupaki mbele yake, Muona alishangaa, dereva wa gari hiyo mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki alishuka katika gari anasogea alipo Muona.

"Tuungane kwa pamoja kumtafuta Job"

Muona akiwa amemkodolea macho mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani.

"Ingia ndani ya gari twende"

"Wapi?"

Mkuu alifikiria kwa muda mara anatoa simu mfukoni anapiga.

"Mpendwa Lisa"

"Ndio bosi"

"Bila shaka upo ofisini?"

"Ndio"

"Ok! naomba unisaidie kitu kimoja, kuna namba nakutumia uingalie simu ya mwisho kupokea ilikua ya nani na akiwa wapi?"

"Sawa! bosi naomba nitumie ili nikuangalizie"

          Mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani alituma hiyo namba ya ofisini. Muona aligundua mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani alikuwa anaongea na mtu wa makao makuu ya mtandao wa simu lakini akujua ni mtandao upi?.

"Ulikuwa unaongea na muhudumu wa mtandao wa simu?'

"Ndio!"

"Mtandao gani?"

          Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani alimtajia Muona huo mtandao wa simu. Muona alizuga kidogo halafu anaandika katika simu muda huo Scorpion anaoongea na huyo mtu wa mtandao wa simu.

"Nimeshatuma makao makuu ya Tigo namba aliokuwa nayo Job, baada ya muda mfupi watatuambia simu ya mwisho kuongea nayo ya nani na huyo mtu akiwa wapi, tutakapota maelezo hayo tutajua kwa kumtafuta"

Muona alishusha pumzi huku anamwangalia usoni mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani.

"Naomba uingie ndani ya gari"

          Scorpion alimwambia Muona huku anamshika mkono anampeleka, Muona bila kipingamizi anaongoza, Scorpion alimfikisha hadi mlangoni anamfungulia mlango anamuingiza na yeye anazunguruka upande wa pili wa gari. Muona akiwa ndani ya gari amekaa unaingia ujumbe mfupi wa maneno katika simu yake. Alifungua na kuanza kusoma huo ujumbe lakini anashtuka baada kusoma ujumbe huo mfupi wa maneno katika simu yake. NI taarifa mbaya ya kutoka kwa O.S.S mkuu wake wa upelelezi inayomuhusu mpelelezi. 

          Mpaka dakika hiyo anapata ujumbe huo mfupi wa maneno, mpelelezi yupo hospitali ya Amana wodi ya maututi ICU. Akujua nini afanye kwa muda huo kwa sababu yupo na mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani. Muona alitafakari ataondoka vipi na kumuacha mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki ili aende hospitali ya Amana.  Mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani anaingia ndani ya gari kabla ajawasha gari ili waondoke simu yake inaita anapokea.

"Samahani kwa kusubiri"

"Usijari"

"Sasa nimeangalia hapa kuna meseji zilizotumwa na hii namba yako ya kutoa taarifa ya kuwaita watu waje ofisini, halafu masaa kumi tisa mbele simu ya kwanza alipigiwa ya kuitwa Buguruni  Skita ya kwenda kubeba pikipiki, nyingine alitumiwa meseji akiitwa sehemu tofauti tofauti akabebe mzigo na alipigiwa simu nyingi sana, nyingine zikirudia kupiga lakini akuweza kupokea"

"Vizuri! kwa hiyo kuna simu ya kwanza iliopigwa aliitwa Buguruni Skita kwenda kubeba pikipiki"

"Ndio bosi"

"Hiyo simu kutoka eneo gani na namba gani?"

