Gari la polisi liliendeshwa kama linawai eneo ambalo limevamiwa na majambazi na kufika ndani ya dakika chache makaburini. Walikuta mchungaji ndio anaifanyia sala maiti ya Imamu Shafii. Mashekhee na askari walishuka katika gari la polisi haraka haraka walisogea hadi sehemu ya kaburi na kutoa maelezo juu ya maiti hiyo kwa sababu maiti hiyo wanayozika sio maiti ya ndugu yao imechanganywa kwa sababu ya kufanana majina na ajari moja ya pikipiki.
Japo na kutolewa maelezo yaliojitoshereza lakini awakuweza kueleweka mbele ya wakulya hao waliotawaliwa na majonzi ya kufiwa na ndugu yao. Mashekhee na askari walitoa amri ya kuzuia taratibu za mazishi lakini wakulya hao ilikuwa ngumu kuelewa amri hiyo ndipo hapo unapotokea kutoelewana.
Ulitokea ugomvi mkubwa, askari wanawatuliza lakini inakuwa ngumu kwakua wakulya walikuwa wengi. Muda huo wote daktari Mbaga alikuwa pembeni asijue nini cha kufanya ili aupate mwili wa Imamu Shafii ili kukamilisha agizo alilopewa na Kivuli cha Imamu Shafii. Baada ya ugomvi kuwa mkubwa askari walipiga risasi angani, kitendo cha kupiga risasi juu ndipo kila mkulya alikimbia njia yake.
Mashekhee waliona hiyo ndio nafasi yao ya kuchukua maiti ya Imamu Shafii na kuondoka nayo. Walianza kuitia maiti katika jeneza ili kuiingiza ndani ya gari la polisi lakini kabla awajafanikiwa zoezi lao ghafla wanaume wa kikulya kila mmoja alikuwa anatokea njia yake mkononi akiwa amebeba panga, shoka na kisu alisogea ilipo maiti huku anaongea kilugha, maneno waliokuwa wanaongea mashekhee na askari awakuweza kuelewa walikuwa wanamaanisha nini?.
Kabla hao wanaume wa kikulya awajafika walipo mashekhee wakitoa maiti ya Imamu Shafii katika sanduku ghafla kikasikika kishindo kizito kikiambatana na kimbunga kikali pale pale daktari Mbaga alipoteza fahamu ndio ilikuwa manusura yake. Alipokuja kupata fahamu alijihisi kama mtu ambae amenyeshewa na mvua kwa maana kuwa nguo zake zote zilikuwa zimeloa alipojitizama vizuri aligundua kuwa akunyeshewa na mvua bali zilikuwa damu ambazo zilitapakaa katika nguo na mwilini.
Hapo ndipo alipoanza kuingiwa na hofu na kutafakari kwa makini huku akipepesa macho huku na huko eneo lote alipokuwa lakini akuweza kujua ni eneo gani, kafikaje na nani kamleta eneo ilo wakati yeye mara ya mwisho anakumbuka alikuwa makaburini Kitunda kufatilia maiti ya Imamu shafii , sasa hapo alipo ni wapi?
Lilikuwa ni fumbo lililotanda mawazoni mwake alishindwa kulipatia ufumbuzi. Lakini anapopepesa macho huku na huko aliona mifurushi mingi imewekwa katika meza imefunikwa shuka na mifurushi mingine imewekwa katika mifuko mikubwa ya lailoni. Alitaka kujua mifurushi hiyo ya nini ndipo aliposogea katika moja ya furushi lililokaribu yake. Taratibu alifungua anaona mwili wa binadamu ukiwa umevunjika miguu, mikono, na tumbo lote limechanika vitu vilivyo ndani ya utumbo vinaonekana, damu imeganda imekuwa mpaka nyeusi.
Aliogopa sana daktari Mbaga, alishindwa kujua eneo ilo ni wapi lakini alipopepesa macho huku na huko ndipo alipoona kibao kimeandikwa MOCHWARI akuamini anachokiona, imani yake ilisadiki kuwa yupo katikati ya ndoto ya kutisha lakini alipogundua akuwa katika ndoto wala usingizi mzito alijawa na hofu, kuona akiwa katika chumba cha kuifadhia maiti Mochwari. Alifikiria sana kwanini amewekwa Mochwari wakati yeye ni mzima.
Alishindwa kuelewa ukweli wa mambo hayo, alikumbuka mara ya mwisho tukio lilivyokuwa, alitaka kujua ni yeye peke yake ndio kawekwa huko Mochwari au na wale wote waliokuwa katika eneo lile la makaburi ususani mashekhee wanaofatilia maiti ya Imamu Shafii na Askari.
Ndipo alipoamua kufungua mfuko mmoja baada ya mwingine kuona maiti zilizokuwa ndani lakini cha ajabu asilimia kubwa ya wale wanaume wa kikulya wameuwawa kikatiri ndipo alipogundua kuwa yeye aligundulika amekufa ndio maana amejumuishwa kuwekwa Mochwari. Alikulupuka na kuanza kutaka kukimbia huku akiomba msaada lakini aikusaidia chochote kwani mlango wa mochwari ulikuwa umefungwa sauti yake ilikuwa aisikiki. Alijitaidi kadri ya uwezo wake kuomba msaada kwa kugonga mlango lakini ilikuwa ngumu kupata msaada na ukichangia baridi kali la humo mochwari inapelekea kuishiwa nguvu na kudondoka chini na kuzimia papo hapo.
*********
Akuweza kujua muda gani aliochukua hadi fahamu zake kumrudia lakini alisikia minong’ong’ono ya watu wakiongea kuwa yule mgonjwa anaendelea vizuri anajitaidi kutaka kuamka ili ajue maala alipo ni wapi sehemu salama au si salama kwake lakini anajikuta anashindwa kuinuka na kusimama huku akijiona kichwa chake kimetawariwa na kizunguzungu ndipo anapoamua kuita.
“Jamani msaada?”
Alikuja nesi akimuuliza kwa upole.
“Unataka nini?”
Daktari Mbaga aliongea kwa tabu sana.
“Naomba nisaidie niinuke nikae kitako”
Nesi alimsaidia daktari Mbaga anamuinua lakini akiwa anainuliwa daktari Mbaga anagundua kuwa amefungwa pingu. Alihisi uenda wale askari waliokuwa katika kufatiria maiti ya Imamu Shafii kule makaburini ndio waliomkamata huku akitafakari wamemkamata akiwa katika mazingira yapi? wakati yeye alikuwa aonekani machoni mwa watu lakini anajipa moyo kuwa kosa lake litakuwa lile lile.
Lakini alijiuliza hapo alipo ni wapi alipojaribu kutazama kwa makini huku akitafakari aligundua kuwa yupo hospitari japokuwa akuweza kugundua ni hospitari gani alipo. Nesi alimaliza kumuweka vizuri anaondoka zake kwenda kuwasaidia wagonjwa wengine.
Muda huo huo, anakuja nesi mwingine akiwa ameshika dripu ya maji na dawa za vidonge vya aina tofauti. Nesi alianza kupita kitanda kimoja na kingine na kumpa dawa mgonjwa mmoja baada ya mwingine. Alipofika katika kitanda cha daktari Mbaga alimwambia masaa mawili tayari yashapita kwa hiyo anyooshe mkono wake ambao aukuwa na pingu ili amtundukie sindano ya dripu ya maji kwa maana alikuwa hana nguvu. Daktari Mbaga alikubari kufanya kama alivyoambiwa na nesi alimtundukia dripu nyingine. Baada ya kumaliza kumtundikia hiyo dripu aliondoka zake.
Masaa yalikatika akiwa hapo kitandani amelala huku akiwa amefungwa pingu yupo chini ya ulinzi wa polisi. Daktari Mbaga alielewa yeye ni mtuhumiwa wa kesi inayomkabili ya kutoa vipimo vya uongo na kura rushwa lakini alishindwa kuelewa alikuwa mzima hana ugonjwa wowote na aonekani machoni kwa watu lakini amepoteza fahamu amezinduka akiwa mgonjwa tena anaonekana machoni kwa watu kilichomkuta ajui.
Mawazo mengi yalimtawara akifikiria nini kilimkuta lakini hakuna alichokumbuka hadi anapitiwa na usingizi wa masaa matatu. Alipokuja kuzinduka akiwa amezungurukwa na kundi kubwa la waumini wa kiislamu wakimpa pole, lakini bado alizidi kujiona ni mtu aliekuwa katika usingzi mzito kama mtu aliekufa.
Alipobaini akuwa ndani ya usingizi wowote alijawa na donge moyoni lililochanganyika na matamanio zaidi ya kutaka kujua mengi kuhusu yeye, alijitahidi kupepesa macho angalau atamuona mtu anaemfahamu ili amuulize chochote kuhusu yeye lakini akuweza kufanikiwa sura hata moja kuona lakini alipotizama huku na huko alikiona Kivuli cha Imamu Shafii pembeni kabisa mbari na hapo katika kitanda chake kikimuangalia na kikimuonesha ishara ya kutoongea chochote. Hali hiyo iLImnyima amani ya roho daktari Mbaga, alijiona kama mfungwa huru au samaki mwenye mengi ya kusema lakini maji yamemzonga mdomoni.
Moyoni alitafakari yeye ni nani na kama daktari Mbaga iweje miongoni waliokuja ni waumini wa kiislamu hakuna hata mmoja aliemjua wala kumtambua na wanamchanganya wanapompa shukrani kwa kazi ipi? na kubwa zaidi kila anaekuja ni muumini wa kiislamu alimsalimia kwa salamu ya kiisalamu.
“ASALAM ALEYKHUM”
Huku akipewa pole nyingi. Alijiuliza iweje wamsalimie kwa salamu hiyo wakati yeye ni mkristo wa Romani katoriki na tena kwanini wampe pole kwa nini?. Alijiuliza maswali mengi akilini mwake yasiokuwa na majibu. Alijitaidi kukumbuka kadri ya uwezo wake mara ya mwisho kilitokea nini lakini akuwa na funguo ya kufungua fumbo zito lililotanda mawazoni mwake.
Alichokumbuka kabla ya kupoteza fahamu alikuwa na waumini wawili wa kiislamu na askari walikwenda Kitunda kufatiria maiti ya Imamu Shafii baada ya kubadilishwa lakini akuweza kukumbuka kilichoendelea kwa sababu alizimia akajikuta yupo mochwari. Hapo mochwari aliona maiti nyingi za wale wakulya waliokuwa wanazuia maiti ya Imamu Shafii isichukuliwe hata hivyo alizimia baada ya kuzidiwa na baridi kali la mochwari, alipokuja kuzinduka alijikuta akiwa amefungwa pingu yupo chini ya ulinzi kilichotokea ajui.
Kadri masaa yalivyozidi kuongezeka idadi ya waumini wa kiislamu ilizidi kuongezeka na miongoni mwao alifika mke wa Imamu Shafii alisogea sehemu alipo daktari Mbaga huku machozi yakimtiririka anamkumbatia daktari Mbaga.
“Pole sana, pole! Pole!”
Yalikuwa maneno ya mke wa Imamu Shafii akimwambia daktari Mbaga, daktari Mbaga aliitikia kwa kichwa na bila kumuelewa huyo ni nani anampa pole huku analia kwa uchungu.
“Mengi yamekukuta ila mungu amekusaidia kabla ya kwenda kuzikwa”
Lilikuwa swali lililomfanya daktari Mbaga kumwangalia mke wa Imamu Shafii kwa muda.
“Nilitaka kuzikwa?”
Daktari Mbaga alishindwa kuelewa ukweli wa mambo hayo anajiuliza alifanya nini mpaka alitaka kuzikwa. Alimwangalia kila mmoja aliopo hapo uenda anaweza kumuona mtu anaemjua ili amuulize kuhusu yeye kipi kilimkuta hadi kutaka kuzikwa.
Alipepesa macho katika sura za watu wote waliopo hapo lakini hakuna hata mmoja aliemjua ila pembeni ya watu waliopo hapo aligongana uso kwa uso na Kivuli cha Imamu Shafii kikiwa kinalia kinabubujikwa na machozi. Daktari Mbaga alijiuliza kwanini Kivuli cha Imamu Shafii kinalia kinalilia nini?.
Alizidi kuwa katika dimbwi la mawazo kuhusu yeye, nini kilitokea, iweje anaonekana machoni mwa watu, wakati alikuwa aonekani machoni mwa watu, na kwanini idadi kubwa waliokuja kumuona ni waumini wa kiislamu hakuna hata mmoja anaenjua, alikuwa katika wakati mgumu sana kuhusu yeye kufahamu siri iliofichika kwa upande wake.
Hali hiyo ilimnyima sana amani ya roho daktari Mbaga ndipo aliamua kuvunja sharti la Kivuli cha Imamu Shafii kutokuongea na badara yake kumuuliza muumini mmoja wapo aliokuwepo hapo ili kutaka kufahamu mengi kuhusu yeye lakini kabla ajamuuliza muumini mmoja wapo.
“Sasa ni wakati wa kuwatia hatiani watuhuumiwa wote mume wangu!”
Kauli hiyo kutoka kwa mke wa Imamu Shafii, ilikuwa kama taa za gari zimewaka ghafla baada ya kusumbua kwa muda mrefu, taratibu daktari Mbaga alimgeukia mke wa Imamu Shafii na kumuangalia, huku akitafakari kauli hiyo.
"Mimi mume wake?"
Baada ya kuitwa mume alitaka kujua kwanini kaitwa mume na mke wa Imamu Shafii ndipo aliamua kuvunja ukimya na kuvunja sharti la Imamu Shafii la kutokuongea. Aliona bora amuulize huyo mke wa Imamu Shafii ili afahamu nini kinaendelea kuhusu yeye lakini kabla ajamuuliza chochote walifika askari wawili aliwatambua, walikuwa ni askari aliokwenda nao pamoja Kitunda kufatilia maiti ya Imamu Shafii.
“Tunahitaji kumfanyia mahojiano”
Waumini waliwapisha askari, askari walimfungua pingu waliondoka nae daktari Mbaga. Daktari Mbaga akiwa anaondoka na hao askari alikuwa anamuangalia mke wa Imamu Shafii huku akitafakari kauli yake aliongea muda mfupi ya kumuita mume wakati yeye ni daktari Mbaga.
**********
Askri waliondoka na daktari Mbaga na kuelekea nae kituo cha polisi Tabata Shule, walipofika kituoni hapo waliingia chumba kilichoandikwa wapelelezi.
“Kaa hapo ostazi”
Askari mmoja alimuelekeza daktari Mbaga sehemu ya kukaa, daktari Mbaga alikaa sehemu alipoelekezwa kukaa.
“Ndio Ostazi bado ukumbuki chochote toka uzinduke?”
Daktari Mbaga alishangaa kuitwa Ostazi, alibaki ameduwaa kwa muda huku akitafakari iweje aitwe Ostazi wakati yeye ni daktari Mbaga, alifikiria alivyoitwa na mke wa Imamu Shafii.
“Sasa ni wakati wa kuwatia atiani watuhuumiwa wote mume wangu”
Kauli hizo zote zilimfanya kuchanganyikiwa baada ya kuulizwa. Kama dakika tano alikuwa kimya lakini ghafla kilitokea Kivuli cha Imamu Shafii kilimpa ishara ya kuongea na kinapotea. Ndio hapo daktari Mbaga alijiona kama mateka wa kivita amepewa uhuru wa kuondoka. Kwakuwa alikuwa anataka kujua ukweli kuhusu yeye alikubali na kujibu kama alivyoulizwa.
“Ni vigumu sana ndugu yangu, ebu niambie kwanza iweje mimi nipo hapa?”
"Ni zaidi ya miezi mitatu (3) ulikuwa hospitali Ostazi”
“Miezi 3, nilikua hospitali ninafanya nini?”
Maelezo yale yalizidi kumchanganya zaidi aktari Mbaga na kubwa zaidi anaitwa Ostazi wakati yeye ni daktari Mbaga na dini yake ukristo. Alitetemeka huku akiwa ahamini uwepo wake duniani. Ni kweli yanayoendelea kumtokea ni ya kweli au yupo ndotoni, ulikuwa ni mtihani asioweza hata kujibu, alijiuliza mwenyewe.
“Miezi 3 nikiwa hospitali naumwa nini na iweje mimi niwe Ostazi? siamini yanayoendelea"
Alishindwa kuelewa ukweli wa mambo hayo, aliamua kumwambia mpelelezi.
"Sikumbuki chochote ila ninachokumbuka zaidi mimi ni Fredy Mbaga ni daktari na nilikuwa nafanya kazi katika hospitari ya Amana lakini sikuweza kujua nini kilinipata mpaka nikawa hospitali ndani ya miezi 3”
“Labda itakapofika siku ya tarehe ya mahakamani ya kesi yako, utapata tu kumbukumbu Ostazi wangu”
“Siku ya mahakama ya kesi yangu?”
“Ndio, kesi yako, kwani hujui kama una kesi nzito?”
Kumbu kumbu za ghafla zilimjaa mawazoni mwake daktari Mbaga, kesi inayomkabili ndio iliofungua mawazo na kumbukumbu zote zilizopotea kwa muda mrefu sana.
“Kesi yangu, naikumbuka vema, nilishtakiwa nikiwa ndani ya hospitari ya Amana , nilikuwa daktari bingwa wa uchunguzi wa maiti”
“Daktari bingwa wa wa uchunguzi wa maiti katika hospitari ya Amana?”
“Ndiyo”
Hakika alijawa na simanzi, machozi yalimmwagika, aliumia alipokumbuka nini kilichosababisha yeye kuwa mtuhumiwa na kuaribu kazi yake katika hospitari ya Amana, picha na taswira za kumbukumbu juu ya waliosababisha yeye kuingia katika kesi nzito zilimrejea mawazoni mwake, mwanzo mpaka mwisho wa tukio.
Alianza kulia kwa uchungu mkubwa, hali iliyomfanya mpelelezi apate kazi ngumu ya kumbembeleza na kumsihi asilie, amueleze nini kilichomkuta maana histori anayoikumbuka sio yenyewe anayoitaka huyo mpelelezi.
“Tafadhari Ostazi, haya ni ya dunia! tena ni mambo ambayo ayahusiani na wewe kabisa, naomba nieleze yanayokuhusu wewe ulipatwa na nini hadi kuwa katika hali hiyo, ili nijue namna ya kukusaidia na kukamilisha upelelezi ili watuhumiwa watiwe hatiani"
"Kama yapi unataka kuyajua kuhusu mimi mheshimiwa?"
"Yaliyokukuta wewe na dereva bodaboda, dereva bodaboda amekufa na wewe umenusurika kufa sasa unaposema wewe ulikuwa daktari bingwa wa uchunguzi wa maiti sio kweli, wewe ni Imamu wa msikiti Tabata Mawenzi"
"Ahaa!
