WAHAMIAJI HARAMU 62 WAKAMATWA MKOANI DAR


Ofisi ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam imekamata wahamiaji haramu 62 kutoka Burundi katika msako uliofanyika usiku wa tarehe 23/03/2026.

 Wahamiaji hao walikamatwa maeneo ya Jagwani, Kata ya Kariakoo, Wilaya ya Ilala, chini ya uongozi wa Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji Fatuma Suleiman.

 Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Uhamiaji Vicent Haule amesisitiza umuhimu wa kufuata taratibu za kuingia na kuishi nchini kwa mujibu wa sheria.


Idara ya Uhamiaji itachukua hatua za kisheria dhidi ya watu wanaowahifadhi au kuwapa kazi wahamiaji haramu kinyume na utaratibu.

 SACI Haule amewaomba wananchi kutoa taarifa za wahamiaji haramu kupitia ofisi za Uhamiaji Wilaya.

Chapisha Maoni

0 Maoni