"Namba 0764 07 07 97, eneo alilokuwa huyo mtu aliokuwa anapiga simu ni hapo hapo Buguruni Skita"

"Nashukuru! kazi njema, kama kuna kitu kitakwama nitakutafuta ili unipatie ufumbuzi ila nitumie hiyo namba"

"Usijari bosi"

          Simu inakatwa, Lisa mfanyakazi wa mtandao wa simu, muda huo huo anatuma hiyo namba. Mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani anachukua hiyo namba anaipiga katika simu yake anagundua ni namba ya mtu ambae aliempa taarifa ya kuingia mpelelezi katika kitengo chake cha wizi wa pikipiki mitaani na anaempa taarifa zote kutoka serikalini. Mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki alipogundua hilo imani yake ilisaidiki kuwa kuna kitu amekifanya huyo mheshimiwa kwa mpelelezi. Alitaka kupiga simu ili aongee nae lakini anashindwa kwa sababu yupo karibu na Muona, alibaki njia panda asijue nini cha kufanya. Muona aligundua mabadiliko hayo kwa mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani lakini akujua kwanini amekuwa hivyo ghafla, akataka kujua ukweli uliofichika.

"Umeambiwaje?"

          Mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani alikuwa kimya kama dakika mbili baada ya kuulizwa ndipo anaongea.

"Mtu wa mwisho kuongea nae sehemu alipokuwa hadi anapiga simu ni tofauti na sehemu alipoenda Job baada kupigiwa simu"

"Kwa sehemu zote si wamekutajia?"

"Ndio!"

"Wapi na wapi?"

"Aliepiga simu alikuwa Buguruni na alipoenda Job baada ya kupigiwa simu ni Makuburi"

"Kwa hiyo tunaanzia wapi"

"Hata tukienda tutasumbuka bila kujua eneo alipo kwa hiyo lazima tutumie Gprs ili kujua sehemu alipo"

          Muona aliposikia kuhusu kutumia Gprs ili kujua sehemu alipo mpelelezi alipata wasi wasi kuwa mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani anaweza kugundua mpelelezi yupo hospitali ya Amana hivyo anaweza kugundua mpelelezi ni askari. Alitafakari cha kufanya ili mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani asitumie Gprs kumtafuta mpelelezi sehemu alipo maana simu yake na simu ya ofisi anazo mpelelezi.

"Ila hii kazi nitaifanya nikiwa mwenyewe maana ina mzunguko mrefu"

          Mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani kama alikuwa katika mawazo ya Muona, Muona baada ya kuambiwa hivyo kimoyo moyo alifurahi sana ili aondoke aende hospitali Amana ili akazichukue simu zote na kuzitoa hapo hospitali ili asigundulike mpelelezi kama yupo hospitali ya Amana.

"Sawa! aina shida naomba unipeleke na gari hadi Tazara"

"Sio uende ofisini ili nikirudi nikuambie kilichojiri"

"Hapana! sipo sawa nahitaji nikapumzike hivyo utanipigia simu baada ya kufanikiwa"

"Ok!"

          Mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani aliwasha gari wanaondoka. Mwendo wa dakika kumi wanafika Tazara kutokana na foleni ya kutoka vetinary hadi tazara. Baada ya kufika Tazara mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani alimpa Muona elfu hamsini, Muona alipokea huku akishukuru. Baada ya kuagana Muona alishuka katika gari na mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki aliondoka na kuelekea mjini njia ya moja kwa moja kuelekea Posta. Muona alisimama hapo Tazara hadi akahakikisha gari ya mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani inapotea machoni mwake. Baada ya kuhakikisha imepotea machoni kwake gari ya mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani, alisimama hapo kama dakika kumi.

          Dakika kumi na moja, alipanda pikipiki hadi vingunguti, alipofika vingunguti alishuka anamlipa huyo dereva pikipiki anaachana nae. Alisimama hapo hadi huyo dereva pikipiki anaondoka. Alipohakikisha kashafika mbali anachukua pikipiki nyingine hadi vingunguti kwa perapera anashuka anapanda daradara inayoelekea Mnazi Mmoja.