Kwa mshangao mkubwa kwa kusikia hayo aliyoambiwa yeye ni Ostazi, alikuwa katika wakati mgumu wa kuelewa hayo mambo ndipo aliomba simu kutoka kwa huyo mpelelezi.
"Una simu ya smart phone?"
"Yah nini?"
"Kama unayo naomba nipige picha!"
"Halafu nikikupiga picha"
"Utafahamu kila kitu"
Mpelelezi alitoa simu yake mfukoni alimpiga picha daktati Mbaga, alipomaliza kumpiga picha.
"Naomba nione hiyo picha"
Mpelelezi alimpa simu daktari Mbaga, daktari Mbaga aliangalia hiyo picha akuweza kuamini anachokiona katika hiyo simu. Hakuwa na hofu yeyote kwani imani yake ilisadiki kuwa yupo katikati ya ndoto nzito ya kutisha, huku akiendelea kuitazama vema ile picha.
Wakati alipobaini akuwa ndani ya usingizi wowote, alijawa na hofu zaidi ya kutaka hata kuchanganyikiwa kwani kila alipojaribu kujiweka sawa sura yake ili kuileta taswira ya sura yake kama daktari Mbaga ilishindikana . Alijitazama tena na tena lakini akuwa na funguo yeyote ya kufumbua fumbo zito lililotanda mawazoni mwake.
Akiwa na sura ya Imamu Shafii, ajabu akumbuki lolote wala kujua chochote kilichofanyika mpaka kuwa na sura ya Imamu Shafii. Hata akuweza kupata bahati ya kushuhudia mabadiliko hayo ya sura yake kutoka daktari Mbaga na kuwa katika sura ya Imamu Shafii. Mawazo mazito yalinamtawara zaidi ya kutaka kuchanganyikiwa na hata mabadiriko ya mapigo ya moyo yali badilika kutoka mdundo wa kawaida na kuwa zaidi ya mdundo wa kawaida.
Mwili wake daktari Mbaga ulikuwa dhaifu na alikuwa anatetemeka juu ya muonekanano wa Imamu Shafii kuwepo katika sura yake. Ghafla alikuwa kama mtu alieingiwa na pepo, aligeuka alimuangalia mpelelezi kwa muda kama dakika tano mara alimpa simu yake mpelelezi. Wakati huo akuwa na budi kuyasimulia yote yaliyomkuta kama Imamu Shafii kuanzia ile misukosuko na tukio zima.
**********
Hali ya hewa ilikuwa baridi katika jiji la Dar es Salaam kiasi kwamba watu wengi wenye makoti waliyavaa kujistili na baridi kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Karibu kila mtu katika jiji la Dar es Salaam, alivaa sweta na kufanana na watu wa mkoa wa Mbea au Kilimanjaro. Hao hulazimika kuvaa hivyo kutokana na hali ya baridi.
Kutokana na hali hiyo siku hiyo ilikuwa yenye utulivu sana kiasi fulani, kwani hali ya hewa ilikuwa na mawingu mazito ya baridi maana hakukuwepo na dalili zozote za kuwepo kwa mwezi kwakuwa mwezi ulizibwa na mawingu mazito. Ilikuwa yapata saa kumi na dakika 39 inaelekea saa kumi na moja alfajiri kama sijakosea. Akiwa anatoka nyumbani kwake Imamu Shafii anaelekea msikitini.
Alikatiza chochoro iliotenganisha nyumba na nyumba akatokea kwa mafundi selemara anavuka barabara kubwa ya lami inayotokea Tabata Kimanga anafika msikitini. Kama Imamu wa msikiti huo alikuwa amewahi kwa hiyo akaelekea moja kwa moja hadi chooni akajitoharisha na kuondoa najisi zote. Ndani ya dakika tano zilimtosha kujisafisha anatoka chooni. Alienda hadi sehemu ya kutia udhu, anatia udhu, alipomaliza anaingia ndani ya msikitini na kuelekea kibla anakaa chini anapiga dua, alipomaliza anamshukuru mungu. Alisogea hadi ilipo maiki anachukua maiki anapiga adhana ya kuwamsha watu kuja katika ibada.
Muda huo wote kiza kilikuwa bado kimetanda na ukimya ulikuwa umetawara. Sauti ya adhana ilisafiri umbali mrefu na kuwaamsha waumini wa kiislamu katika usingizi na kujiandaa kuja msikitini. Baada ya kumaliza kupiga adhana anajiandaa kuswali sala ya sunna lakini ghafla alisikia kishindo kikubwa kwa nje, alisikiliza kwa umakini ili kujua kishindo hicho cha nini ndipo anasikia mtu anavuta pumzi kuashiria kuna kitu anajitahidi kukibeba alishangaa sana! huku anasikiliza kwa makini. Akiwa ametegesha masikio kama sungura aliehisi hatari kutoka hatua chache eneo alilokuwa.
Hali hiyo iliendelea na ilikuwa inazidi kusogea eneo la msikiti. Imamu Shafii taratibu alitoka hadi nje uso kwa uso na watu watatu wawili wenye miili minene na mmoja mwili wa kawaida wamevalia suti nyeusi. Wawili wamebeba mwili wa mtu na mmoja alikuwa amebeba rundo la vitabu walikuwa wanasogea karibu na mlango wa msikiti. Watu hao walipomuona Imamu Shafii walishtuka wanaudondosha chini huo mwili wa binadamu. Imamu Shafii alipouangalia huo mwili aligundua ni maiti, hapo hapo hali ya uwoga ilitawara akiwa amesimama mlangoni amekodoa macho kama panya kabanwa na mlango.
Hao wavaa suti waliangaliana na kupeana ishara walimsogerea Imamu Shafii. Imamu Shafii alikimbia ndani ya msikiti, alitaka kufunga mlango lakini alichelewa, hao wavaa suti wanawai kuingia ndani ya msikiti wanamkamata. Walimlazimisha kumtoa nje lakini Imamu Shafii alikuwa mgumu kutokana alikuwa anajua kareti aliwasumbua hao wavaa suti. Mmoja wa wavaa suti haraka haraka alitoka nje mara anarudi akiwa mkononi ameshika nyundo ya kupasuria kokoto.
Alifika hadi walipo wenzake wakiwa wanapambana na Imamu Shafii. Imamu Shafii alikuwa makini sana kumuangalia huyo aliyokuja na nyundo na kutowazingatia hao wengine lakini matokeo yake mmoja wapo alimpiga mtama anaanguka chini. Hapo hapo wanamvamia kwa pamoja wanamdhibiti. Huyo alioshika nyundo alisogea, bila huruma ananyau nyundo anampiga ya kichwa Imamu Shafii. Alipiga kelele kali za maumivu, kichwa kilipasuka damu ziliruka, Imamu Shafii alianza kuishiwa nguvu alishindwa kufanya chochote hatimae alianguka chini.
**********
“Mpelelezi, naimani pale ndio ulikuwa mwisho wa maisha yangu”
Alimaliza kwa kusema hivyo Kivuli cha Imamu Shafii kikiwa katika mwili wa daktari Mbaga. Mpeleezi japo na kuhadithiwa chanzo chote lakini bado alikuwa njia panda kutokana Kivuli cha Imamu Shafii kusema yeye ameshakufa.
“Nimekusikiliza na nimekuelewa kwa umakini sana, mwanzo mpaka mwisho wa matukio yako, lakini najua itakuwa vigumu sana mimi kuamini ukweli wa mambo haya?
“Kwanini?”
“Unasema pale ndio ulikuwa mwisho wa maisha yako wakati nakuona upo hai”
“Ukweli wazi uwezi kuamini kutokana na unachokiona ila amini ninachosema”
“Hapana! wewe ulizimia kwa kipindi kirefu ila sasa umezinduka kwa msaada wa madaktari kwa hiyo ni jambo la kumshukuru mungu labda useme akili bado aijakaa sawa! ila yote ya dunia Ostazi wangu hadi kufika hapo mshukuru mungu na mungu atakusadia utakua sawa kiakili na nakuahidi nipo pamoja na wewe bega kwa bega mpaka mwisho wa kesi yako na kuhakikisha watuhumiwa nawatia hatiani”
Mpelelezi alimaliza mahojiano aliaga anaondoka. Baada ya mpelelezi kuondoka ndipo ufahamu wa daktari Mbaga ulirudi kama kawaida lakini daktari Mbaga alikua kama mtu alietoka katika usingizni mzito huku akiwa kama anaota na kutambua yote yalioendelea hapo kati ya mpelelezi na Kivuli cha Imamu Shafii.
Ilimbidi tu kuamini yote yanayotokea mwilini mwake na yanayotaka kufanyika ili kuwa uhuru. Kwa hiyo kuanzia hapo tena akukifikiria vibaya Kivuli cha Imamu Shafii ndani ya mwili wake, bali sasa alitambua kiasi gani Kivuli cha Imamu Shafii kimekuwa msaada kwake na ndio anatambua lengo la Kivuli cha Imamu Shafii kumzuia kuongea kwa muda mrefu.
Machozi yenye nusu furaha na nusu huzuni yalimmwagika na kuanza kulia, muda huo huo walifika askari walimchukua daktari Mbaga ambaye alionekana akiwa katika umbo la Imamu Shafii walimrudisha hospitali alikokuwa mwanzo kwa matibabu.
**********
Mpelelezi alitaka kujuwa sababu ya hao wavaa suti kupelekea maiti hapo msikitini na hilo rundo la vitabu na ilikuwaje mpaka barabarani na Imamu Shafii kukutwa barabarani na yule dereva bodaboda tena tukio la kuchomwa moto na ikisemekana ni ajari ya pikipiki.
Alielekea hadi chumba cha mafaili ya kesi alichukua faili la kesi inayomkabiri daktari Mbaga alielekea moja kwa moja hadi chumba cha upelelezi. Alipofika alianza kupitia maelezo ya faili hilo kurasa moja na nyingine kwa umakini mwanzo mpaka mwisho ndipo aligundua kitu.
“Kuna tija ya kuonana na huyu daktari Mbaga ili kupata maelezo yake maana hii kesi ipo katika utata, kuchukua rushwa na kutoa vipimo vya uongo?”
Alifikiri kidogo huku akiangalia hilo faili.
“Uchunguzi wa akili unahitajika”
Alifunika mafaili yote.
“Imamu ndio muhasirika wa ili tukio maelezo yake ndio yenye ukweli lakini chanzo akijulikani mpaka yeye kuwa muhasirika wa ili tukio mhm! Uvamizi msikitini bila kuwepo sababu ya uvamizi sio kweli na huyu daktari kuchukua rushwa na kutoa vipimo vya uongo kuna kitu kimefanyika!.....lazima nionane nae”
Aliweka hayo mafaili katika sehemu yake, aliinuka alitoka hadi nje. Alipanda gari maeneo ya Tabata Shule na kuelekea Segerea. Alitumia dakika kadhaa kufika jera ya segerea, aliomba kuonana na mtuhumiwa daktari Mbaga, aliruhusiwa. Baada ya dakika kumi kukamilisha tartibu zote, daktari Mbaga aliletwa na askari magereza.
“Daktari Mbaga kesi inayokukabili ni kura rushwa na kutoa vipimo vya uongo lakini mimi kama mpelelezi naomba tuongee ili nijue nakusaidia vipi na kufika mwisho wa kesi hii”
Daktari Mbaga kimya bila kuongea chochote, mpelelezi alimuuliza mara kwa mara lakini daktari Mbaga kimya, akionekana kama anawaza kitu kingine, mawazo yake hayakuwa hapo kabisa na zaidi anaonekana kama mtu anaeanza kuingiwa na uchizi au uzezeta.
Mpelelezi aligundua mapema hali hiyo alihisi akili imechanganyikiwa kutokana na hali ya kukaa mahabusu kwa muda mrefu na ukichangia kesi inayomkabiri lazima atakuwa katika hali kama hiyo.
Mpelelezi akutaka tena kuendelea kumuuliza zaidi na zaidi aliita askari wamchukue, bila kupoteza muda askari walifika wanamchukua wanamrudisha mahabusu. Mpelelezi alibaki chumba cha mahojiano akitafakari juu ya kupata maelezo yake ili kukamilisha upelelezi. Baada ya kuisumbua akili yake.
Alipata wazo, alitoka hapo eneo la kuonana na wafungwa, alienda kuonana na bwana jera na kumueleza daktari Mbaga akuongea chochote.
“Ni ngumu sana kupata maelezo ya huyo mtuhumiwa kwakuwa tangu, akuongea na mtu wa aina yeyote, mwanzoni nilijua bubu lakini nilipopata kumfahamu na kuijua historoa yake sikuweza kujua kwanini ataki kuongea na mtu kwa sababu alifanyiwa mahojiano akuonesha ushirikiano wala kuongea na mtu yeyote”
Bwana jera alimwambia mpelelezi, mpelelezi anashangaa sana kusikia maelezo hayo, bwana jera aliendelea.
“Wakili wake alijitahidi sana kufika hapa gerezani kumuhoji ili kumsaidia kesi inayomkabili lakini ameshindwa, aliongea mara moja tu mahakamani na kumwambia hakimu kuwa kama ameonekana na hatia na kesi inayomkabili basi ahukumiwe”
“Duu!!!!”
“Kwanini sasa anafanya hivi?”
“Ni swali kila mtu aliuliza ili kutaka kujua lengo lake nini lakini hakuna ila kama amekili kosa hakimu anabudi kumuhukumu”
“Ni kweli maana msaada pekee kutoka kwake ni kuonesha ushirikiano ili kutetea kesi inayomkabiri lakini kama ataki kuonesha ushirikiano, hakimu atatoa hukumu”
Mpelelezi akuwa na la ziada waliagana na bwana jera, anatoka ndani ya jera ya segerea anapanda daradara inayoelekea Mnazi Mmoja. Mpelelezi akiwa ndani ya daradara aliahidi kurudi tena hapo gereza la Segerea kuonana na daktari Mbaga huku akiwa na imani kuwa kadri atakavyokuwa anakuja kuonana nae, atamuweka sawa kisaikolojia na atakuwa sawa atapata nafasi ya kumuuliza mawili matatu.
Lakini bila kujua kuwa huyo aliokuwa mahabusu ndani ya gereza la Segerea sio daktari Mbaga bali ni Kivuli cha daktari Mbaga na akiwezi kuongea wala kutamka neno lolote kutokana na kile alicholishwa daktari Mbaga na Kivuli cha Imamu Shafii akiwa ndani ya chumba cha upelelezi na kusababisha kutokea daktari Mbaga wawili ndani ya ukumbi wa mahakama.
**********
Mpelelezi safari yake iliishia hospitali ya Amana. Alishuka ndani ya daradara moja kwa moja alielekea kwa daktari mkuu wa hospitali ya Amana.
"Habari yako"
"Salama!"
"Pole kwa majukumu"
"Usijari! ni sehemu ya kazi yangu"
"Naitwa Job ni mpelelezi kutoka kituo cha polisi Tabata shule"
"Nashukuru kukufahamu, na mimi naitwa dokta Wilson"
"Nashukuru pia kukufahamu"
“Kubwa zaidi nahitaji kupata vipimo vyote vya maiti zote mbili za kesi inayomkabiri daktari Mbaga”
"Ohoo! aina shida naomba nipe dakika chache"
"Usijari!"
Daktari aliinuka anaaelekea moja kwa moja hadi chumba cha uchunguzi wa maiti, anakutana na madokta wake, anamwita daktari ambae msaidizi wa daktari Mbaga katika kitengo cha uchunguzi wa maiti, alienda nae moja kwa moja hadi ofisini kwake.
"Utafanikisha yote kwa daktari hapa"
Mpelelezi alimsalimia daktari msaidizi wa daktari Mbaga, baada ya salamu.
“Naitwa Job ni mpelelezi kutoka kituo cha Tabata Shule, nahitaji vipimo vya uchunguzi wa maiti mbili za kesi inayomkabili daktari Mbaga”
“Sawa mheshimiwa, naomba dakika tano”
Daktari msaidizi wa daktari mbaga kitengo cha uchunguzi wa maiti anamwambia mpelelezi.
“Sawa”
Daktari msaidizi wa daktari Mbaga alitoka ofisi ya daktari mkuu alielekea moja kwa moja katika ofisi yake, alichukua faili la uchunguzi wa vipimo vya maiti ya Imamu Shafii na dereva boda boda. Alienda nalo hadi katika ofisi ya daktari mkuu wa hospitali ya Amana, alimpa mpelelezi. Mpelelezi alipokea na kuanza kulipitia faili hilo lakini baada ya kufunua kurasa kadhaa.
“Una uhakika Imamu Shafii amekufa kwa kugongwa na pikipiki hadi kufa”
Lilikuwa swali gumu lilileta ukimya kwa daktari msaidizi wa daktari Mbaga.
"Daktari umesikia nilichokuuliza?"
"Ndio kwa mujibu wa vipimo"
“Sawa! kwa mujibu wa vipimo vinathibitisha hivi itabidi nikubaliane na vipimo”
Daktari mkuu alimwangalia daktari msaidizi wa daktari Mbaga, kama alihisi kitu kwa daktari msaidizi wa daktari Mbaga lakini akuongea chochote.
“Sawa sina la ziada nilitaka kujua juu ya vipimo kwa hiyo naondoka ila nahisi haya mafaili ni kopi, orijino mnayo basi naomba kwenda nayo”
Kwa sauti ya chini na ya unyonge daktari msaidizi wa daktari Mbaga alisikika.
“Sawa”
Mpelelezi bila kusubili swali au maelezo kutoka kwa daktari mkuu wa hospitali ya Amana, aliaga aliondoka,. Ofisini alibaki daktari mkuu na daktari msaidizi wa daktari Mbaga.
“Vipimo vinasibitisha Imamu amekufa na dereva bodaboda amekufa”
Daktari mkuu wa hospitali ya Amana alimuuliza daktari msaidizi wa daktari Mbaga.
“Ndio”
“Kwanini ameuliza kuwa una uthibitisho Imamu na dereva bodaboda wamekufa”
“Hapo kiongozi sijajua”
“Sawa! kama umethibitisha maiti zote mbili ajari ya pikipiki ndio iliowaua kwanini ulikuwa mzito kujibu baada ya kuulizwa?"
"Nilishangaa kwanini ameniuliza hivyo, ndio maana sikutaka kujibu haraka maana yule mpelelezi yupo katika upelelezi sasa naweza kujibu haraka mwisho wa siku nikawa najibu kitu ambacho si sahihi"
"Ohoo! hakuna tatizo, kaendelee na kazi”
Daktari msaidizi wa daktari Mbaga aliondoka anamuacha daktari wake mkuu wa Amana akiwa na mawazo juu ya swali alilouliza mpelelezi. Swali ilo lilimnyima amani ya roho sana ndio hapo alipobaki njia panda juu ya swali ilo, anafikiria kwa kina bila jibu. Aliinuka na kutoka ndani ya ofisi yake alielekea moja kwa moja hadi ofisi ya mafaili ya vipimo vya uchunguzi.