          Mwendo wa nusu saa, anafika hospitali ya Amana, anashuka katika daradara anaelekea ndani ya hospitali ya Amana. Anakutana na O.S.S mkuu wake wa upelelezi, lakini kabla ya yote hata kupewa taarifa juu ya mpelelezi, Muona alimwambia mkuu wake wa upelelezi O.S.S ampeleke wodi aliolazwa mpelelezi. O.S.S mkuu wa upelelezi alimpeleka Muona hadi wodi aliolazwa mpelelezi. Walipofika, Muona alimfunua shuka la wagonjwa alilofunikwa mpelelezi lakini alichokiona alikata tamaa ndipo anamuuliza mkuu wake.

"Nguo za Job zipo wapi?"

"Nahisi zimeifadhiwa na madokta baada ya kumbadilisha nguo kutoka,nguo zake zilitapakaa damu"

"Madokta wao si ndiyo waliombadilisha nguo?"

"Ndio!"

"Awakuwapatia simu mbili?"

"Hapana! hata na sisi ndiyo tulioenda kubeba mwili wake eneo la tukio lakini atukumkuta na kitu chochote mfukoni"

Muona anafikiria kwa muda.

"Kuna nini?"

O.S.S mkuu wake wa upelelezi aliuliza.

"Simu moja ya kile kitengo cha wizi wa pikipiki na nyingine ya Job sasa nahofia wanaweza kuitafuta kwa Gprs wakagundua sehemu alipo Job"

"Kweli! lakini kwakuwa hana simu aiwezi ikawa hivyo"

          Muona anaelewa ndipo anauliza kuhusu mpelelezi imekuwaje hadi yupo katika hali hiyo, ndipo O.S.S mkuu wake wa upelelezi anamwambia mpelelezi amepigwa na watu wasiojulikana hadi kufika hapo hospitalini ni msaada wa msamalia mweme aliekwenda katika jengo la gorofa hapo buguruni Skita kwa ajiri ya kufanya mazoezi katika ilo jengo.

          Muona anakumbuka maelezo ya Scorpion mkuu  wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani anagundua amemdanganya, alipomwambia aliepiga simu alikuwa Buguruni na alipoenda mpelelezi baada ya kupigiwa simu ni Makuburi. Moja kwa moja alihisi kitu kutoka kwa Scorpion ndipo alipomuuliza O.S.S.

"Matatizo hayo yamemkuta akiwa peke yake au na watu wengine"

"Akiwa peke yake'

          Ndipo hapo anagundua kuwa mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki atakua anajua waliohusika na kumpiga mpelelezi kwa sababu simu aliopigiwa mpelelezi hadi kwenda huko Buguruni Skita ni simu ya ofisini. Aliempigia hadi kumwita huko anaijua hiyo simu ya hapo ofisini katika kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani kwa hiyo ni muhusika wa hapo hapo katika kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani. 

          Kama angekua sio muhusika au aijui hiyo namba ya hapo katika kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani angepiga katika namba ya mpelelezi lakini mpaka amepiga katika namba ya kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani, aliehusika na kumpiga mpelelezi mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani anamjua na anatoka hapo hapo katika kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani.

"Mkuu tayari mambo yameshaharibika, sijui nifanye nini?"

"Kwa nini Muona?"

"Watu waliompiga Job ni kwa lengo la kumuua kwa hiyo hata mimi nitakua hatarini kwa sababu  katika kile kitengo cha wizi wa pikipiki wameshagundua kama mimi na Job ni wapelelezi"

"Kwa hiyo unataka tufanye nini?"

"Ni kuwatia nguvuni kabla awajachukua maamuzi juu yangu"

"Ok! mimi nakusikiliza wewe tu"

          Walikubaliana kuvamia katika kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani na kuwatia nguvuni wezi wote na kuwafikisha katika mikono ya sheria ili kuwafungulia mashtaka. Baada ya kukubaliana hayo kwa usalama kwa upande wa mpelelezi wanamuhamisha mpelelezi kimya kimya hospitari hiyo ya Amana wanampeleleka hospitali ya Lugalo. Ilikuwa ni siri ya Muona na mkuu wake wa upelelezi O.S.S.

    Hospitali hiyo ya Lugalo mpelelezi aliendelea kupatiwa matibabu. Muda wote alikuwa chini ya uangalizi wa madaktari kwa kupatiwa matibabu ili kuhakikisha wanaokoa maisha yake. Baada ya Muoana kuhakikisha mpelelezi yupo sehemu salama na anaendelea na matibabu, siku hiyo hiyo baadaye, alienda katika kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani hadi ofisini kwa mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani kwa lengo la kuweka mambo sawa ili kuwatia nguvuni wezi wote.

Lakini alipofika karibu na mlango wa kuingia ofisini kwa mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani anamsikia Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani anaongea na simu, maongezi yake ya kuomba msamaha. Muona akuweza kuelewa msamaha anaouomba wa nini, haraka haraka aliandika katika simu yake siku, tarehe, mwezi, mwaka na muda huo mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki anaongea na simu. Baada ya kumaliza kuandika alifungua mlango anaingia ofisini kwa mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki bila kupiga hodi.

na anamsikia anauliza kwa mshangao.

"Akufa?"

          Ndilo swali alilolisikia Muona anatamka mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani, mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani alishtuka baada ya kumuona Muona anaongea kwa wasi wasi huku akichanganya la nyuma mbele la mbele nyuma.

"Ajari akitibiwa mbaya atapona"

          Muona anakaa katika kiti. Mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki anakata simu anaiweka simu yake katika ndroo.

"Karibu Muona"

"Ahsante!"

"Ulifanikiwa Gprs?"

"Yeah! Gprs inasoma eneo la Lugalo"

"Lugalo?"

Lisa aliuliza kwa mshangao.

"Ndio! inaposoma system ya simu"

"System! system ya simu kwa maana Gprs inaonesha simu aliokua nayo Job ipo Lugalo au Job yupo Lugalo"

"Kama system ya simu inasoma katika Gprs simu ipo Lugalo basi hata Job yupo Lugalo"

          Muona alishtuka baada ya kuambiwa hivyo, ghafla mapigo ya moyo yalibadilika na kudunda mara mbili yake.

"Ok! sasa umechukua uhamuzi gani baada ya kugundua hayo?"

"Tulifika hadi Lugalo lakini ndani ya hospitali ya Lugalo, tulishindwa kuingia kwa sababu sijajua Job mpaka yupo Lugalo hospitali kwa nini na kipi kimemfanya yupo ndani ya hospitali maana ni mazingira ya kutatanisha"

"Ni kweli ila ngoja nifatirie mimi nitajifanya kama mume wangu, naweza kufahamu ukweli"

"Ni hatari kwako"

"Kwa nini?"

"Sote atujui kipi kimemkuta hadi yupo hospitali ya Lugalo"

"Vijana wote si wamerudi salama jana kutoka katika kazi"

"Ndio"

"Basi hakuna baya yawezekana ni ajari tu"

          Mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki akuwa na la kusema alibaki kimya anamwangalia Muona, Muona anaaga anaondoka. Mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki alibaki njia panda juu ya Muona na mpelelezi nini afanye maana tayari amesemwa na huyo mtu anaemuita Mheshimiwa na anaempa taarifa kutoka serikalini kwa kukaa na mpelelezi na Muona bila kuwachukulia hatua wakati wao ni wapelelezi wamejiunga katika hicho kitengo cha wizi wa pikipiki kwa lengo la upelelezi.

**********

          Safari ya Muona iliishia makao makuu ya kituo cha polisi anapofanyia kazi anakutana na mkuu wake wa upelelezi O.S.S anamwambia mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani amegundua mpelelezi yupo hospitali ya Lugalo kwa matibabu.

"Nani amewapa taarifa hizo"

"Gprs"

"Gprs?"

"Ndio"

"Kivipi?"