Alipofika alichukua faili la vipimo vya Imamu Shafii na dereva bodaboda alianza kupitia kurasa moja baada ya nyingine ndipo aliona maelezo kuwa Imamu Shafii amegongwa na pikipiki hadi kufa papo hapo na dereva bodaboda ameungua na moto na kufa papo hapo. Daktari mkuu ndipo anaona utofauti kati ya vipimo vya maiti ya Imamu Shafii na dereva bodaboda na alipoikumbuka kauli ya mpelelezi.
“Una uhakika Imamu Shafii amekufa kwa kugongwa na pikipiki hadi kufa”
Alikuwa katika wakati mgumu wa kuelewa ukweli upo wapi kati ya vipimo na kauli ya mpelelezi. Alitafakari kwa kina lakini bila kupata majibu, alitoka chumba cha mafaili alielekea chumba cha uchunguzi wa maiti alikutana na daktari msaidizi wa daktari Mbaga.
“Nahitaji kuongea na wewe, nakuomba ofisini kwangu”
Daktari mkuu alielekea ofisini kwake, daktari msaidizi wa daktari Mbaga hali anayomuona nayo mkuu wake anahisi kuna tatizo, lakini alienda hadi ofisini.
“Naomba tuongee mimi na wewe na uniambie ukweli wa mambo maana tukichukulia mambo juu juu tunaweza kukosa kazi”
Daktari msaidizi wa daktari Mbaga kauli hiyo ilimshtua sana na aliuliza kwa wasi wasi.
“Kwanini na ukweli upi?”
“Ni kweli vipimo vinaonesha vimechunguzwa na dokta Mbaga kwa uthibitisho wa saini sasa vipimo ulivyochunguza wewe vipo wapi?”
Daktari msaidizi wa daktari Mbaga alishtuka.
“Kesi ipo mahakamani na daktari Mbaga anashikiriwa na polisi kwa kutoa vipimo vya uongo na kura rushwa lakini mwisho wa kesi utaitajika ukweli wa vipimo sahihi, je! wewe kama wewe ulichunguza kwa mara ya pili katika maiti zote?”
“Hapana”
“Kwa sababu gani wakati unajua kesi inayomkabili mkuu wako ni kutoa vipimo vya uongo”
Daktari mkuu alimuuliza daktari msaidizi wa daktari Mbaga, lakini daktari msaidizi wa daktari Mbaga alikuwa kimya kama dakika tatu ndipo alianza kujitetea.
“Dakika ya mwisho maiti zilichanganywa ya Imamu walipewa watu wengine na watu wengine ilibaki hospitali na ya yule dereva bodabda maiti yake hadi leo bado ipo mochwari hakuna ndugu aliejitokeza”
“Sawa hapo hapo katika maiti ya Imamu, maiti ilipochukuliwa na watu wengine kimakosa ulichukua utaratibu gani?”
“Ndugu wa ile maiti waliomba kibali maalumu ili kufatiria hiyo maiti, tuliwapa”
"Ulipata taarifa za kupatikana kwa hiyo maiti?"
"Hapana!"
"Kwa nini"
Daktari msaidizi wa Daktari Mbaga kimya.
“Ok!!...kesi nzito naomba uchunguzi ufanyike wa maiti ya dereva bodaboda haraka iwezekanavyo nahitaji vipimo vyake”
“Sawa mkuu!”
“Kazi njema”
Daktari msaidizi wa daktari Mbaga aliinuka aliondoka alielekea moja kwa moja hadi mochwari lakini alipofika karibu na mochwari uso kwa uso na Job mpelelezi akiwa na jopo la madokta wanatoa maiti ya dereva bodaboda ndani ya mochwari.
“Ohoo!! Shit!!”
Kitendo hicho kilimkera sana daktari msaidizi wa daktari mbaga. Job askari mpelelezi alitembea huku anamwangalia kwa jicho kali daktari msaidizi wa daktari mbaga. Kwa muonekanao wa daktari msaidizi wa daktari Mbaga aliokuwa nao, mpelelezi alihisi kitu lakini akumsemesha wala kumuongeresha anampita.
Madokta walifikisha maiti ya dereva bodaboda katika gari la wagonjwa iliondaliwa wanaiingiza ndani ya gari hilo la wagonjwa na wao wanapanda katika hiyo gari ya wagonjwa. Mpelelezi alielekea moja kwa moja hadi ofisi ya daktari mkuu.
“Dokta vibari vyote nimekamilisha ili kuchukua maiti ya yule dereva bodaboda kwa upelelezi, kilichobaki kutoka kwako ni sahihi ili kuruhusu maiti kutoka katika hospitali yako”
Alitoa fomu maalumu ya kusaini daktari mkuu, daktari mkuu alibaki katika hali ya mshangao lakini Job askari mpelelezi alimsogezea hiyo fomu ya kutia saini ili asaini maiti ya dereva bodaboda ipate kutoka. Daktari mkuu akuwa na la ziada anaweka saini.
Baada ya daktari mkuu kumaliza kuweka saini. Mpelelezi alishukuru alimuaga daktari mkuu anaomdoka. Daktari mkuu alibaki katika mawazo bila kujua afanye nini mara muda huo huo anaingia daktari msaidizi wa daktari Mbaga.
“Vipi mkuu hoda kutoka kwako?”
Daktari mkuu alimwangalia daktari msaidizi wa daktari Mbaga kwa jicho kali. Daktari msaidizi wa daktari Mbaga alihisi kuna tatizo taratibu anageuka anaondoka ndani ya ofisi ya daktari mkuu. Daktari mkuu alichukia kitendo hicho anajifyonya huku akijalaumu.
“Daaa!!” Kosa langu kutokuwa makini na utaratibu wa hospitali”
Anashika kichwa.
“Sijui itakuwaje mwisho wa ili?”
Yalikuwa ni majuto yaliomtawara daktari mkuu lakini mwisho wa siku aliamua kukusanya vitu vyake na kuweka vizuri na kufunga ofisi na kuondoka lakini alipitia chumba cha uchunguzi wa maiti, kupitia dirishani alimuona daktari msaidizi wa daktari Mbaga akiwa anafungua faili moja baada ya lingine lakini kila faili alilokuwa anafungua, anafungua kurasa mbili tatu anafunga anafungua lingine. Daktari alimwangalia kwa muda alibaki kusikitika, ilimjia sauti fulani mithili ya malaika,
“Umuhimu wa kazi unakuja baada ya tatizo”
Aliondoka daktari mkuu chumba cha ucnguzi wa maiti lakini kauli hiyo iliendelea kumnyima amani ya roho,
“Ndipo ugumu wa kazi unapoonekana na kushindwa kutatua tatizo akili inaposhindwa kutoa maamuzi sahihi”
Ndipo hapo daktari mkuu alipobaki njia panda asijue nini cha kufanya zaidi akili inamvuruga alijiona mkosaji kwa daktari Mbaga, njia yote kichwa kinakuwa kizito kimetawariwa na mawazo.
**********
Baada ya kutoka ndani ya ofisi ya daktari mkuu wa hospitali ya Amana aliingia ndani ya gari ya wagonjwa tayari kuelekea kwenye hospitali ya ya kijeshi ya Lugalo. Mpelelezi alipanda gari moja na askari wenzake. Safari ilianza huku gari hilo la wagonjwa likiwa katika mwendo wa kasi kama unavyojua magari hayo yakiwa safarini hata ikiwa umbali mrefu unalisikia kutokana na king’ola kinacholia. Magari ya kawaida yaliokuwa njiani upisha na kuliacha linapita ili kuwaisha mgonjwa.
Ndani ya nusu saa gari ilo la wagonjwa aina ya ambulance likiwa na maiti ya dereva bodaboda linafika katika hospitali ya kijeshi ya lugalo linaacha njia ya kuelekea Tegeta linakata kulia na linaingia kambi ya jeshi Lugalo. Kitendo cha haraka haraka madokta wanashuka wanateremsha maiti ya dereva wa bodaboda wanaingiza moja kwa moja hadi ndani ya hospitali wodi ya uchunguzi wa maiti. Ilipokelewa na madokta wa kijeshi, muda huo huo walianza kuufanyia uchunguzi mwili wa dereva bodaboda.
Mchana wa siku hiyo walikamilisha uchunguzi katika mwili wa dereva bodaboda. Waligundua sumu ndio iliondoa uhai wa huyo dereva bodaboda, vipimo hivyo alifikishiwa mpelelezi.
“Kwa kutumia elimu niliokuwa nayo na uthibitisho wa vipimo tulivyochunguza katika maiti vimekuja vipimo sahihi kabisa na tukio husika”
Daktari alifunua hilo faili lenye vipimo, ndipo hapo mpelelezi alipotegesha masikio na kusikiliza vizuri, moyoni akiwa na shahuku ya kujua vipimo vilivyopatikana katika maiti ya dereva bodaboda.
“Vipimo vinathibitisha ni sumu iliomuua mpaka umauti kumfika”
“Dokta sijakuelewa?”
“Kivipi labda?”
“Sumu ndio ilikatisha uhai wake, kivipi unaposema sahihi na tukio husika?”
“Vizuri! Nina maana hii, kuwa sumu ndio iliomuua na kuondoa uhai wake lakini vipi kuungua moto? uoni ni tukio ili kuficha kifo cha sumu ili aonekane kilichomuua ni moto”
Mpelelezi alishusha pumzi na alikaa vizuri katika kiti. Daktari aliendelea kufungua faili analipitia kurasa ya pili, kurasa ya tatu na kurasa ya nne aliendelea.
“Maana katika tumbo lake hakuna mafuta ya aina yeyote labda alikunywa mafuta ili kujichoma moto ila kilichoonekana ni sumu ilitawara katika ini”
Hapo hapo mpelelezi alikumbuka maelezo ya Imamu Shafii alivyomuhadithia mwanzo wa tukio msikitini, ndipo hapo alijiuliza mwenyewe.
“Hapa bado sijaelewa maiti ya huyu dereva bodaboda ililetwa msikitini na hawa wauaji kwa ajiri gani?”
Ni swali lililomuumiza akili yake bila kulipatia majibu, Daktari alimuona akiwa katika hali hiyo, moja kwa moja alihisi anafikiria kitu lakini akutaka kumuuliza kwakuwa anawajua wapelelezi kwa mafikirio ya haraka ili kufanikisha upelelezi wake. Zaidi alimuongeza faida kwa kumuuliza swali ili kufungua ubongo wake kwa mapana ili apate wepesi wa kutambua kwa haraka tukio.
“Tukio limefanyika wapi mpaka maiti inakutwa na serikali kufika?”
“Tabata Mawenzi darajani”
"Sawa! basi hapo ni mwisho ila kuna mwanzo"
"Kivipi?"
“Nina maana hii, hapo mlipoikuta maiti ni mwisho wa tukio ila kuna mwanzo wa tukio ndio aliporishwa au kuchomwa sindano ya sumu”
Mpelelezi alifikiri melezo ya Imamu Shafii aliposikia kishindo kikubwa akiwa ndani ya msikiti na alipotoka uso kwa uso na wavaa suti wakiwa wamebeba maiti ya dereva bodaboda.
“Kwa mantiki hiyo mwisho wa tukio ni hapo ila kuna mwanzo wa tukio ndio aliporishwa au kuchomwa sindano ya sumu, Yes!”
“Vipi mheshimiwa?”
“Nimekuelewa sana uliposema sahihi kabisa na tukio husika”
“Kivipi?”
“Mwisho wa tukio ni Tabata Mawenzi Darajani mpaka maiti inakutwa ikiwa imechomwa moto ila kuna ukweli uliopo nyuma ya panzia chanzo na sababu ya kuuliwa na sumu, na nani?, wapi?, na mpaka kufika msik…..!”
Alisita kumalizia kuongea, alizuga kwa kubadirisha maongezi.
“Mpaka kufika usiku wa tukio na kuamkia asubuhi hakuna aliejua nani amehusika”
Mpelelezi alitaka kusema msikitini lakini aalizuga kwa kusema usiku, daktari aligundua kuna kitu amefichwa na mpelelezi lakini akutaka kumuuliza zaidi alimshauri kwakua anajua kazi ya upelelezi ndivyo ilivyo.
“Cha msingi kwa sasa kujua sababu, chanzo nini, nani na ni wapi hii maiti enzi ya uhai wake ilipolishwa sumu au kuchomwa sindano ya sumu”
“Ndio! Na inahitaji akili na umakini kama kumtafuta nyenyere katika kiza”
Daktari wa kijeshi alitabasamu, waliagana na mpelelezi, mpelelezi alichukua faili la vipimo aliondoka.
Mpelelezi alipanda daradara kwa ajili ya safari kutokea Lugaro ambako ndiko alikokuwa hospitali ya jeshi alielekea nyumbani kwake maeneo ya Tabata Mawenzi. Njiani alikuwa alifikiria kwa kuanzia upelelezi ili kugundua alipouliwa dereva wa bodaboda kwa sumu. Kutokana na kutawariwa na mawazo gafra alipata hisia za usingizi usio wa kawaida ambao ulimtawara mpaka macho yalikuwa mazito, alijiraza katika siti. Baada ya kulala ghafla alijisikia ukungu machoni, mwili wake ukawa dhaifu sana kutokana na nguvu za usingizi.
Alimuona mtu mithili ya malaika amevaa kanzu jeupe refu likiwa limefungwa kwa kamba ya rangi ileile, akiwa anatembea kuelekea pale alikokuwa amelala. Kulikuwa na nuru imemzunguruka kana kwamba ilikuwa ikitokea kwake. Alikuwa yupo peku peku huyo mtu aliomfananisha na malaika na mwonekano wake ulikuwa kama wa watu wa nchi za kiarabu, huku akiwa na ngozi nyeupe. Uso wake ulikuwa wa unyenyekevu lakini akuweza kumtazama machoni. Aliongea kwa sauti ya upole ya huruma, matone ya machozi yalikuwa yakitoka machoni kwake akimaanisha anachokiongea.
Alimnyooshea mkono wake mpelelezi na kumnyanyua kutokea pale alipolala. Ghafla mpelelezi alijiona akiwa na mwili mzuri sana kama malaika alieshushwa na mungu.Alikuwa Amevaa joho jeupe na kamba nyeupe. Japokuwa joho lake lilikuwa jeupe, lilitengenezwa kwa matirio tofauti na joho la yule mtu aliomfananisha na malaika . Joho lake lilikuwa jeupe huku liking’aa kiasi kwamba kama kioo.Mtu huyo alisema kwa sauti ya upole na unyenyekevu
“Naomba uwe mbali na ilo jambo litagharimu maisha yako”
Sauti hiyo ilijirudia rudia na kupenya masikioni mwa mpelelezi gafra alizinduka kutoka katika usingizi alishangaa huku na huko akiangalia yupo eneo gani?. Alihisi kapitiriza kituo lakini sauti ya konda ikiwa inapiga debe mawasiliano mia tatu alipoangalia vizuri ni mwenge, alitulia akawa anatafakari sauti ya mtu aliomfananisha na malaika.
"Naomba uwe mbali na ilo jambo litagharimu maisha yako”
Kauli hiyo ilimnyima amani ya roho lakini gari lilijaa na kuanza kuondoka hadi wanafika mawasiliano bado alikuwa anaifikiria hiyo kauli. Alishuka anapanda daradara ya kuelekea Tabata Kimanga. Ulikuwa ni mwendo wa lisaa limoja kutoka ubungo mawasiliano kuelekea Tabata Mawenzi kutokana na foleni za magari ya njia hiyo. Kwanza mataa eneo la ubungo magari yanayotoka kariakoo, mbezi, buguruni na mwenge yanakutana sehemu hiyo ya mataa, vilevile kutoka ubungo mataa hadi kuipata Tabata Sheri foleni kubwa na ukichangia njia panda magari yanayotoka Buguruni, Tabata Kimanga na ubungo yanakutana hapo kwa hiyo hadi kufika kwake ni lisaa limoja hadi lisaa limoja na nusu.
Hali hiyo watu wanaoishi Tabata Mawenzi na Kimanga walishaizoea, miongoni mwao ni mpelelezi kashaizoea kutokana na adha za njia hiyo. Alishuka katika gari kituo cha Mawenzi anavuka barabara upande wa pili aliingia mtaa wa Mawenzi Garden na kunyoosha njia ya kuelekea Mandera juu na zahanati ya muzdarifa. Alitembea mwendo wa mfupi anaipita baa ya HIBURY anafika nyumbani kwake, baada ya kupita nyumba ya mzee wa kihaya na kufika nyumba ya daktari mstaafu wa Muimbili Mikidadi Mbiligenda alifungua geti anaingia ndani anamkuta mke wake anaandaa chakula.
Mke wake alipomuona mume wake mpelelezi alimpokea kwa furaha lakini mpelelezi akiwa kawaida sana kutokana na uchovu wa safari. Hali hiyo mke wake aitwae Rabia Salum binti wa Kipogoro kutoka Morogoro Mtimbira au mama Michiko aligundua mapema alihisi mume wake kuna kitu kinamsumbua maana si kawaida yake kuwa katika hali hiyo.
“Kuna tatizo?”
“Hapana! ni uchovu tu, naomba niweke maji nikaoge nipumzike”
“Sawa!”
Rabia Salum alimuandalia maji ya kuoga mume wake mpelelezi alimpelekea bafuni, mpelelezi alienda kuoga. Alitumia muda mchache kuoga alipomaliza, alikuta mke wake Rabia Salum mama Michiko kamuandalia chakula. Alikaa mezani alikula chakula, alipomaliza alienda kulala. Ulikuwa ni usingizi uliombatana na uchovu wa mwili na ugumu wa kazi yake ya upelelezi.
Alilala kwa muda mrefu kutoka saa sita mchana hadi saa kumi jioni, kilichomuasha ni sauti ya adhana kutoka msikiti wa Tabata Mawenzi. Aliamka anaingia bafuni anaoga anapomaliza anajiandaa anamuaga mke wake anaondoka. Alitumia mwendo wa dakika tano kutoka nyumbani kwake hadi Mawenzi stendi lakini alipofika kituo cha Mawenzi mara gari ya ubungo inayotokea Kimanga mwisho inafika kituoni hapo.