"Kuna simu ya ofisi katika kile kitengo cha wizi wa pikipiki aliondoka nayo Job kabla ajapata tatizo ndio hiyo wanayotumia kujua sehemu alipo"

"Sio kweli kwa sababu kama nilivyokwambia Job tumemkuta hana simu wala kitu chochote nahisi wasamalia waliomsaidia ndio wamechukua vitu hivyo"

"Kweli?'

"Ndio! kwanini nikudanganye"

Muona anafikiria.

"Akili ya ziada inahitajika"

"Kwanini?'

"Job amjamkuta na simu mfukoni wala kitu chochote, lakini Gprs imesoma yupo Lugalo sasa kipi hapa kipo sahihi?"

Kila mmoja anafikiria kwa kina, ndipo Muona anamwambia mkuu wake wa upelelezi.

"Ndio maana nimesema akili inahitajika la sivyo wote tutaangamia kwa ajiri ya hii kesi"

          Mkuu wa upelelezi O.S.S alibaki kimya bila kuwa na cha kuongea. Muona aliaga anaondoka, njia nzima alitawariwa na mawazo mengi ndipo anakumbuka walivyomuhamisha mpelelezi kumtoa hospitali ya Amana kumpeleka Lugalo ni siri ya yeye na O.S.S, sasa iweje Gprs isome Lugalo wakati amesema wamemuokota mpelelezi awakumkuta na simu wala chochote. Sasa Gprs imesomaje Lugalo na mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani amejua kama mpelelezi yupo hospitali ya Lugalo. Alishindwa kuelewa ukweli wa mambo hayo ndipo  imani yake iLIsadiki kuwa O.S.S mkuu wake wa upelelezi anashirikiana na waarifu. 

**********

          Siku iliyofuata Muona alikwenda hospitalini Lugalo na kukuta mpelelezi bado hajitambui ingawa mapigo yake ya moyo yalikuwa yakipiga vizuri. Hakuwa na matumaini ya mpelelezi kupona. Muona alilia sana, daktari anaemuhudumia mpelelezi alimbembeleza bila mafanikio yeyote.

"Usilie sana, hii yote ni mipango ya Mungu"

"Sawa daktari, lakini inauma, wenyewe wanatupa kazi tuondoe uhalifu lakini hao hao ndio wanatuzuru ili kuficha uhalifu"

          Kwa wiki nzima, Muona aliendelea kuwa katika hali hiyo na madaktari walidai angekuwa hivyo kwa siku nyingi, wakati ubongo wake ukipona taratibu. Walitoa jibu hilo baada ya kumfanyia operesheni na kutoa damu iliyoganda kichwani mwake. Kwa Muona siku zote zilikuwa huzuni tupu, alilia usiku na mchana mpaka machozi yakamkauka. Mwisho wauguzi walimzuia kuingia wodini kwa sababu kila alipomwona mpelelezi kitandani akiwa amefungwa na mashine ya kuhemea alilia zaidi. Kila siku  alifikiri ni kwa jinsi gani angeweza kumwamsha mpelelezi kutoka katika usingizi mzito wa mauti, aliolala.

          Mawazo hayo yalimsababishia kukumbuka kitu ambacho aliamini kingemuamsha mpelelezi. Badala ya kutumia madawa, alikumbuka kuwa mpelelezi alikuwa akiwa ofisini chumba cha upelelezi  kituo cha polisi alikuwa anapenda kuvua vitu na kubaki na soksi. Muona alikuwa anamwambia kuwa avae viatu vyake vinatoa harufu lakini mpelelezi alikuwa anamwambia Muona kuwa viatu vyake avitoi harufu na kumthibitishia kwa kumnusisha lakini Muona alikuwa anamtekenya unyayoni. Mpelelezi akitekenywa hata kama alikuwa anafanya kazi gani, aliacha na kushtuka na haraka alivaa viatu vyake.

"Nikimtekenya tu, naamini ataamka!"

          Aliwaza Muona kisha akasogea hadi katika miguu ya mpelelezi akafunua shuka aliofunikwa ambako alianza kushika nyayo zake za miguu na kuanza kumtekenya taratibu mithili kama anamfanyia masaji. Alimtekenya unyayoni hadi katika vidole vyote vya miguu, taratibu msisimko ulianza kumsisimua mpelelezi.

"Haah! Katabasamu!"

          Alipiga kelele Muona baada ya kumuona mpelelezi ametabasamu na meno yake kuonekana.Aliruka juu na kushangilia ikabidi aongeze kumtekenya zaidi ili kumzindua mpelelezi kutoka katika usingizi wa kifo. Sauti ya Muona iliwafanya madaktari waliopo ofisini walikuja mbio mbio hadi chumbani na kushuhudia hali ya mpelelezi. Hakuna aliyekuwa tayari kuamini kwamba, kweli mpelelezi alitabasamu, ilikuwa ni kama ndoto! Muona aliruka akishangilia na kujiona mshindi, wazo lake lilikuwa limezaa matunda. Kumtekenya kumemfanya mpelelezi kurejea duniani.

          Aliongeza kumtekenya. Aliamni kwamba badala ya kutabasamu angenyanyuka kitandani na kukaa na huu ndio ungekuwa mwisho wa mateso na maumivu yake. Madaktari waliamini bila ya Muona kutoa wazo la  kumtekenya, mpelelezi asingetabasamu. Mpelelezi alionyesha tabasamu lake vizuri. Vishimo katika mashavu yake vilionekana na meno yake meupe yaliong'ara na kupangwa vizuri yalionekana.

          Ilikuwa furaha kubwa mno kwa Muona ndani ya chumba hicho. Madaktari walimwambia Muona atoke nje, Muona alitii lakini muda wote akimuomba mungu mpelelezi afumbue macho. Madaktari wote walianza kumpa huduma ili kumfanya aweze hata kufumbua macho ili awe katika hatua nyingine nzuri zaidi, pengine angekuwa hata na uwezo wa kuongea maneno machache.

          Walijitahidi kwa uwezo wao wote, mpelelezi alianza kuchezesha kidole cha mkono hatimae mpelelezi alitingisha mwili wote ndipo hapo tumaini lingine la kuinuka mpelelezi lilionekana kwa mpelelezi. Siku hiyo hiyo baadaye, jitihada za kuokoa uhai wa mpelelezi ziliwezekana na mpelelezi aliweza kuzinduka kutoka katika usingizi mzito wa kifo. Muona alirukaruka kwa furaha, hadi machozi yalimtoka! Alijisikia yu kama malaika kwa kuweza kumzindua mpelelezi kutoka katika usingizi mzito.Hakuamini kuwa tayari alikuwa amezinduka mpelelezi.

**********

          Baada ya siku kadhaa, mpelelezi alipona kabisa na alirudiwa na afya yake kama zamani. Alikukutana na Muona, O.S.S mkuu wa upelelezi kituoni na R.C.O mkuu wa upelelezi ngazi ya juu kila mmoja anampa pole kutokana na kuumwa kwa muda mrefu. Walijadiri juu ya kitengo cha wizi wa pikipiki juu ya kuvamia ili kuwatia nguvuni wezi wote na kusambaratisha hicho kitengo. Walipanga kwa pamoja siku ya kuvamia lakini mpelelezi anaomba iwe siri hata askari watakao tumiwa washtukizwe.

“Kwanini iwe ivyo”

Ni swali lililoulizwa na R.C.O mpelelezi ngazi ya juu.

"Kwa sababu, nikiwa nimetekwa nimeshapigwa nipo hoi hoi nilisikia sauti ya mtu ambae sauti naijua kabisa lakini sikumbuki ni sauti ya nani?”

“Aukuweza kumuona sura?”