Mpelelezi alisogea katika gari anapanda, muda huo huo gari linaanza safari. Lakini hiyo daradara ilipofika kituo cha Shiba inasimama na konda anaanza kuita abiria. Sauti ya Imamu wa kiislamu akimaliza kusalisha katika msikiti wa Almasjid Tidc uliopo karibu na kituo cha Shiba ndio inayomfanya mpelelezi ashuke katika hiyo daradara anavuka barabara na kuelekea moja kwa moja hadi hapo msikitini.
Alipofika anawakuta waumini ndio wanamalizia kusoma dua, anasimama nje ya msikiti mpaka wanamaliza. Walipomaliza waumini walianza kutoka na kutawanyika. Mpelelezi aliwaona waumini wawili wakiwa mbele ya msikiti wamekaa chini wanaongea. Mpelelezi taratibu alipiga hatua hadi kibarazani anavua viatu anaingia ndani ya msikiti hadi walipo hao waumini. Alipofika alitoa salamu baada ya salamu alijitambulisha na kuanza kuongea nao.
“Hadi mnapokea taarifa za tukio la Imamu Shafii ulikuwa muda gani?”
“Saa kumi na mbili asubuhi”
“Muda huo alikuwa anatoka wapi anaenda wapi?”
“Kwa kweli atujui ila atakuwa alikuwa anakuja msikitini maana yeye ndio alikuwa kiongozi wa swala kama Imamu wa msikiti”
“Nyinyi mlipata taarifa mkiwa wapi?”
“Tulikuwa msikitini muda wa ibada umefika atumuoni Imamu lakini alikuja muumini mwenzetu kutoka nje akatuonesha damu ndipo tulipoingiwa na mashaka tukaanza kutafuta huku na huko ndipo akaja muumini mwingine kutupa taarifa ya kifo cha Imamu tukaenda sehemu ya tukio tukakuta tukio la ajari ya pikipiki”
“Vizuri! kuna umbari gani kutoka msikitini na eneo la tukio?”
“Karibu tu hapo”
Huku anaonesha upande wa wa kulia kwa jinsi alivyokaa, alionesha maeneo ya darajani.
“Ok! Kwa hiyo amjui chochote kuhusu chanzo cha tukio labda ugomvi kati ya yeye na mtu yeyote?”
"Imamu alikuwa na ugomvi na mtu mmoja lakini huo ugomvi ulikuwa wa kawaida tu uliisha"
"Huyo aliogombana na Imamu ni muumini wa hapa msikitini?"
"Sio muumini wa msikiti huu ila tumemuona kwa siku ya kwanza katika huo ugomvi tena alikuja peke yake na awajui alipotokea"
Mpelelezi alifikiria kwa muda lakini akuuliza tena kitu kingine, maelezo aliyoyapata yalimtoshereza, aliwaaga akaondoka. Safari yake iliishia kituoni kwake, alipofika anafikiria maelezo ya waumini juu ya huyo aliegombana na Imamu Shafii lakini bila kupata jibu kwa sababu akuweza kuambiwa chanzo cha ugomvi kati ya Imamu Shafii na huyo mtu kwakua waumini walimuona huyo mtu kwa mara ya kwanza akiwa anagombana na Imamu Shafii na sio muumini wa msikiti huo wa mawezi.
Mpelelezi akili ilimvuruga kupata ufumbuzi wa kesi hiyo kila hatua aliyokuwa anapiga linakuja jipya. Akili ilimuenda mbio kama saa mbovu.Kazi ikawa aifanyiki mawazo yalimzonga lakini mara linamjia wazo.
"Kama waumini awajui chanzo cha ugomvi na huyo aliegombana na Imamu Shafii awamjui basi atakuwa ni mtu wa mtaani kwake hivyo ugomvi utakuwa umetoka nyumbani kwake"
Haraka haraka aliinuka alipokaa na kuondoka hadi stendi Tabata Shule alipanda daradara hadi Tabata Chama. Safari yake iliishia hadi msikitini akaomba apelekwe nyumbani kwa Imamu Shafii, muumini mmoja alimpelekea mpelelezi hadi nyumbani kwa Imamu Shafii. Mpelelezi alipofika nyumbani kwa Imamu Shafii alikutana na mke wa Imamu Shafii Salama Selemani au Mama Muu, mpelelezi alijitambulisha kama askari mpelelezi na kuanza kumuhoji mke wa Imamu Shafii.
“Naomba ushirikiano wako ili kufanikisha upelelezi?”
“Usijari mheshimiwa najua uwepo wenu kwa hiyo ruksa unaweza kuniuliza chochote!”
“Unaweza kuniambia matatizo yote yaliyomkuta mume wako yametokana na nini?”
“Kwa kweli sijui ni taarifa ya ghafla”
Mpelelezi alifikiria kidogo aliendelea.
“Hakuna mtu yeyote walikuwa na utofauti baina yao aidha msikiti au hapa mtaani?”
Mke wa Imamu alifikiria na anakumbuka.
“Kuna siku mume wangu alirudi akiwa ayupo sawa lakini nilipomdadisi zaidi akaniambia amegombana na mtu mmoja ila akuniambia ni nani?”
“Siku gani?”
“Muda kidogo kabla ya tukio”
“Huyo mtu wa dini gani?”
“Muislamu”
Mpelelezi alifikiria kidogo aliendelea kumuuliza.
“Huo ugomvi ulikuwa wapi na ulifanyika siku ngapi?”
“Sijajua maana mimi nilijua kama amegombana na mtu kwa hali aliorudi nayo nyumbani ya hasira wakati sio kawaida yake”
Mpelelezi alifikiria kwa muda aligundua ugomvi hule hule aliombiwa na waumini msikitini ndio huo wote.
“Sawa mama kwa ushirikiano wako”
Waliagana na mpelelezi aliondoka hadi kituo cha polisi anapofanyia kazi. Alipofika akutaka kuilaza akili alichukua faili la tukio hilo la dereva bodaboda na Imamu Shafii alianza kulipitia hilo faili ndipo aligunduua preti namba za pikipiki iliokuwa katika hiyo ajari. Hapo hapo aliona njia ya kufanikisha upelelezi wake katika hiyo preti namba ya pikipiki. Alitoka chumba cha upelelezi alienda hadi kwa askari mtunza vifaa vya watuhumiwa na ushahidi aoneshwe pikipiki ya dereva wa pikipiki aliokutwa nayo amekufa.
Askari mtunza vitu hivyo alimpeleka mpelelezi hadi ilipo hiyo pikipiki zikiwa na pikipiki nyingine. Alimuonesha hiyo pikipiki na mpelelezi aliangalia preti namba ya hiyo pikipiki namba za usajiri MC669 BG....
Lakini siku ya kufa nyani miti yote utereza, pikipiki ilikuwa imeungua hadi eneo la preti namba, namba hizo zilikuwa azijatimia sehemu kidogo ya kipande cha kibati cha preti namba kimeungua. Herufi hiyo ya mwisho ilikuwa aieleweki ni herufi gani kama b au p au d kwa hiyo ilikuwa ngumu kuijua herufi hiyo.
Mpelelezi alijiona mkosaji na mtu asiyefikia malengo yake kwa wakati, akili ilimvuruga kutaka kufikia kuchanganyikiwa maana kila analopanga linakuwa gumu kufika mwisho. Akujua afanye nini mpaka kujua hiyo herufi ya mwisho lakini akili ilimtuma akitoe hicho kibati cha preti namba akakipige msasa anaweza kujua hiyo herufi ya mwisho.
Iliitajika kazi ya ziada ya kuanza kung’oa hicho kibati cha preti namba, aliidondosha chini hiyo pikipiki na kuilaza upande wa kulia ukiwa umelalia chini na upande wa kushoto unaangalia juu. Alianza kung’oa hicho kibati cha preti namba lakini akiwa katika purukushani za kung’oa hicho kibati akiwa amekaa kwa kuchutama mara aliona namba zikiwa zimejipanga kwa urefu kuelekea juu. Aliacha kung’oa hicho kibati cha preti namba na kuzikagua hizo namba zikiwa zimeandikwa *MD2A21BZ3EWD56895*.
Mpelelezi alipoziona hizo namba alitabasamu, haraka haraka alitoa peni mfukoni na kitabu chake cha kumbukumbu aliziandika hizo namba. Alipomaliza anairudisha pikipiki kama ilivyokuwa na aliondoka hadi kituo cha Tabata Shule alipanda daradara lakini safari yake iliishia makao makuu ya Tra.
“Naomba kujua juu ya hizi namba usajiri wake”
Aliwaonesha hizo namba. Tra walipoziona hizo namba wanagundua ni namba za chechesi ambazo zinapatikana katika pikipiki mbele ya pikipiki katika bomba linalounganisha na vifaa vingine vya pikipiki karibu na injini. Waliziingiza hizo namba katika mashine walianza kutafuta maelezo ya kina juu ya hizo namba za chechesi katika mashine.Baada ya kusachi katika mashine yao zilileta namba za injini ya pikipiki, preti namba, jina kamili la mmiliki wa pikipiki pamoja na namba yake ya simu.
Mpelelezi alifurahi sana aliona anakwenda kufika mwisho wa upelelezi wake na kesi kiujumla. Aliwashukuru watu wa Tra lakini huo ni mwanzo wa mafanikio sio mwisho ili kufikia mwisho wa mafaniko aliomba kitu kutoka Tra.
“Naomba mumpigie simu huyo mmiliki aje hapa nina mazungumzo nae, naomba msaada wenu?"
Tra walifanya kama walivyoambiwa kwakuwa mpelelezi alijitambulisha kama askari mpelelezi, hivyo waligundua yupo katika majukumu ya kazi ya upelelezi ili kufanikisha upelelezi wake. Walimpigia simu huyo mtu ambae jina lake limepatikana baada ya kuingizwa namba chechesi katika mashine ya Tra wanamwita hapo makao makuu yao. Huyo mtu baada ya kuitwa na Tra aliitikia wito anaenda lakini alipofika hapo makao makuu ya Tra aliwekwa chini ya ulinzi. Mpelelezi moja kwa moja alijua huyo ndio mtuhumiwa wa tukio zima la dereva bodaboda na Imamu Shafii kwakua ndio mmiliki halali wa hiyo pikipiki iliokutwa katika tukio. Mpelelezi alijitambulisha kwa huyo mtu kama mpelelezi na alianza kummfanyia mahojiano.
“Bila shaka wewe ndio mmiliki halali wa pikipiki ya usajiri wa namba MC669 BGA?”
“Ndio”
“Mara ya mwisho pikipiki yako kuitumia ni lini?”
Huyo mtu alisikitika baada ya kuulizwa mara ya mwisho kutumia pikipiki yake.
“Daa! Mmenikumbusha majonzi niliokuwa nishayasahau”
"Kwanini?"
“Mara ya mwisho pikipiki yangu nilimuachia ni dereva wangu ambae alikuwa ananifanyia kazi kama dereva bodaboda lakini hadi kufika jioni napokea taarifa amekutwa amekufa maeneo ya bonde la mchicha Tabata Mawenzi”
Wote walishangaa juu ya taarifa hiyo lakini mpelelezi aliendelea kumuuliza ili kujua ukweli.
“Lini?”
“Yapata sasa miezi sita tangu litokee tukio ilo”
Mpelelezi alitabasamu huku imani yake ikisadiki ni uongo,
“Sikia ndugu, mpaka nimekuita hapa kwa jambo moja tu, pikipiki yako ipo chini ya mikono ya polisi imekutwa eneo la tukio la mauaji”
“Mauaji.......!!?”
"Ndio"
“Wapi?”
“Tabata Mawenzi, kituo cha Chama eneo la darajani”
“Lini?”
“Miezi minne ilizopita”
Huyo mtu mmiliki wa pikipiki alitetemeka na kusababisha mpelelezi kumshangaa pamoja na watu wa Tra.
“Sio kweli”
“Sio kweli kwanini wakati ushahidi wote upo na pikipiki imekutwa na preti namba zako baada ya uchunguzi kwa kina katika mitambo ya Tra limetoka jina lako na namba yako ya simu”
“Ni kweli ilo ndilo jina langu na hiyo ndio namba yangu ila hiyo pikipiki imeibiwa miezi sita iliopita na dereva wa pikipiki hiyo ameuliwa kinyama amechinjwa kichwa na kutenganishwa na mwili”
Mpelelezi na watu wa Tra walishangaa mpaka wengine walishtuka.
"Kuna watu wana roho mbaya kumuua binadamu mwenzako kama kuku"
“Roho iliniuma sana, nimenunua jumatano, jumamosi pikipiki inaibiwa, imedumu siku tatu, kubwa zaidi kilichoniuma dereva wangu waliomuua bora wangeiba pikipiki wao wakamuacha hai”
Mpelelezi aikumuingia akilini anajua huyo mtu mmiliki wa pikipiki anakwepa hiyo kesi wakati pikipiki iliokuwa katika tukio ndio yake.
“Sawa ila ulitoa taarifa kituo cha polisi baada ya tukio ilo kutokea?”
“Ndio nilitoa kituo cha Tabata Shule na kesi bado ipo katika uchunguzi lakini mpaka dakika hii watuumiwa awakukamatwa na mimi nimechoka kufatiria nimemuachia mungu”
“Rb unayo?”
“Ndio ninayo”
“Naomba”
Nimeiyacha nyumbani maana sitembei nayo mara kwa mara”
“Ok!...tunaweza kwenda”
“Sawa! Twende”
Aliinuka huyo mtu ili kuanza kuondoka lakini mpelelezi alimwita.
“Naomba nikufunge pingu kwa usalama zaidi”
“Usijari fanya kama kazi yako inavyokuruhusu”
Alinyoosha mikono mpelelezi anamfunga pingu huyo mtu mmiliki wa pikipiki anawaaga watu wa Tra wanaondoka. Ulikuwa mwendo wa nusu saa hadi kufika nyumbani kwa huyo mtu mmiliki wa pikipiki Tabata Segerea mwisho wanafika anaingia ndani anatoa Rb anampa.Ndipo hapo mpelelezi alithibitisha na wanaambatana kwa pamoja hadi kituo cha polisi Tabata Shule alipofungua kesi hiyo. Walifika, mpelelezi anatafuta faili ya kesi yake anaangalia anathibitisha huyo mtu pikipiki yake lakini imeibiwa na dereva wake ameuliwa kinyama.
Mpelelezi aliferi tena kwa mara nyingine kufanikisha kumpata muuaji wa dereva wa bodaboda. Alimruhusu huyo mtu mmiliki wa pikipiki na kumuomba samahani kwa usumbufu. Huyo mtu mmiliki wa pikipiki akuwa na la ziada anaondoka zake. Mpelelezi alifikiria juu ya kesi hiyo jinsi ya kufanikisha lakini bila majibu. Alitoka hapo kituoni alipanda daradara maeneo ya buguruni anaelekea Tabata Kimanga lakini akiwa njiani linamjia wazo.
“Uwezi kujua yaliopo ndani lazima uingie ndani kwa hiyo kuna ulazima kufatiria kesi ya pikipiki ilioibiwa na dereva wake kuchinjwa utakapo wapata wauaji hao utafanikiwa kuwapata wauaji wa dereva wa bodaboda wa kesi inayokusumbua”
Baada ya kupata wazo hilo alishuka kituo cha mbele anapanda gari la Segerea anaelekea Segerea. Akiwa ndani ya gari alimpigia simu yule mtu mmiliki wa pikipiki ambae dereva wake kauliwa kwa kuchinjwa.
“Upo wapi?”
“Nyumbani”
“Nakuja ili unipeleke nyumbani kwa yule dereva wako kuna vitu nahitaji kujua ili niifatirie kesi yako kwa undani nikusaidie kuwapata wauaji na wezi wa pikipiki yako”
“Sawa poti njoo”
“Ok! Kama dakika kumi na tano nitakuwa hapo”
Walikubaliana anakata simu anaweka mfukoni. Gari iliendelea na safari hadi inafika Segerea, mpelelezi anashuka anaenda moja kwa moja hadi kwa yule mtu mmiliki wa pikipiki. Walikutana wanaelekea moja kwa moja hadi nyumbani kwa yule dereva. Walikutana na familia ya dereva alieuwawa kwa kuchinjwa. Baada ya kufika mpelelezi alijitambulisha, bila kupoteza muda na anaanza kuuliza maswali mawili matatu.
“Marehemu hana muda gani na kazi ya bodaboda?”
“Tangu alipomaliza kidato cha nne aliingia katika bodaboda nilimwambia sitaki kazi hiyo nenda veta lakini akunisikia"
“Baba hiyo mipango ya mungu, mimi naomba kufahamu uzoefu wake katika kazi yake ya bodaboda”
Baba wa dereva wa bodaboda alitawariwa na uzuni kwakua amekumbushwa tukio la kinyama alilofanyiwa mtoto wake hivyo aliongea kwa majonzi.
“Tangu amalize kidato cha nne mwaka 2009 hadi mwaka jana 2019 ndio umauti unamkuta”
“Mara ya mwisho aliondoka saa ngapi nyumbani na aliaga anaenda wapi?’
“Tangu alipoanza kufanya kazi ya bodaboda tulianza kupishana kiswahili baada ya kumwambia kazi ya bodaboda sitaki aende veta kusomea ufundi akaamua kuama nyumbani kwenda kupanga na kujitegemea kwa hiyo kuja hapa nyumbani mara moja moja kuja kunisalimia tu”
“Kwa hiyo siku aliokufa akuwai kuja hapa nyumbani labda kukwambia anaenda wapi?’
“Hapana kama siku tatu ajafika nyumbani kunisalimia lakini ya nne nikapokea taarifa ya kifo chake nilishtushwa japo nilikuwa sipendi hiyo kazi yake lakini damu nzito kuliko maji iliniuma sana”
Baba alianza kutokwa na machozi lakini mpelelezi anamtuliza ili asilie.
“Pole mzee wangu hayo yote ni mipango ya mungu ila ni mbali na hapo alipokuwa amepanga na kuanza maisha yake?”
“Kwa kweli sijawai kufika hata siku moja nilisikia tu amepanga lakini sijawai kufika”
“Mimi napajua alipokuwa amepanga”
Huyo mtu mmiliki wa pikipiki alimwambia mpelelezi.
“Sawa! Itakuwa vizuri kama tutafika”
“Sawa!”
Mpelelezi na huyo mtu mmiliki wa pikipiki waliaga familia ya huyo dereva bodaboda wanaondoka hadi nyumba aliopanga dereva wake. Walipofika wanakuta wapangaji wenzake wanajitambulisha na wanaomba kuonana na mama mwenye nyumba au baba mwenye nyumba. Mama mwenye nyumba aliitwa anafika anakutana na mpelelezi wanasalimiana baada ya salamu mpelelezi alijitambulisha na kuanza kuongea kilichomleta.