“Nilijitaidi kuangalia ili nione sura yake, lakini sikuweza kumuona vizuri kwa sababu nilikuwa hoi hoi halafu alikua mbali na nilipokuwa mimi ila alikuwa amevaa vazi la polisi”

Wote walishtuka, mpelelezi anaendelea kutoa maelezo la tukio lake.

“Ili tukio niliwai kuliota na limenitokea kweli sasa kuna asilimia mia moja kuna askari wanatuzunguruka kwa hiyo tusipokuwa makini yatatokea mengine yatabaki majina”

 “Kama ni hivyo wapelelezi wote wanaojua hii kesi waitwe waifanye hii kazi washirikiane na wewe kama miongoni wa hao wapelelezi yupo huyo msaliti ni rahisi kumjua na kumtia nguvuni”

          R.C.O mkuu wa upelelezi ngazi ya juu alimwambia mpelelezi lakini O.S.S mku wa upelelezi wa kituo anadakia haraka haraka.

“Aina haja ya kuita wapelelezi wote maana wapo mbali kikazi, hata hivyo kazi ishaisha tunachopanga siku ya leo ni lini kuvamia ili kuwatia nguvuni maana orodha yote ya watuumiwa wa hicho kitengo wanajulikana na wanapokaa na picha zao tunazo”

“Kazi nzuri! wote majina yao mnayo?”

“Ndiyo tunayo”

          O.S.S alifungua komputa na kuanza kumuonesha, R.C.O mkuu wa upelelezi ngazi ya  juu picha moja baada ya nyingine.

“Kwa hiyo mkuu kazi imeisha kilichobaki kuvamia na kuwakamata mmoja baada ya mwingine ila atujapanga siku ya kuvamia”

“Sawa! ila siku ya kuvamia mnijulishe”

“Hakuna shida”

          Wanamaliza kikao chao kila mmoja anaondoka katika majukumu yake ya kikazi lakini Muona na mpelelezi waliondoka kwa pamoja, wakiwa njiani.

"Ukweli wazi japo tumepanga mpango wa kuvamia kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani lakini sina imani na mkuu"

"O.S.S au R.C.O?'

"Mkuu wetu ambae kila kitu tunachopanga na kukifanya tunamwambia yeye"

"Kwa nini auna imani nae?"

"Wakati unaumwa ilikua siri kukutoa hospitali ya Amana kukupeleka hospitali ya Lugalo sasa mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani amefahamu sasa unatakiwa ujiulize je kaambiwa na nani"

          Mpelelezi alishtuka baada ya kupewa taarifa hiyo ndipo anamuuliza tena Muona, Muona anarudia maelezo mwanzo hadi mwisho.

"Nani kamwambia?"

"Hata mimi nilijiuliza nani kamwambia kama wewe unavyoniuliza mimi?"

"Unachosema ni kweli au unatengeneza mazingira niamini O.S.S anashirikiana na watu baya"

"Najua uwezi kuamini, hata mimi sikuweza kuamini ila ukweli ndio huo"

"Hakuna! kitu kama hicho Muona, O.S.S awezi kufanya hivyo hata mara moja"

"Utakapomshuhudia kwa macho yako ndiyo utaamini"

"Muona sitaki kuamini sauti ninayoifananisha nikiwa napigwa ni ya O.S.S"

"Funika kombe mwana haramu apite"

          Muona aliongoza njia anatembea kusogea kituo cha daradara Tabata Shule, mpelelezi anafuata nyuma,wanafika kituoni wanapanda gari la temeke wanaondoka. Safari yao iliishia katika kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani. Walipofika hapo makao makuu ya kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani kila mwanachama alipomuona mpelelezi anampa pole huku akimwambia ndio majukumu ya kikazi maana raia wana hasira kali. Mpelelezi imani yake ilisadiki kuwa taarifa imefika hapo makao makuu matatizo yaliomkuta na kila mwanachama alijua amepata matatizo kutoka kwa raia wenye hasira kali ndio maana wanampa pole.

          Alishukuru pole zote alizopewa na wezi wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani, baada  ya muda kumaliza kuongea nao mawili matatu, aliongozana na Muona walielekea moja kwa moja ofisini kwa Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani. Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki alipomuona mpelelezi alifurahi sana na anampa pole kwa matatizo yaliomkuta huku akijifanya ajui chochote na kumuuliza ilikuwaje. Mpelelezi alihadithia ilivyokua mwanzo hadi mwisho lakini anasema akuweza kuwafahamu waliomfanyia yote hayo. Mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki anamwambia mpelelezi kwakuwa amepona amshukuru mungu hayo mengine amuachie mungu.

          Masaa mawili baada ya mazungumzo kati ya mpelelezi, Muona na Scorpion mkuu wao wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani wanatoka ofisini kwake wanaenda kuendelea na kazi kama kawaida ya kuwapangia kazi wezi wa pikipiki mitaani. Ujio mpya na wa kishindo wanaweka mazingira ya kuwatia nguvuni wezi wote wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani ili kukiteketeza hicho kitengo chote kwa sababu wameingia katika kitengo hicho ili kumjua muuaji wa dereva pikipiki alieuliwa Segerea kwa kuchinjwa kichwa.Endapo wakimjua huyo itakua rahisi kumjua mtu aliehusika katika tukio la Imamu Shafii na dereva bodaboda Tabata Mawenzi kwa sababu pikipiki iliotumika ni moja.

          Siku ya siku ilifika, walianza kumpigia simu mwizi mmoja mmoja wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani na kuupa taarifa ya kikao na kukutana katika bar moja maarufu katika wilaya ya temeke inayoitwa Sugar Rey ili kujadili utendaji wa kazi na mambo mengine ya maendeleo kuhusu kitengo chao cha wizi wa pikipiki mitaani. Kila mwizi alipopata taarifa hiyo aliahidi kufika. 

          Dakika mia moja na kumi baadaye, kila mwizi wa pikipiki aliyopata taarifa ya kikao alifika katika hiyo bar Sugar Rey wanaanza kikao. Ghafla na bila kutegemea, walishtukia gari la polisi linafika likiwa na askari wengi wanawaweka chini ya ulinzi. Wezi wote walipatwa na mshtuko wa ajabu na kujikuta wakiweka mikono juu kutii sheria bila shuruti. Ilikuwa ni ngumu kukimbia wala kufanya chochote kwa sababu askari walijiandaa na siraha za moto. Walikamatwa wezi wote na mpelelezi walijifanya kama awamtambui na kumjumuisha nao. Waliingizwa katika gari la polisi kubwa aina ya Leland na kupelekwa kituo cha polisi Tabata Shule. Japo ilikua ni Wilaya mbili tofauti, walipelekwa kituo cha Tabata Shule. Walipofikishwa kituoni waliwekwa sero tofauti tofauti na mpelelezi aliachiwa. 

          Yaliyotokea nusu saa baadaye, alitolewa sero mwizi mmoja mmoja wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani na kufanyiwa mahojiano, mahojiano yaliambatana na kipigo kikali ili kusema wanaoshirikiana nao, matukio mangapi walioyafanya, pikipiki walizoiba na mauaji waliyoyafanya na maeneo waliofanya hayo matukio. Kila mwizi aliehojiwa alisema ukweli wote kutokana na mateso makali, ndipo mmoja anasema alifanya tukio maeneo ya  Tabata Segera na mwenye pikipiki akamchinja shingo. O.S.S baada ya kusikia tukio ilo na analijua ambalo ni tukio lililotokea Tabata Mawenzi wanamshikiria huyo jamaa na wanajua ndie aliehusika katika hilo tukio.

         

         *************ITAENDELEA IJUMAA IJAYO ************


MAWASILIANO ZAIDI TUCHEKI KUPITIA NAMBA HII KWA KUTUTUMIA HABARI +255682842818        

Chapisha Maoni

0 Maoni