“Mara ya mwisho lini kuonana na mpangaji wako Michael”
“Niliondoka yeye akiwa katika kazi yake, nikiwa huko nilipoenda nikapokea taarifa ya kifo chake”
“Kwa hiyo mpaka unaondoka amjaonana?”
“Ndio”
“Waliokuwepo kina nani?”
“Wapangaji wenzake”
“Naomba niitie”
Wapangaji wote waliitwa wanakusanyika wanaanza kuulizwa maswali na mpelelezi.
“Mara ya mwisho Michael aliaga anaenda wapi?”
Wapangaji baada ya kuulizwa swali ilo walikuwa wanaangaliana wanajishauri kujibu lakini mmoja anajibu kwa niaba ya wenzake.
“Alitoka asubuhi kama kawaida yake na kwenda kazini kwake”
“Akurudi tena mchana na kusema anaenda sehemu?”
“Hapana! alipotoka asabuhi akurudi hadi siku ya tatu tukapokea taarifa ya kifo chake”
“Kutoka kwa nani mlipata taarifa hiyo?”
“Kwa dereva bodaboda wenzake anapofanyia kazi”
“Kwa hiyo asubuhi alipotoka akuaga anaenda wapi?"
"Ajaaga na sio kawaida yake kuaga"
"Hata kurudi kwa siku hiyo ajarudi hadi mnapokea taarifa ya kifo chake”
“Ndio”
Wapangaji walijibu wote kwa pamoja, mpelelezi akuwa na la ziada anawashukuru kwa ushirikiano wao anaaga anaondoka na huyo mtu mmiliki wa pikipiki hadi Segerea stendi. Walipofika hapo stendi ya daradara Segerea, mpelelezi aliagana na huyo mtu mmiliki wa pikipiki alipanda gari anaondoka zake. Akiwa njiani alifikiria maelezo yote ya watu aliowahoji ndipo yanafungua ubongo wake japo alikuwa anaferi katika kufanikisha lakini anajipa moyo atafanikiwa kuwajua wauaji wa dereva boda boda kwa kuchinjwa kutokana na maelezo aliopewa.
“Mungu awezi kumtupa mtu mwenye dhamira ya kweli, hawezi kata tamaa hawezi kushindwa”
Alishuka Tabata Shule alienda kituoni anapofanyia kazi. Alipofika anasaini katika daftari la maudhurio anaondoka zake hadi nyumbani kwake kupumzisha akili yake.
Siku iliofuta anapata akili nyingine ya kufanikisha upelelezi wake. Alikwenda anapanga chumba maeneo ya Kinyerezi. Alitoka katika umbo la askari mpelelezi na kuwa katika muonekano wa raia mwema. Alishirikiana na O.S.S mkuu wake wa upelelezi wananunua pikipiki. Baada ya kununua pikipiki alienda kuanza kazi ya kubeba abiria katika kituo cha daradara Tabata Segerea kama bodaboda.
Kutokana na ugeni wake alipata shida kuzoeleka, kuwazoea, kuzoea mazingira na kuzoea hali ya kuwa raia mwema. Ilikuwa ngumu sana kwa upande wake lakini anajitaidi kadri ya uwezo wake.
Siku zilisogea na anafanikiwa kuzoeleka na akawa anabeba abiria vizuri na kuwapeleka sehemu mbalimbali za Segerea. Lakini hela aliyokuwa anapata baada ya kubeba abiria anaimaliza katika starehe ya kunywa pombe, mademu kwa sana na kujirusha club kama Forty Forty iliopo bima, The Great iliopo Barakuda na Kwetu Pazuri iliopo njia ya Segerea kituo cha Sanene. Tabia hiyo ilipelekea kupata marafiki ambao wavuta bange, wanywaji wa pomnbe na wapenda starehe kwa kujirusha na wanawake leo huyu kesho yule ambao ni madereva bodaboda wa eneo hilo la Tabata Segerea.
Staili hiyo ya maisha mpelelezi ilimfanya kujulikana haraka kwa jina la kazi na dawa maana pikipiki yake aliiandika kazi na dawa na kutokana na vitendo vyake vya starehe alijizolea umaarufu mkubwa na kupendwa na dereva wa boda boda wenzake ambao wanywaji wa pombe. Siku nyingine akikosa pesa wenzake wanamnunulia pombe. Lakini matumizi yake mpelelezi yanakuwa ni tofauti na hao bodaboda wenzake yeye matumizi yake ya elfu sabini hadi laki moja na wakati mwingine kiwango kinashuka hadi elfu hamsini lakini cha kushangaza hao bodaboda wenzake kwa siku moja wanatumia pombe za laki na nusu hadi laki mbili.
Wakati hata ufanyaji wao wa kazi wa kusua sua na muda mwingi pikipiki zao wanawapa watu deiwaka. Mpelelezi alipata maswali mengi juu ya hao dereva bodaboda wenzake wanapopata pesa za kunywa pombe kila siku ya mungu wakati pikipiki zao wanatoa deiwaka na hesabu wanakamilisha vipi?. Kwakua alitaka kujua chanzo cha upataji pesa cha hao bodaboda wenzake na kubwa zaidi kujua muuaji wa dereva bodaboda alieuliwa kwa kuchinjwa kichwa. Alimuandaa mtu kama bosi wake wa pikipiki na kumfuata kijiweni kwake na kuhitaji hesabu yake ya wiki nzima. Mpelelezi alitoa hesabu nusu ndipo anapogombana na huyo bosi wake wa kumuandaa na kupewa onyo asipotimiza hesabu kwa wiki nyingine atampokonya pikipiki.
Hali hiyo iliendelea kwa mpelelezi unywaji wa pombe na matumizi yasiokuwa na mpango huku dereva bodaboda wenzake wakimshauri akamalishe hesabu lakini yeye akuwajari wala kuwasikiliza, aliendelea kufanya sterehe kila siku ya mungu. Siku akikosa pesa anauza vitu vya ndani kwake mara deki, mara sabufa, ilifika hatua aliuza hadi simu yake aliokuwa anatumia. Tena alikuwa anauza madalali madereva bodaboda wenzake na hela anaimalizia katika pombe. Aliendelea na hali hiyo na anampanga tena yule mtu wake aje kumdai hesabu ya pikipki. Alifika anamdai mpelelezi anajifanya hana hesabu. Huyo bosi wa kuandaliwa anampokonya pikipiki mpelelezi.
Baada ya kupokonywa pikipiki mpelelezi, ndani ya wiki moja alijifanya shida zimemuandama anaaanza kuomba msaada wa pesa ya kula na matumizi mengine kwa dereva bodaboda wenzake aliokuwa anakunywa nao pombe.Dereva bodaboda wenzake aliokuwa anakunywa nao pombe wanamsaidia kutokana walikuwa wanakunywa wote pombe. Lakini kadri alivyokuwa anasaidiwa anazidi kuomba zaidi na kueleza shida mbalimbali ndipo mmoja wa hao aliokuwa anakunywa nao pombe anamchoka na anamsema kwa tabia hiyo.
“Ndugu yangu kiukweli wazi plan b umekosa?”
“Kivipi?”
“Washikaji wote wamekuchoka kuomba omba kila siku”
"Hata mimi najisikia vibaya kuomba omba kila siku ila sio kama napenda ni shida ndugu ila kama vipi naomba msaada wako"
"Msaada upi?"
"Kama kuna bosi wa pikipiki anipe maisha"
"Sasa wewe umepewa pikipiki umeshindwa kupeleka hesabu sasa hata ukipewa pikipiki nyingine hesabu ya watu itafika"
"Itafika"
"Sio kweli, hapo umekosea mwenyewe na siku zote acha kazi uone ugumu kupata kazi"
"Daa! ni kweli ndugu yangu"
“Ndio hivyo ila mimi sina bosi wa pikipiki maisha yangu yote nategemea deiwaka”
“Deiwaka?”
“Yah! Usumbufu na mabosi siwezi”
“Sasa deiwaka ndio inakupatia pesa za pombe ndugu?”
“Ahaa!! Mjini hapa mishe nyingi”
Mpelelezi aliposikia, akili fasta ilinasa anachotaka kuongea anabadilisha.
“Mishe nyingi na mimi si unipe mishe au unapenda wakiumeni mwenzako niwe naomba omba hata nikipata demu hela ya nyumba ya wageni nije kuomba”
“Utaweza wewe?”
“Acha! dharau bwana mimi mtoto wa kike mpaka nishindwe, leta dili nijimwae mwae”
Huyo dereva bodaboda alicheka anaangalia huku na huko anasogea karibu na mpelelezi anaongea kwa sauti ya chini.
“Ishu za hatari kama unaweza fresh ila kuuza roho nje nje”
Mpelelezi alishangaa huku ametoa macho kama panya kabanwa na mlango.
“Kama?”
“Kuiba pikipiki”
Mpelelezi alijisemea kimoyo moyo.
“Nashukuru mungu naelekea kufahuru mtihani wangu”
Anashusha pumzi.
"Unaona ushaanza kuogopa"
"Hakuna! si nimepumua tu!"
“Ok! ila tunaiba mtaani kama hapa kijiweni kwetu, ila kama mimi siibi hapa naenda kijiwe labda cha mbagara baada ya kupewa taarifa na mwenzangu ambae yupo katika chama hiki, maana tupo wengi kila kijiwe cha bodaboda wapo, endapo akija mtu na pikipiki mpya nawajulisha makao makuu anatumwa mtu kutoka kimara anapewa mchongo wote hadi pikipiki preti namba za pikipiki anapewa na kulengeshwa vizuri kwa hiyo kama utaweza fresh ila kazi kazi si unajua raia”
Mpelelezi akutaka kufikiria alijua akifikiria kujibu ataonekana awezi haraka haraka alikubali ili afike malengo ya upelelezi wake japokuwa anaona anauza roho yake.
“Tunaishi nao raia kazi kazi hiyo ishu ndogo tu!"
"Utaweza"
"Unanionaje kwani?"
“Poa! Ila sipo peke yangu kuna bosi ndio mpango mzima na hizo pikipiki tunapoziiba tunatoa injini zinapelekwa kuuzwa bagaboyo kuwekwa katika boti”
“Poa aina shida nikutanishe na huyo don”
“Pamoja sana”
Waliagana kila mmoja anaondoka zake, mpelelezi alielekea nyumbani kwake lakini njia nzima mpelelezi anafikiria sana juu ya hiyo kazi kwakua ni kazi ngumu ya wizi wa pikipiki ni kuuza roho kwa raia, kama unavyojua raia walivyokua na hasira kali. Aliingiwa na uoga hadi anafika nyumbani kwake alikuwa anafikiria aende katika hicho chama cha wizi au asiende. Akiwa njia panda bila kujua uhamuzi gani ahamue, inamjia sauti fulani alioifananisha na malaika.
“Ulikula kiapo utalitumikia jeshi la polisi mpaka mwisho wa tone la mwisho wa damu yako”
Kauli hiyo ilimuondoa hofu na inampa matumaini ya kuingia katika hicho chama cha wizi wa pikipiki.
"Ndiyo mwanzo wa kufanikiwa upelelezi wako"
Baada ya kushawishiwa na sauti aliofananisha na malaika, aliamua kujiunga na hicho kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani. siku ya pili aliambatana na huyo dereva bodaboda waliokuwa wanakunywa wote pombe hadi makao makuu ya hicho chama cha wizi wa pikipiki. Walipofika wanaelekea moja kwa moja hadi kwa mkuu wa hicho chama ofisini kwake lakini kwa bahati mbaya awakuweza kumkuta. Walimkuta msaidizi wa hicho kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani.
“Kiongozi nimemleta mtu wa kazi, namuamini na hana tatizo lolote”
Kiongozi msaidizi wa hicho kitengo cha wizi wa pikipiki alimwangalia mpelelezi kama anamfananisha kuna sehemu aliwai kumuona, mpelelezi nae alimkazia macho huyo msaidizi wa hicho kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani akimuangalia. Waliangaliana kwa muda, baadae alikubaliwa kujiunga katika hicho kitengo cha wizi wa pikipiki, aliandikwa jina lake na namba yake ya simu na kuambiwa ataitwa siku yeyote kuja kuanza kazi.
Mpelelezi aliondoka na huyo dereva bodaboda hadi kijiweni kwao wanaachana hapo kila mmoja anaenda njia yake. Mpelelezi alienda hadi stendi ya daradara alipanda gari anaelekea hadi nyumbani kwa mkuu wake wa upelelezi ambae ni O.S.S.
"Nimekijua kitengo ambacho kinashughurika na wizi wa pikipiki mtaani"
"Kipo wapi?"
"Temeke muembe yanga kuna gereji moja inaitwa Scorpion"
"Vizui sana!"
"Kwakuwa tumekifahamu hicho kitengo, natumaini itakuwa njia moja wapo ya kuwagundua wezi wote wa pikipiki mitaani, kupitia hao wezi tutafahamu hata mauji ya dereva bodaboda aliechinjwa kichwa na endapo tukiwafahamu wauaji wa dereva huyo ndio tutafahamu wote waliohusika katika tukio la Tabata Mawenzi"
"Vizuri! sasa tujiandae kwenda kuvamia ili kuwatia nguvuni”
“Hapana! Maana hata tukiwakamata hatuna ushahidi wa kukamilika ngoja tuwapeleleze kwa undani tukiwajua vizuri tunawakamata wakiwa na vizibiti”
“Sikiliza ujue ni hatari kwako?”
“Kivipi mheshimiwa?”
“Kuingia katika wizi wa pikipiki mtaani! si unajua raia walivyo na hasira kali”
“Kuwa na amani mheshimiwa aitatokea tendo ilo si unajua uwezo niliokuwa nao?”
“Uwezo ulionao mbele ya raia wenye hasira kali?”
“Kuwa na amani kazi itaenda vizuri”
“Sawa!”
O.S.S alikubali kwa shingo upande wanaagana na mpelelezi anaondoka. O.S.S baada ya kupata taarifa hiyo alimpigia simu kiongozi wake ngazi ya juu ya upelelezi ambae ni R.C.O
“Mheshimiwa kijana wetu amefikia hatua nzuri”
“Hatua ipi?”
“Ameshafanikiwa kulijua genge la wizi wa pikipiki ambao wanaziiba mtaani kwa raia kwa hiyo tutafanikiwa kumjua muuaji wa yule dereva bodaboda"
"Vizuri sana!"
"Ila hao watu mtandao wao mkubwa sana wana kampuni na wanachama wapo kila sehemu yenye kituo cha bodaboda”
“Ni wapi kilipo hicho kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani?”
“Temeke muembe yanga kuna gereji moja inaitwa Scorpion”
“Weka vijana vizuri ili tuwatie nguvuni na kuteketeza hicho kitengo”
“Sawa mheshimiwa lakini wana kila sehemu wanachama kwa hiyo ngoja tuwagundue wote tuteketeze genge lote na wanachama wote”
Walikubaliana, waliagana O.S.S anakata simu.
**********
Mpelelezi baada ya kuachana na mkuu wake wa upelelezi O.S.S hakutaka tena kuelekea kituoni siku hiyo. Aliondoka na kwenda nyumbani kwake ambako alikwenda kujipumzisha. Akiwa katika usingizi mzito uliochanganyika na uchovu ilimjia ndoto akiwa ametekwa na watu wasiojulikana anapigwa hadi anakuwa hoi hoi. Mbali na hapo alipokuwa anamuona mtu anatoa amri auliwe na hao wanaopiga.
Mpelelezi alipepesa macho anajitaidi kumuangalia huyo mtu ili amjue ni nani lakini mboni za macho zilishindwa kuona mbali kutokana na kipigo alichopigwa. Huyo mtu aliendelea kutoa amri ya kumuua lakini mpelelezi sauti ya mtu huyo alihisi sio ngeni masikioni kwake lakini akumbuki wapi aliwai kuisikia sauti ya mtu huyo. Akiwa katika kuifikiria sauti ya mtu huyo anaetoa amri ili auliwe ndipo hapo mpigaji mmoja alichukua nondo anampiga nayo ya kichwa mpelelezi. Hapo hapo mpelelezi alizinduka kutoka katika usingizi mzito na ndoto inatoweka. Hali hiyo ilimuogopesha sana mpelelezi huku akiwa anaitafakari hiyo ndoto.
“Mungu wangu kwanini ndoto hii”
Ndoto hiyo ilimsumbua sana mpelelezi na ilimnyima amani ya roho anashindwa afanye nini?. Aliomba kwa imani ya dini yake lakini alipomaliza kuomba bado amani ya roho aikuwepo kabisa katika akili yake. Ilifika muda alitawariwa na hofu juu ya kesi hiyo anayoifatiria lakini kutokana amekula kiapo atalitumikia jeshi la polisi mpaka mwisho wa maisha yake, alipata nguvu ya kuendeleea kufatiria hiyo kesi. Kwa hiyo mipango mingi iliendelea kichwani mwake. Ambayo akitaka kufika mwisho wa kesi anayoifatiria na ili afike mwisho wa kesi hiyo ilikuwa ni lazima aingie katika hicho kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani.
Hakuwa na njia nyingine ya kufanikisha upelelezi wake, zaidi ya kujiunga na hicho kitengo cha wizi wa pikipiki cha temeke muembe yanga katika gereji ya Scorpion. Alichofanya siku iliofuata ni kumfuata O.S.S ambae ni kiongozi wake alimuelezea juu ya ndoto zinazomuandama.
“Ndoto siku zote ni kama hadithi hazina ukweli wowote, unaweza ukaota tajiri lakini ukiamka asubuhi umasikini bado upo pale pale"
“Sawa lakini muda mwingine nakuwa kama napewa maono na malaika na kunikataza kufatiria hii kesi”
“Sawa ndio maana nikamwambia ndoto kama hadithi au wewe unatakaje?”
“Zinaniogopesha sasa naomba uniongeze nguvu maana kidole kimoja akivunji chawa”
“Ohooo!......sasa wewe unaona nani atakufaa?”
Alicheka huku anainama chini.
“Niambie?”
“Yule yule adui wa mke wangu”
“Nilijua kama ni Muona ila sawa nadhani unajua ukiwa na Muona mnakuwa mnafanya kazi vizuri na kuelewana kama mapacha japokuwa mke wako anajua nyumba ndogo yako”
“Ndio akili za wanawake ila mimi na Muona damu damu na tunaheshimiana sana”
“Sawa Muona akifika nitamfikishia taarifa”
“Sawa kiongozi nakutegemea”
Mpelelezi na mkuu wake wa upelelezi walikubaliana katika majukumu ya kikazi ya kuongeza nguvu ili kufanikisha upelelezi katika kitengo cha wizi wa pikipiki. Lakini kabla ajaondoka akiwa hapo anapokea simu kutoka katika kitengo cha wizi wa pikipiki na kuhitajika haraka. Alimuaga mkuu wake wa upelelezi anaondoka.
Alipanda daradara kituo cha Tabata Shule anaelekea temeke. Ulikuwa mwendo wa dakika arobaini na tano kutoka kituo cha polisi Tabata Shule hadi Temeke. Alifika makao makuu ya kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani anakutana na yule rafiki yake dereva bodaboda na wenzao wawili. Jumla ilikuwa timu ya watu wanne walipewa hoda ya kwenda kuiba pikipiki Mbagara Maji Matitu. Baada kupata taarifa kwa njia ya simu na mwanachama mwenzao wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani Scorpion Gereji ambae anafanya kazi ya bodaboda hapo kituo cha Maji Matitu kuwa kuna mtu katika kijiwe chao amenunua pikipiki mpya aina ya Boxer.
**********
Mpelelezi na yule jamaa yake na mwenzao mmoja walioneshwa kupitia simu picha ya huyo jamaa mwenye pikipiki wanayoenda kuiba, pikipiki wanayokwenda kuiba na preti namba za hizo pikipki. Baada ya kupata maelezo hayo walipanda pikipiki moja waliondoka lakini yule mwenzao anachukua haisi ambayo aikuwa na kiti hata kimoja.
Mpelelezi alishangaa kuona hiyo haisi aina siti hata moja na wanaenda nayo huko katika kuiba pikipiki, alishindwa kujua ina kazi gani hiyo haisi wakati aina siti hata moja. Waliambatana na hiyo haisi safari moja na kuelekea Mbagara Maji Matitu. Walipofika Mbagara Rangi Tatu, walimshusha mpelelezi katika pikipiki.
“Panda daradara linaloelekea Chamanzi shuka kituo cha Maji Matitu jamaa umemuona na pikipiki umeiyoa na preti namba umeziona kwa hiyo ukifika mkodi njoo nae hadi Chamanzi, ukifika Chamanzi tutakuelekeza kwa kuja nae tutajifanya kama ndugu zako unapokuja upajui sawa sawa!”
“Ndio”
Bila kupoteza muda wenzake waliwasha pikipiki wanaondoka. Mpelelezi alibaki hapo Mbagara Rangi Tatu peke yake akiwa na mawazo kibao huku imani yake ikisadiki anakwenda kuchukua haki ya mtu kinguvu. Roho ilimuuma sana na anajishauri mwenyewe aende au asiende na aondoke ahachane na hiyo kazi lakini ilimjia sauti ambayo anaifananisha na malaika.
"Hata ukiondoka awakomoi hao wezi, unajikomoa wewe mwenyewe kwa sababu hupo katika upelelezi"
Sauti hiyo alioifananisha na malaika iliendelea kumshawishi ili aende kuiba pikipiki,
"Kwa hiyo una budi kwenda maana ndio njia ya kufanikisha upelelezi wako kwa kesi unayoifatiria"
Ndio hapo mpelelezi alipobaki njia panda bila kujua achukue uhamuzi gani? lakini baada ya kushawishiwa na sauti alioifananisha na malaika anaamua kupanda daradara inayoelekea Chamanzi huku akiwa ameweka msimamo kuwa wakifanikiwa kuiba hiyo pikipiki wasimfanye chochote huyo mwenye pikipiki, hizo zilikuwa fikra zake. Baada ya daradara kujaa safari ilianza njia nzima mpelelezi alikuwa anaomba mungu amsaidie afanikiwe katika hiyo kazi ya kuiba pikipiki, amuepusha na kukamatwa na raia wenye asira kali na arudi salama. Akiwa katika sala hiyo mara simu yake inaita, anaitoa mfukoni anapokea.
"Hupo wapi?"
"Njiani bado sijafika Maji Matitu"
Wenzake walichukia na kuanza kumfokea, kumtukana na kumuona mzembe muda wote anafanya nini ndani ya daradara, lakini anawaambia kuwa gari ilikuwa inajaza abiria kituoni. Baada ya kuwaambia hivyo, simu ilikatwa. Kitendo hicho cha kutukanwa na kudharaulika kama mtoto,na kuonekana mjinga kwakuwa ndio kwanza anaanza hiyo kazi kilimuuma sana mpelelezi lakini anajikaza na kuficha makucha yake kama askari mpelelezi. Konda alitangaza kituo cha Maji Matitu anashtuka kama mtu aliepigwa na shoti za umeme.
"Shusha Maji Matitu"
Kwa sauti kubwa, daradara ilisimama kituoni hapo Maji Matitu na mpelelezi anashuka lakini kitendo cha kushuka tu! hofu ilimtawara mwili unaanza kutoa jasho na anatetemeka. Lakini anajikaza kiume anapepesa macho huku na huko. Dereva wa bodaboda wanamuona anavyopepesa macho, walihisi anataka pikipiki wakaanza kumfata kwa pamoja wakijua abiria.
Mpelelezi akuwa na muda na dereva bodaboda mwingine zaidi anapepesa macho kumuangalia muhusika wake. Aliwapita maderva bodaboda wote wakajua sio mteja kashafika eneo ilo. Dereva wote bodaboda walirudi katika maegesho yao ya bodaboda. Mpelelezi aliwazungruka hao madereva bodaboda na kukagua preti namba moja baada ya nyingine kimya kimya bila wenyewe kujua ndipo anaiyona pikipiki anayohitaji. Baada ya kuiyona alifikiria kwa muda huku akishindana na nafsi yake aende au asiende, lakini kama mtu alieingiwa na pepo anapiga hatua za haraka anasogea katika hiyo pikipiki.
Akiwa anasogea katika hiyo pikipiki mara simu yake inaita anashtuka anaangalia anaona jamaa zake anapokea na wanamuuliza alipo lakini anaikata simu na anazima. Alisogea ilipo hiyo pikipiki anayoitaji anapofika anaongea nae na kumuelezea anapoenda. Dereva wa bodaboda anamuelewa mpelelezi, wanakubaliana bei anapanda wanaondoka. Laiti dereva bodaboda huyo angejua kinachokwenda kutokea huko anapoenda asingeenda ila ndio hivyo mungu ameficha siku ya kuijua baya linalotokea mbele yako. Baada ya mwendo wa dakika kumi na tano wanakaribia Chamanzi anawasha simu na unaingia ujumbe wa maneno kwa mfululizo na mara anapigiwa simu anapokea.
“Upo wapi na kwanini unazima simu?”
“Nimeshafika mliponielekeza wapi nipite”
“Upo nae?”
“Achana na hizo habari nielekeze mimi nishachoka bwana kama ingekuwa mbali nisingekuja sehemu ya kupanda gari unaniambia nipande bodaboda”
“Ok! Nyoosha ilo rodi mbele huku nimesimama njiani nakusubiri”
“Sawa! Nikukute sio tena mimi ndio nakusubiri”
Alikata simu anamwambia dereva wa bodaboda waende hiyo njia alioelekezwa inayoelekea Chamanzi Sekondary School lakini dereva wa bodaboda alisimamisha pikipiki ghafla.
“Kaka huku tunapoenda hela nyingine sasa tukubariane kabla atujaondoka sio tunafika tunaanza kuzungushana?”
“Usijari ndugu yangu nakupa hela nifikishe au kama vipi chukua hii”
Mpelelezi aliingiza mkono mfukoni anampa elfu kumi dereva bodaboda, dereva bodaboda anapokea.
“Utakata hela yako ya kutoka pale uliponitoa hadi huku tunapoenda kama ndogo ukifika utapewa nyingine”
“Sawa!”
Dereva bodaboda aliweka mfukoni hiyo hela anawasha pikipiki wanaondoka, mpelelezi alimuangalia dereva bodaboda mfuko anaoweka hiyo hela. Safari iliendelea lakini wakiwa njiani mpelelezi akatumiwa ujumbe ukifika katika mkorosho mkubwa simama na piga simu kuniuliza nilipo sisi tutakuwa karibu tunakusikia tunatoka tunamdhibiti tunachukua pikipiki. Baada ya kupata ujumbe huo, mpelelezi alimuangalia dereva bodaboda huku alimuonea huruma anatamani hata amwambie warudi ili kuyanusuru maisha yake. Kabla ajachukua hayo maamuzi aliuona huo mkorosho anataka kupiga simu lakini roho ilisita anamuangalia huyo dereva bodaboda roho ya huruma inamtawara. Akiwa katika hali hiyo anaukaribia mkorosho kuupita anaamua kupiga mlio katika simu kujifanya simu inaita.
“Simu inaita, hebu simamaisha pikipiki”
Huku anampiga begani dereva bodaboda, dereva bodaboda akapangua gea akasimamisha pikipiki katika huo mkorosho.
“Ehee kabipu huyu vipi! Ngoja nimpigie”
Alipiga simu haraka haraka dereva bodaboda hana ili wala lile bila kujua kinachoendelea.
“Upo wapi?”
Gafra watu walitoka kutoka walipojificha wanamvamia dereva bodaboda na kuanza kumzibiti mmoja anatoa nyundo anampiga nayo ya paji la uso. Dereva bodaboda anapata maumivu makali anapiga kelele na anaanguka chini anaachia pikipiki. Mwingine alimpiga panga la paji la uso damu zinaruka kama bomba la maji limepasuka, dereva bodaboda anapiga kelele kali. Wanamnyamazisha mdomo kwa kumziba mdomo mara mmoja wa hao wezi anampiga nyundo ya kichwa mara panga la kichwa, mpelelezi anashtuka mpaka anapiga kelele.
“Mungu wangu!”
Alitamani mpelelezi atumie cheo chake lakini ilishindikana alihisi angeweza kujumuishwa na yeye akacharangwa mapanga, alipoa kama maji ya mtungini. Dereva bodaboda kutokana ameshtukizwa na hicho kipigo akuwa na uwezo wa kujiteteta, anapigwa mpaka anakuwa hoi hoi anakoroma, damu zinamchuruzika kila sehemu za majeraha. Wezi waliendelea kumpiga mapanga na nyundo za kichwa, kichwa kinabondeka ili kumuua kabisa kupoteza ushahidi lakini mpelelezi anawazuia.
“Inatosha"
Kitendo hicho wezi wa pikipiki walichukia sana, mmoja wa hao wezi akataka kumpiga mpelelezi.
“Tulia na wewe tutakujumuisha na huyu”
“Wewe unaingia katika kazi hii unakuwa na huruma”
Mpelelezi anakuwa kimya.
“Oya muda maliza tuondoke”
Mmoja alioshika panga anampiga panga la shingo huyo dereva bodaboda na kusababisha kutenganisha koromeo na shingo na kusababisha dereva bodaboda kukuruka kama kuku anaekata roho. Mpelelezi roho ilimuuma sana hata hela yake aliompa alishindwa kuchukua kutokana na huruma. Wezi awakuwa na huruma kabisa, wanamkokota hadi polini wanamtupa wanarudi mmoja anapanda pikipiki ya huyo dereva bodaboda na kuondoka yalo njia yake aliobaki anaendesha pikipiki waliokuja nayo anampakiza mpelelezi na kuondoka zao eneo ilo.
Safari ilikuwa ya mwendo wa haraka ili kupotea eneo ilo kabla awajashtukiwa. Walipita ndani kwa ndani walienda kutokea Mbande na wanakutana njiani na ile haisi ya kampuni yao. Mpelelezi anamuona yule jamaa aliekuwa anaendesha pikipiki ya dereva bodaboda waliomuibia akiwa katika hiyo haisi waliokuja nayo. Ndipo anagundua kuwa hiyo haisi kazi yake kubeba pikipiki zote zinazoibiwa mitaani ndio maana aina siti hata moja.
"Daaa!!"
Masikitiko na huzuni ikiwa imemtawara mpelelezi kwa yule dereva bodaboda huku akitafakari kuwa atapona au atakufa kutokana na kipigo kile alichopigwa.
**********
Walifika makao makuu ya kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani Scorpion Gereji salama bila tatizo lolote wanashusha hiyo pikipiki. Fundi alianza kuifungua na kutoa injini na kutenganisha na vitu vingine. Wezi walikuwa wanapongezwa kwa kazi nzuri huku wakionekana wenye furaha kwa kufanikiwa kuiba hiyo pikipiki. Mpelelezi akuwa na furaha hata chembe kwa sababu akupenda kitendo cha kumpiga yule dereva bodaboda.
Alizidi kuumia inapoingia simu kwa kiongozi msaidizi wa kitengo hicho cha wizi wa pikipiki mitaani kutoka kwa vijana wengine, Kimara, Ubungo, Bagamoyo, Mkuranga na Masaki ya Msanga, Chanika Msumbiji na Mvuti kuwa wamefanikiwa kuiba pikipiki wapo njiani wanarudi. Mpelelezi alijua wote wenye hizo pikipiki zilizoibiwa wamepigwa vibaya kama yule wa Chamanzi au wameuliwa kabisa. Roho ilimuuma sana maana tayari Taifa lishapoteza nguvu kazi na familia za hao wenye pikipiki zilizoibiwa kwao kutakuwa na misiba.
Akili ilimtuma amalize upelelezi wake siku hiyo hiyo apige simu kwa mkuu wake atume jeshi ili wavamie wawatie nguvuni wezi wote. Yalikuwa maamuzi ya kukurupuka yasiyotumia akili, alipofikiria juu ya jambo lililomleta hapo ni kugundua muuaji wa kifo cha dereva wa bodaboda akiwa na Imamu aliamua kuwa mpole ili kuvumilia hiyo hali japokuwa watu wanakufa kila kukicha.
Furaha ndani ya kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani iliendelea kutokana kila aliepewa hoda ya kwenda kuiba pikipiki sehemu aliopangiwa amefanikiwa kazi imeenda poa. Waliamua kujipongeza msaidizi alimtuma mmoja wa vijana wake akanunue kreti tano za bia ili wanywe washereheke mafanikio. Bia zililetwa inakuwa fungua chupa kunywa, wengine wanarudi wanaungana na wenzao na kujumuika pamoja kunywa. Mpelelezi ni mpenda pombe lakini siku hiyo alikuwa kama nguruwe katambuka maboga, akutaka kugusa pombe kabisa. Kutokana na hali iliotokea Chamanzi ya kumpiga dereva bodaboda. Lakini wenzake walishaizoea hali hiyo na wana muda nayo, kuua kwao kawaida kuona damu kama mgojwa na dawa au kiu na maji kwa hiyo walikuwa wenye furaha, lakini mpelelezi akutaka kuonesha hali inayomuumiza katika nafsi yake, muda wote alionesha tabasamu huku anasoma mazingira ya humo ndani bila wao kujua.
Baada ya furaha ya muda mfupi ya kusheherekea kuiba pikipiki mitaani kila mmoja alipewa posho yake ya ufanyaji kazi anaondoka. Kwa mpelelezi pesa yake aliopewa alikwenda kuitoa msikitini na kuwaombea dua wale wote dereva bodaboda walioibiwa pikipiki zao na kuuliwa mungu azilaze mahala pema peponi roho zao na wale wote waliokuwa na hali mbaya baada ya kupigwa warudiwe na afya yao kama zamani.
Alipomaaliza kufanya maombi hayo anaondoka hadi Tabata Segerea alipopanga, alipofika analala kupumzisha akili yake kutokana na uchovu wa siku hiyo.
**********
Wiki moja tu baada ya kujiunga na kitengo hicho mpelelezi alitengeneza mazingira yeye na mkuu wake wa upelelezi O.S.S ili kukamilisha upelelezi wake kwa haraka na ushahidi wa kutosha ili kuwatia nguvuni wezi wote wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani cha gereji ya Scorpion. Aliamini kwa asilimia 100% mazingira hayo yanaweza kufanikisha upelelezi kwa haraka. Alienda moja kwa moja hadi makao makuu ya wizi wa pikipiki mitaani alikutana na kiongozi wake wa kazi alimwambia sehemu kama tatu zenye pikipiki za kuiba. Kiongozi msaidizi wa kitengo hicho cha wizi pikipiki mitaani alipitisha hoda yake, anawaandaa vijana kadhaa wanaungana na mpelelezi wanaenda kuiba hizo pikipiki.
Siku hiyo hiyo jioni walirejea na hizo pikipiki na katika huo wizi mpelelezi alionesha uwezo mkubwa wa kuiba pikipiki hadi wezi wenzake walishangaa kwa uwezo aliokuwa nao. Mpelelezi aliendelea kutoa hoda mara kwa mara na hoda zote wakienda walifanikiwa kuiba pikipiki zote na hizo pikipiki ni mpya kabisa lakini wanaoibiwa wote inakuwa ngumu kuuliwa. Alichokuwa anafanya mpelelezi kwa hao wanaowaibia alikuwa anawazimisha bila kuwajeruhi na siraha yeyete. Wezi wenzake walijua anawaua hata walipokuwa wanawakagua waliamini wamekufa. Wezi wenzake walimkubali sana hadi kiongozi msaidizi wa kitengo hicho cha wizi wa pikipiki.
Mwezi mmoja baadaye, baada ya kuaminika na kila mmoja katika kitengo hicho cha wizi wa pikipiki mitaani katika gereji ya Scorpion.
“Kiongozi nilikuwa na ombi?”
“Ombi gani tena?”
“Hapa naona kuna wanawake wanafanya hii kazi?”
“Ndio “
“Kuna mdada yupo vizuri, namuamini na anaiweza kazi, endapo nikiwa nae katika kazi hii nitafanya vizuri zaidi ya nilioyafanya”
Msaidizi anamwangalia kama dakika tatu anamuuliza swali la kukatisha tama.
“Wewe umezaliwa na mama yako unaonaje usije na mama yako maana ndio aliokuzaa atakulinda muda wote katika hatari na wewe utamlinda muda wote kwa maana hiyo mtafanya kazi vizuri sana?”
“Unamaana gani kiongozi?”
“Una hata miezi sita tangu uingie katika hii kazi, leo hii unataka kumleta mgeni wakati wewe mwenyewe mgeni, huku ukisema una muamini sasa mtamlindana vipi wakati wote wageni?”
“Kiongozi hii kazi ausomei bali tunatumia akili”
“Ndio elimu hiyo”
“Sio hivyo ki……!”
Mara inasikika sauti kutoka mlangoni.
“Sikiliza aiwezekani na aitawezekana”
Mpelelezi na msaidizi waligeuka uso kwa uso na mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipki mitaani Scorpion.
“Bado mgeni auwezi kuleta mgeni naomba uende”
Msaidizi alimpa ishara mpelelezi ya kuondoka, mpelelezi anaelewa anaondoka.
“Kwa kauli zake sina imani nae”
“Kwa nini?”
“Elewa hivyo ila nitazidi kumchunguza”
Mkuu alichukua faili la wanachama anafunua na kuangalia.
“Kuna wageni wangapi wamejiunga?”
“Mpaka dakika hii wewe umesafiri ni mgeni mmoja tu”
“Si ndo huyo alietoka?”
“Ndio! Hakuna zaidi ya huyo”
“Una uhakika huyo mgeni anaweza kazi na mwaminifu?”
“Yah! kwakuwa aliemleta ni mtu wake wa karibu sana na kingine kana uwezo mkubwa sana”
"Uwezo gani?"
"Anaua bila kutoa damu"
"Kivipi?"
"Anatumia mikono kuvunja mshipa wa fahamu, halafu taarifa zote za hizi pikipiki mpya tulizoziiba ni hoda kutoka kwake"
“Sawa! tutaongea vizuri maana sijafika kwangu nimeamua kufika kazini kujua maendeleo”
“Usijari kiongozi kazi zinaenda vijana wanachapa kazi”
“Sawa kazi njema ngoja niwai nyumbani”
Waliagana, Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani anaondoka lakini anapofika katika gari yake kabla ajawasha gari anatoa simu anapiga simu.
“Nahitaji kukukwambia kitu?”
“Kipi tena tajiri wangu?”
“Huyu kijana ulioniambia nimemuona nazidi kukuamini kuwa ni mpelelezi”
“Kwanini?”
“Hata mwezi hana lakini anaomba kuna mwanamke aingie ili wasaidiane katika kazi atafanya vizuri akiwa na huyo mwanamke lakini nimemkataria kabisa nimemfukuza na zaidi nitamfukuza”
“Umefanya kosa"
"Kwa nini?"
“Sikiliza nimeshakwambia usimpinge kwa jambo lolote ili tujue idadi yote wanaoijua Scorpion gereji na wanaofatiria na kuijua hiyo kesi sasa mkubalie maana huyo anaetaka ajiunge hapo anapajua Scorpion gereji na anaijua hiyo kesi na anaifatiria kwa hiyo wote wakijiunga hapo tunapata urahisi kuwamaliza na kupoteza ushahidi wote”
“Sio hatari?”
“Hakuna hatari niamini mimi kwa sababu mimi ndio kila kitu kwao, chochote wanachotaka kukifanya lazima nikijue”
“Sawa mheshimiwa”
Walikubaliana anakata simu, anawasha gari anaondoka. Mpelelezi baada ya kukatariwa ombi lake, alimpigia simu mkuu wake wa upelelezi anamwambia amekatariwa ombi lake. Mkuu wa upelelezi anamwambia mpelelezi asikate tamaa afanye kazi peke yake, mungu atasaidia upelelezi utakamilika.
**********
Kila mwanachama wa kitengo cha wizi wa pikipiki Scorpion anapokea taarifa kutoka makao makuu kuwa wanahitajika, mpelelezi nae miongoni mwao. Bila kupoteza muda kila aliepokea taarifa alifika makao makuu. Walipofika kila mmoja alipewa majuku ya kwenda kuiba pikipiki sehemu zilizoletwa taarifa na wanachama wenzao wa sehemu hizo. Mpelelezi alipangiwa na wenzake wale wale aliokwenda nao kuiba pikipki chamanzi.
Wakiwa wanajiandaa kuondoka mara anafika Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani ambae ni bosi. Alito agizo mpelelezi asiende katika kazi anahitaji kufanya mazungumzo nae. Wezi wenzake walishangaa ghafla mpelelezi anahitajika na bosi aliyakuwa amfahamu lakini awakutaka kufatiria hayo yote waliondoka katika majukumu yao ya kazi. Mpelelezi alitii amri alienda. Alipofika ofisini na kukutana na bosi wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani alitawariwa na wasi wasi huku imani yake ilisadiki uenda labda ameshtukiwa kama yeye ni askari mpelelezi.
“Kubwa zaidi nimesitisha usiende katika majukumu ya kikazi kunakazi nataka kukupa”
Mpelelezi alishangaa sana kusikia anataka kupewa kazi wakati yeye ni mgeni katika kitengo hicho amewaaacha wazoefu. Alizidi kupatwa na wasi wasi.
“Kama unavyojua katika kitengo chetu wapo hadi wanawake lakini siku hizi wanawake wanalinga sana ukiwapigia simu kwenda katika majukumu ya kazi wanatoa visingizio vingi”
Mpelelezi aliposikia hivyo kidogo nafsi yake ilianza kufarijika kabla ajajua dhamira ya bosi wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani.
“Kwa hiyo kama ulivyosema huyo dada anaweza kazi na mkiwa pamoja mnafanya kazi kwa ufasaha?"
"Ndio!"
"Naomba mlete”
“Sawa bosi nitamleta”
“Ok! Kwakuwa wenzako wameenda katika kazi na wakirudi mifuko itanona basi na wewe kwa kazi ya kumleta huyo dada nakupa kiasi kitakachokusaidia kwa matumizi”
Alitoa waleti yake mfukoni anampa kama laki moja na nusu, mpelelezi anapokea huku anashukuru sana wanaagana, mpelelezi anaondoka anamuacha ofisini kwake mkuu wake.
“Ukitaka kumuua kobe lazima utumie akili”
Ilikuwa kauli ya mkuu akimfananaisha mpelelezi kama kobe. Mpelelezi alimpigia simu mkuu wake anamueleza hali halisi ya kukubaliwa juu ya ombi lake. Mkuu wake wa upelelezi alifurahi sana, aliahidi kumpa taarifa Muona ambaye ni askari mpelelezi mwenzake.
Siku hiyo hiyo jioni mpelelezi alimbatana na Muona hadi makao makuu ya kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani. Walikutana na Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani. Scorpion alipomuona Muona.
“Uzuri huu mbona afanani na kuwa askari”
Neno hilo lilikuwa likimwelekea Muona ambae ni askari mpelelezi, aliyeumbwa na Mola akaumbika haswa. Mwenye rangi ya asili. Kila kiungo chake kilikaa mahala pake na kumpendezesha, umtoe kasoro gani mrembo huyo jamani! Ukizungumzia hipsi, hakika zilikuwa kubwa za kututumua nguo aliyovaa. Chuchu zake hazikuhitaji msaada wa sidiria, hii ni kutokana na lishe na ubora wake ambao labda tangu utotoni mwake zilisema zitaendelea kusimama hadi uzeeni. Hakika zilikuwa za saa sita, nyonga yake iligawanyika katika sifuri mbili, juu na chini kiasi cha kuleta umbo namba nane. Miguu yake minene ya wastani ilimfanya atembea kwa umbo la kike haswa. Kila akipiga hatua chini ungedhani anaionea huruma ardhi ya Mwenyezi Mungu.
Hata umpe nguo ya aina gani, kwake ingempendeza na kumvutia kila mtu aliyemtia machoni. Jina lake liliongezea sifa za umbo lake. Muona Mwamsumbwe lilimstahili. Kifupi ni kwamba, alikuwa chakula cha macho ya wanaume wengi, lakini wanaume wengi waliogopa kujaribu bahati yao kumtongoza kutokana na kuhofia kazi yake ya askari mpelelezi, walibaki kuambulia kula kwa macho tu.
Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani kutokana na uzuri wa Muona akuwa na imani kabisa kuwa ni askari mpelelezi kwa jinsi alivyokuwa mrembo. Mpelelezi alimtambulisha Muona kwa Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani. Muona aliposalimiana na Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani, sauti yake ilipenya masikioni kwa Scorpion na kuzibua masikio yake jinsi sauti ilivyokuwa nzuri.
Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani alichanganyikiwa na Muona kutokana na uzuri wake, sauti yake ilimsukuma kumpitisha Muona kufanye kazi katika kitengo hicho cha wizi wa pikipiki mitaani bila kipingamizi.
Ni nguvu ya upendo ndio iliotawara kwa Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani juu ya Muona. Alitekwa kihisia na Muona kutokana na uzuri na umbo lake lililoumbwa likaumbika ukichangia na sauti ndio kabisa alidata aswaa. Moja kwa moja alitokea kumpenda akasahau kama Muona ni askari mpelelezi. Nguvu ya upendo ilimtawara alisahau yote juu ya mpelelezi na Muona, ama hakika mapenzi yana nguvu kuliko breki dauni.
Kazi ya kwanza kwa Muona aliambatana na mpelelezi, na yule rafiki yake mpelelezi ambae alikuwa dereva bodaboda mwenzake Tabata Segerea. Waliaelekea maeneo ya kigamboni mji mpya kwenda kuiba pikipiki. Walipofika Kigamboni wanamtuma Muona akakodi pikipiki na kumuelekeza kwa kuja. Muona alienda kukodi pikipiki mpaka eneo aliloelekezwa atamkuta mpelelezi na yule rafiki yake dereva bodaboda wa Segerea. Alipofika eneo ilo na huyo dereva bodaboda walimtia nguvuni. Mpelelezi aliwai alimpiga huyo dereva bodaboda sehemu ya fahamu kama kawaida yake anamzimisha. Huyo mwizi alitaka kumuongezea kumpiga panga lakichwa lakini mpelelezi na Muona walimzuia.
"Mkimuaucha hai ni hatari!"
Mpelelezi na Muona awakuweza kumuelewa, msimamo wao ulikuwa ule ule wa kumzuia kuua, mwizi akuwa na nguvu kwa sababu alikuwa peke yake lakini Mpelelezi yupo na Muona nguvu ilikuwa kubwa kwa upande wao. Huyo mwizi alichukia sana lakini akuwa na jinsi anakubali matokeo wanamuacha huyo dereva bodaboda akiwa amezimia wanaondoka na pikipiki yake wanapita njia ya daraja la Kigamboni wanatokea uhasibu wanaondoka bila kuonekana hadi wanafika makao makuu ya kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani.
Walipofika makao makuu, huyo mwizi anatoa taarifa kwa msaidizi wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani kuwa mpelelezi na Muona wamezuia kumuua dereva bodaboda waliomuibia pikipiki, matokeo yake wamemzimisha. Msaidizi aliposikia anachukia sana kwa sababu ni hatari endapo kama huyo dereva bodaboda amewatambua kwa sura ni rahisi kukamatwa. Msaidizi alianza kuwafokea mpelelezi na Muona, hadi Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani anasikia anatoka ofisini anafika hadi hapo, lakini mpelelezi anajitetea kutokana na hilo.
“Sikiliza kwani pikipiki tulioiba mali ya nani na mnunuzi dukani nani?”
“Huyo mliomuibia”
“Sasa kama mali ya tuliomuibia na yeye ndio mnunuzi kama kila tunaemuibia tunaua wakiisha nani atanunua pikpiki ili tuibe kampuni ipate pesa?”
Lilikuwa swali gumu ambalo kiongozi msaidizi alishindwa kujibu.
“Vile vile kama tunawaibia na kuwaua je wataogopa wengine kununua pikipiki wakiofia kuuliwa”
Mpelelezi alizidi kumuongezea sindano za maswali kiongozi msaidizi inapelekea kuwa mpole na kumsikiliza mpelelezi.
“Tuwaibie lakini tusiwaue ili waendelee kununua tuibe tuzidi kuingiza pesa katika kampuni yetu”
Msaidizi akuwa na la kujibu, Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani aliwaruhusu kuondoka. Mpelelezi, Muona na huyo mwizi waliondoka walienda kuungana na wenzao ambao wamerudi baada ya kufanikiwa kuiba pikipiki. Maongezi yalikuwa ya kupeana ongera kwa kukamilisha kazi na kufanikiwa kuiba pikipiki. Lakini yule mwizi bado alikuwa na kinyongo na kile walichokifanya mpelelezi na Muona kutomuua waliomuibia pikipiki, alikuwa na hofu na usalama wake. Alijitenga alikaa peke yake, wenzake waligundua hali hiyo, walimuuliza kinachomsumbua lakini akutaka kuongea na mtu.
Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani aliyatafakari maneno ya mpelelezi, anagundua yana tija ya kuyafanyia kazi. Baadaye baada ya wafanyakazi wote kuruhusiwa kuondoka, alimpigia simu mpelelezi anaomba wakutane. Mpelelezi aliitikia wito anakutana na mkuu wake wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani.
"Nimeitikia wito mkuu"
"Nashukuru! lakini awali ya yote natanguliza samahani kwa kufokewa na kiongozi wako wa kazi"
"Kawaida kiongozi, mambo kama hayo yapo katika majukumu ya kikazi"
"Nashukuru kama una fahamu ilo, lakini pia nakuunga mkono kwa lile wazo lako la kutowaua mnaowaibia pikipiki"
"Nashukuru"
"Nakuahidi nitaitisha kikao na kuwaambia vijana wote ili wasiwaue wanaowaibia kama kuuliwa inapobidi labda mtu mbishi na msumbufu ila kama mshamzibiti azimishwe na kuachwa"
"Itakuwa vizuri mkuu"
"Usijari ilo limepita"
"Sawa kiongozi"
“Tumemaliza la kazi ila kuna lingine nataka unisaidie”
“Nini tena mkuu nikusaidie?”
“Napenda kujua juu ya Muona ni mpenzi wako?”
“Hapana! Mimi na Muona ni marafiki tu na ukaribu wetu wa kazi”
“Unasema kweli?”
“Ndio”
“Vipi kuhusu mwanaume wake?”
“Sijawai kumuona hata siku moja na mwanaume na ajawai kunitambulisha mwanaume fulani shemeji yako”
"Kweli?"
"Yah!"
"Sijui lakini maana yule mwanamke mrembo awezi kukosa mwanaume hata siku moja"
"Anaweza kuwa nae ni siri yake lakini kwa upande wangu sijawai kumuona"
“Ok! Sasa naomba unisaidie”
“Nikusaidie nini?"?
“Namuhitaji niwe nae kupitia wewe itakuwa rahisi”
“Sawa! Sio mbaya ila unajua mimi na Muona tunaheshimiana sana, sasa kumwambia kitu kama hicho nakuwa na aibu ila kwa ushauri nenda atakuelewa unajua watu wanaogopa wanawake wazuri lakini wanawake wazuri ni waelewa sana”
Mkuu alitabasamu anakohoa kidogo kulainisha koo.
“Una hakika na ilo?”
“Asilimia mia moja”
Walikubaliana, wanamaliza kikao chao cha muda mfupi, wanaagana kila mmoja anaondoka. Mkuu imani ya kuwa Muona na mpelelezi ni askari ilitoweka akilini kwake kadri ya siku zinavyozidi hii inatokana ushauri wa mpelelezi katika majukumu ya kazi na nguvu ya upendo inayomsukuma kwa Muona. Siku zilizidi kwenda bila Scorpion kumwambia chochote Muona alibaki kuumia moyoni lakini siku zote majanga yakizidi kimo moyo uota kutu. Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki aliomba kuongea na Muona.
Muona akuwa na kipingamizi kwakuwa mpelelezi alishamwambia kuwa mkuu wake anamtaka kimapenzi aliitikia wito, alikutana na Scorpion, Scorpion alimueleza juu ya hitajio lake la kimapenzi kwake. Muona bila kipingamizi alikubali ili kupata nafasi nzuri ya kumpeleleza Scorpion.
Katikati ya mwezi huo, bila kutegemea Muona na Scorpion mkuu wa kiteno cha wizi pikipiki mitaani walijikuta katika mapenzi mazito! Halikuwa tegemeo la Muona kufanya hivyo, bali alijikuta ndani ya himaya ya Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani bila kutegemea na kujisikia kama mtu aliyeisaliti nafsi yake. Siku ya kwanza wapenzi hawa kutoka pamoja, ilikuwa ni siku ya wapendanao{Valentine day} Usiku wa siku hiyo walikwenda sehemu mbali mbali za starehe na mwisho wa siku walikwenda kulala katika hotel mashuhuri hapa mjini HYAUPEGENCY DAR ES SALAAM THE Kilimanjaro ilipo posta.
Ilikuwa mara yake ya kwanza Muona katika maisha yake kwenda hoteli hiyo, alifurahi sana. Zawadi pekee Muona aliompatia Scorpion ni penzi la dhati na hata alipokuwa anafanya kitendo hicho, karibu mwili wake wote aliusikia kama umepigwa shoti ya umeme, ulikuwa ni msisimko wa ajabu!
"Hii ni mara yangu ya kwanza! kupewa penzi kama ili"
"Hakika"
"Yeah! sijawahi kufikishwa kileleni na mwanaume!"
"Lazima unanitania?"
"Sitanii!"
"Kwa hiyo wote uliokutana nao walikuwa wanamaliza shida zao bila ya kukurizisha?"
"150%"{Asilimia mia moja na hamsini}
"Kwanini?"
"Sijajua lakini kwanini wewe umeweza?"
"Kila kijiti na utamu wake"
"Hakika! nakuruhusu endelea tena na tena ili nisikie raha zaidi"
Scorpion bila aibu akitaka kuujua ukweli, alianza kumchezea Muona sehemu zote za msisimko. Alijua alichokuwa anakifanya hivyo alisababisha kuamsha hisia za Muona na kurudi kwa mara ya pili mchezoni. Alirudia tena na tena na kujikuta wote wapo hoi kila mmoja kajitupa upande wake kitandani. Baada ya mchezo wa dakika tisini, aligundua yaliosemwa na Muona yalikuwa na ukweli mtupu lakini kwa kushiriki na wanaume kama wawili au watatu Muona, jambo hilo lilikuwa miujiza!
"Umewezaje kuwavumilia wanaume wote wasiokurizisha?"
"Sikuwa na hisia nao nilikuwa nafanya kwa sababu tu!"
"Sababu ipi?"
"Kuna kitu nilikuwa nahitaji kutoka kwao"
"Kama?"
"Pesa"
"Muona will you marry me?"{Muona utakubali nikuoe?}
"I will marry you!"{Nitaolewa nawe}
"Sure?"{Hakika?}
"Yes, because I love you, I have never felt like this in my entire life"{Ndiyo kwa sababu nakupenda na sijawahi kujisikia hivi katika maisha yangu yote}
"Kama ni hivyo nitakupenda na kukukujari siku zote za maisha yangu"
"Thank you! I love you."{Ahsante, nakupenda}
Alisema Muona akiwa amemkumbatia Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani, walipoangaliana waligundua kuwa wote wenye hisia na mwenzake. Hivyo ndivyo walivyoanza na penzi lao lilikomaa siku hadi siku, wakiwa wameahidiana kufunga ndoa. Muona alivaa pete ya uchumba ya Scorpion kidoleni mwake. Ilikuwa furaha mno katika maisha yao. ili kumuepusha na matatizo ya mitaani katika kuiba pikipiki mitaani Muona, Scorpion aliamua kumzuia kwenda mitaani kuiba pikipiki na kumpa kiteno cha kuwapangia wezi wote kwenda kuiba pikipiki mitaani.
“Kweli mapenzi yana nguvu kuliko breki dauni”
**********
Taarifa ya Muona kusimamishwa kwenda mitaani kuiba pikipiki zilimfikia mpelelezi, mpelelezi alienda moja kwa moja kwa kiongozi msaidizi wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani ambaye ndiyo anawapangia wezi wote kwenda mitaani kuiba pikipiki.
“Mkuu nilishakwambia kuwa ninapokuwa katika kazi na Muona nafanya kazi kwa ufanisi mkubwa, sasa imekuaje Muona amezuiliwa kwenda mitaani?”
“Najua ilo lakini sio mimi niliotoa agizo ilo ni mkuu mwenyewe kwa hiyo mimi ni mtekerezaji, sina uwezo wa kumrudisha”
Mpelelezi akuogopa alienda moja kwa moja hadi ofisini kwa Scorpion mkuu kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani.
“Samahani mkuu ila nimekuja kuna jambo linanitatiza?”
“Jambo gani tena au pesa?”
“Hapana! Sina tatizo la pesa ni kuhusu Muona”
“Muona kafanyaje tena!”
Alishangaa anajua Muona labda kapata tatizo maana bado ajafika kazini.
“Kuna tatizo limemkuta?”
“Hakuna tatizo lililomkuta ni kuhusu hapa ofisini wakati naomba Muona ajiunge nilisema ninapokuwa karibu na Muona katika kazi, kazi zinakamilika katika umakini na tunafanikiwa sana sasa nasikia Muona kabadirishwa kitengo atakuwa anabaki ofisini, kwanini inakua hivi?”
“Sitaki aende mitaani katika matukio”
"Kwanini?"
"Nimeamua tu!"
“Sawa! Kiongozi ila tambua ufanisi wa kazi nakosa, sasa kama ni hivyo bora niache kazi tu endapo kama sitakuwa na Muona katika kazi”
Mkuu aliposikia maamuzi hayo kwa mpelelezi alihisi mpelelezi akiacha kazi na Muona awezi kuendelea na kazi lazima ataacha na yeye ataacha kazi.
“Sio kama nimefanya hivyo kwa kukualibia wewe utendaji wako wa kazi bali nimeanza na Muona na wewe nafasi yako ipo kama niliompa Muona kwa hiyo usiache kazi, mtakuwa karibu kama kawaida na Muona”
Mpelelezi alielewa lakini akuipokea kwa furaha hiyo taarifa kwa sababu lengo la yeye kuongeza nguvu ya Muona ni kuzuia wezi wanapoenda kuiba pikipiki mitaani kutowaua madereva bodaboda wanaowaibia pikipiki sasa kama watakuwa wanabaki ofisini watakosa nafasi ya kuwazuia. Akutaka kumuonesha Scorpion kuwa akupenda hayo mabadiliko ya kazi ya Muona aliaga na kuondoka.
Mipango ilifanyika na Muona na mpelelezi wote wawili wakapewa kitengo cha kuwapangia kazi wezi wote kwa kwenda kuiba pikipiki. Ilikuwa ni mabadiliko ya ghafla na kila mwanachama wa kitengo hicho cha wizi wa pikipiki mitaani akutarajia uteuzi huo kati ya Muona na mpelelezi. Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa wageni kupewa vitengo vikubwa katika kitengo hicho cha wizi wa pikipiki mitaani.
Siku ya kwanza ya kuanza kazi ya kuwapangia wezi wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani kwenda kuiba pikipiki ndipo Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani akawaambia wezi wote kuwa wanapoenda katika kazi wasiwaue wanaowaibia pikipiki ili waendelee kununua pikipiki, waibe tena kampuni ikue. Wezi wote walielewa lakini rafiki yake mpelelezi ambaye alikuwa dereva bodaboda mwenzake Segerea aliemleta mpelelezi katika kitengo hicho, alichukia sana huku akiamini ushauri huo wa mpelelezi lakini akuwa na jinsi lazima akubali, bosi ameshasema. Walizingatia walichoambiwa na mpelelezi aliwafundisha jinsi ya kuwapiga ili kuwazimisha bila kuwajeruhi na siraha yeyote.
**********
Baada ya miezi miwili kupita, Scorpion anapigiwa simu na mtu ambae anamwita mheshimiwa.
"Amefikia wapi mpaka sasa?"
"Mheshimiwa si ulisema mpaka tuwajue wote wanaokijua hichi kitengo ili tupate kuwamaliza wote"
"ndio!"
"Ndio! maana mimi nilikuwa kimya bila kukupa taarifa zozote"
"OK! kwa sasa aina maana tena kuwajua wote, hao walioingia wachukuliwe hatua haraka iwezekanavyo ili kupoteza ushahidi wote"
"Sawa! nitalifanyia kazi"
Walikubaliana hivyo! Mheshimiwa anakata simu. Mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani anabaki njia panda asijue nini cha kufanya. Mpelelezi na Muona awakuyajua waliopangiwa wao waliendelea na kazi ya kuwapangia wezi sehemu za kwenda kuiba pikipiki. Wakiwa hapo ofisini walipata nafasi kubwa sana ya kupitia mafaili mbalimbali na kufanikiwa kuona faili lenye majina ya wezi wote, picha za sura zao pamoja na namba zao za simu.
Awakuishia hapo walichunguza sehemu tofauti tofauti wanagundua stoo zinazoifadhiwa mabaki ya pikipiki zinazochenguliwa yasiokuwa na kazi na preti namba za pikipiki zinazoibwa mitaani. Baada ya kugundua hayo, walitumia simu ya Muona kupiga picha hizo picha za wezi wote, kupiga picha majina na namba zao za simu, walipiga picha hayo mabaki ya pikipiki stoo na rundo la preti namba na kuzituma kwa O.S.S mkuu wao kwa njia ya mtandao wa whatsApp. O.S.S mkuu wa upelelezi aliziona vitu vyote alivyotumiwa aliwapongeza kwa kazi nzuri. Alikwenda kuifadhi vitu vyote katika faili maalumu katika komputa hapo kituo cha polisi Tabata Shule. Siku hiyo hiyo baadaye, O.S.S alikutana na kiongozi wake ngazi ya juu ya upelelezi R.C.O alimfikishia taarifa hizo. R.C.O alifurahi sana kwa kazi nzuri wanayoifanya vijana wake.
"Hatua nzuri ya mafanikio ya upelelezi, nakuahidi ukifanikiwa hilo lazima upandishwe cheo"
"Nashukuru mkuu"
"Maana umefanya kazi kubwa wewe na vijana wako kuhakikisha unatokomeza uharifu nchini"
"Ni kweli kabisa kwa sababu wanaohathirika na kitengo hichi ni madereva bodaboda"
"Hakika!"
"Sasa lazima tukusanye nguvu kubwa ili kuwatia nguvuni wezi wote na kuteketeza kitengo chote cha uharifu"
"Vizuri sana!"
Walipanga mambo mengi ya upelelezi ili kuvamia katika hicho kitengo ili kuwatia nguvuni wezi wote.
**********
Masaa matatu baadaye, tayari ilikuwa saa kumi jioni juu ya alama. Sauti ya adhana ilisikika katika misikiti mbali mbali kuingia katika nyumba za ibada ili kufanya ibada. Mpelelezi na Muona wakiwa hapo ofisini katika kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani walisikia simu ya ofisi inaita. Mpelelezi alinyanyuka kutoka mahali alipokaa na kuanza kutembea taratibu kuelekea mahali simu inapoita. Alipofika aliangalia simu iliyoingia ni namba ngeni, hakuwa na wasi wasi anapokea, aliepiga anamwambia mpelelezi apeleke gari ili akabebe pikipiki.
Mpelelezi akupoteza muda alimuaga Muona na anachukua gari aina ya haisi ambayo wanaitumia kubeba mapikipiki baada ya kuiba anaelekea alipoelekezwa maeneo ya Buguruni Skita katika viwanja vya mpira. Dakika thelathini na moja baadaye, mpelelezi anafika eneo la Buguruni Skita alisimamisha gari katika jengo kubwa la golofa. Akiwa ndani ya gari alipepesa macho huku na huko bila kumuona mtu. Alishuka katika gari anapiga hatua kusogea katika hilo jengo mara anawekwa chini ya ulinzi kwa nyuma na watu wasiojulikana kumuamuru aelekea ndani ya hilo gorofa. Mpelelezi alitii kama walivyomuamuru hadi ndani ya hilo gorofa lisiloisha lililo maeneo hayo ya Skita karibu na minazi.
Baada ya kumfikisha ndani ya hilo gorofa walianza kumpiga mpaka anakua hoi hoi. Akiwa katika hali mbaya kutokana na kipigo cha hao watu, alisikia sauti ikitoa amri waamue kabisa. Japo alikuwa katika hali mbaya lakini hiyo sauti alihisi sio ngeni masikioni kwake.Alijitaidi kuangalia inaposikika hiyo sauti kwa shida na tabu ili hakikishe anachokihisi ndipo anamuona mtu akiwa katika vazi la polisi lakini alishindwa kumjua ni nani anajitahidi kuangalia uenda anaweza kumjua lakini wapi! mboni za macho yake azikuweza kutoa taswira ya kuona vizuri kutoka alikuwa katika hali mbaya ya kipigo. Aliona msaada pekee wa kumjua mtu huyo ni kumbukumbu zake, alijitahidi kuvuta kumbukumbu alipowai kusikia sauti hiyo lakini pia alishindwa kutokana na hali aliokuwa nayo. Hao wapigaji baada ya kupewa ruhusa ya kuua waliendelea kumpiga mpelelezi hadi mpelelezi hadi pumzi zinakata.
"Ameshakufa tayari!"
Huyo askari alietoa amri kuuliwa mpelelezi alisogea hadi sehemu walipo hao watu na mpelelezi. Alipofika alimkagua mapigo ya moyo mpelelezi kimya hakuna mdundo wowote wala hakuna pumzi anayosikia kutoka kwa mpelelezi.
"Vizuri! kazi nzuri"
**********
Msaidizi wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani akiwa hapo makao makuu ya kitengo cha wizi wa pikipiki akiendelea ya kubomoa pikipiki na kutoa injini mara simu yake iliita. Aliaacha kazi aliokuwa anaifanya anapokea simu. Mtu aliepiga simu alianza kutoa malalamiko muda mwingi amepiga simu katika simu ya ofisini ili gari ije kubeba pikipiki lakini simu inaita bila kupokelewa.
Msaidizi wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani baada ya kupewa taaria hiyo alienda ilipo simu ya ofisi huku anaongea na huyo mtu lakini alipofika bila kumuona mpelelezi wala Muona. Alikata simu ya huyo mtu anapiga simu ya ofisini ambayo ipo kwa ajiri ya kupokea taarifa za kwenda kubeba pikipiki mitaani zilizoibiwa lakini anapiga mara nyingi bila simu kupokelewa. Alienda moja kwa moja hadi ofisini kwa mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani anamkuta akiwa na Muona.
"Mkuu napiga simu ya ofisi lakini bila kupokelewa sasa sijajua dereva yupo wapi maana vijana wanataka gari kubeba pikipiki"
"Kwani Job ametoka muda gani?"
Mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki alimuuliza Muona.
"Kama lisaa limoja na nusu baada ya kupigiwa simu akabebe pikipiki"
"Ajafika eneo la tukio lolote maana vijana wote wanapiga simu na kutuma meseji wanapiga simu ya ofisi ambayo anayo dereva wa gari lakini aipokelewi"
Mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani na Muona wote walishangaa, Muona haraka haraka anapiga simu ya mpelelezi lakini inaita bila kupokelewa.
"Atakua wapi sasa"
"Kama apokei simu jaribu kutuma meseji yawezekana yupo sehemu mbaya ila hakikisha unatuma meseji ya kawaida"
"Vijana baada ya kupiga simu aipokelewi walituma meseji lakini hakuna meseji hata moja iliojibiwa"
Mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani alifikiria kama dakika mbili huku anachezea simu kama mtu anaepiga mahesabu.
"Fanya hivi wajulishe vijana wote kila mmoja afanye anavyoweza afike ofisini na hizo pikipiki na hakikisha unawaambia wasitume meseji wala kupiga simu tena katika simu ya ofisini aliokuwanayo Job"
"Sawa! mkuu"
Msaidizi wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani alitoka humo ofisini kwa mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani aliondoka. Muona muda wote akuwa na amani wala furaha kutokana na mpelelezi, alifikiria nini kimemkuta mpaka apokei simu wala ajibu meseji. Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki aligundua hali hiyo kwa Muona.
"Muona"
Lakini Muona kimya akiwa katika mawazo mazito.
"Muona"
Mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani alimwita huku akimshtua mkononi ndipo Muona anashtuka kama mtu alietoka usingizini na kuitikia.
"Vipi mbona mawazo mengi?"
"Job"
"Natumaini atakua sehemu salama,yawezekana apokei simu yupo sehemu mbaya si unajua kazi yenyewe hii"
"Bora hata ajibu meseji nipate tumaini"
"Usijari kila kitu kitakua sawa"
Mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani alichukua simu yake anapiga katika simu ya ofisini aliokuwa nayo mpelelezi lakini simu ikawa aipatikani kabisa.
"Simu aipatikani kabisa"
"Mungu wangu"
Muona alitaka kulia lakini Mkuu wakitengo cha wizi wa pikipiki anamtuliza.
"Sijui kimemkuta nini Job wangu"
Alichukua simu yake anapiga simu ya mpelelezi anapiga lakini nayo simu aipatikani kabisa, Muona alichanganyikiwa anainuka na kutoka ndani ya ofisi ya mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani. Mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani alimfuata nyuma anamuwai mlango wa kutoka nje.
"Muona unakwenda wapi?"
"Job nahitaji kujua alipo na nini kimemkuta"
"Wapi sasa?"
"I don't know"{Sijui}
Anapiga hatua anaondoka.
"Ni hatari kwako"
Muona wala akujari alipiga hatua anaondoka na kutoka ndani ya jengo hilo la kitengo cha wizi wapikipiki mitaani. Jengo ilo kwa nje ukiliona unajua ni gereji lakini kumbe ndani inafanyika biashara chafu ya wizi.Mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki akutaka kumfuata tena Muona kuepusha kuvutana vutana mbele za watu. Muona akiwa njiani aliondoka kwa miguu ghafla inakuja gari na kupaki mbele yake, Muona alishangaa, dereva wa gari hiyo mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki alishuka katika gari anasogea alipo Muona.
"Tuungane kwa pamoja kumtafuta Job"
Muona akiwa amemkodolea macho mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani.
"Ingia ndani ya gari twende"
"Wapi?"
Mkuu alifikiria kwa muda mara anatoa simu mfukoni anapiga.
"Mpendwa Lisa"
"Ndio bosi"
"Bila shaka upo ofisini?"
"Ndio"
"Ok! naomba unisaidie kitu kimoja, kuna namba nakutumia uingalie simu ya mwisho kupokea ilikua ya nani na akiwa wapi?"
"Sawa! bosi naomba nitumie ili nikuangalizie"
Mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani alituma hiyo namba ya ofisini. Muona aligundua mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani alikuwa anaongea na mtu wa makao makuu ya mtandao wa simu lakini akujua ni mtandao upi?.
"Ulikuwa unaongea na muhudumu wa mtandao wa simu?'
"Ndio!"
"Mtandao gani?"
Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani alimtajia Muona huo mtandao wa simu. Muona alizuga kidogo halafu anaandika katika simu muda huo Scorpion anaoongea na huyo mtu wa mtandao wa simu.
"Nimeshatuma makao makuu ya Tigo namba aliokuwa nayo Job, baada ya muda mfupi watatuambia simu ya mwisho kuongea nayo ya nani na huyo mtu akiwa wapi, tutakapota maelezo hayo tutajua kwa kumtafuta"
Muona alishusha pumzi huku anamwangalia usoni mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani.
"Naomba uingie ndani ya gari"
Scorpion alimwambia Muona huku anamshika mkono anampeleka, Muona bila kipingamizi anaongoza, Scorpion alimfikisha hadi mlangoni anamfungulia mlango anamuingiza na yeye anazunguruka upande wa pili wa gari. Muona akiwa ndani ya gari amekaa unaingia ujumbe mfupi wa maneno katika simu yake. Alifungua na kuanza kusoma huo ujumbe lakini anashtuka baada kusoma ujumbe huo mfupi wa maneno katika simu yake. NI taarifa mbaya ya kutoka kwa O.S.S mkuu wake wa upelelezi inayomuhusu mpelelezi.
Mpaka dakika hiyo anapata ujumbe huo mfupi wa maneno, mpelelezi yupo hospitali ya Amana wodi ya maututi ICU. Akujua nini afanye kwa muda huo kwa sababu yupo na mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani. Muona alitafakari ataondoka vipi na kumuacha mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki ili aende hospitali ya Amana. Mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani anaingia ndani ya gari kabla ajawasha gari ili waondoke simu yake inaita anapokea.
"Samahani kwa kusubiri"
"Usijari"
"Sasa nimeangalia hapa kuna meseji zilizotumwa na hii namba yako ya kutoa taarifa ya kuwaita watu waje ofisini, halafu masaa kumi tisa mbele simu ya kwanza alipigiwa ya kuitwa Buguruni Skita ya kwenda kubeba pikipiki, nyingine alitumiwa meseji akiitwa sehemu tofauti tofauti akabebe mzigo na alipigiwa simu nyingi sana, nyingine zikirudia kupiga lakini akuweza kupokea"
"Vizuri! kwa hiyo kuna simu ya kwanza iliopigwa aliitwa Buguruni Skita kwenda kubeba pikipiki"
"Ndio bosi"
"Hiyo simu kutoka eneo gani na namba gani?"
"Namba 0764 07 07 97, eneo alilokuwa huyo mtu aliokuwa anapiga simu ni hapo hapo Buguruni Skita"
"Nashukuru! kazi njema, kama kuna kitu kitakwama nitakutafuta ili unipatie ufumbuzi ila nitumie hiyo namba"
"Usijari bosi"
Simu inakatwa, Lisa mfanyakazi wa mtandao wa simu, muda huo huo anatuma hiyo namba. Mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani anachukua hiyo namba anaipiga katika simu yake anagundua ni namba ya mtu ambae aliempa taarifa ya kuingia mpelelezi katika kitengo chake cha wizi wa pikipiki mitaani na anaempa taarifa zote kutoka serikalini. Mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki alipogundua hilo imani yake ilisaidiki kuwa kuna kitu amekifanya huyo mheshimiwa kwa mpelelezi. Alitaka kupiga simu ili aongee nae lakini anashindwa kwa sababu yupo karibu na Muona, alibaki njia panda asijue nini cha kufanya. Muona aligundua mabadiliko hayo kwa mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani lakini akujua kwanini amekuwa hivyo ghafla, akataka kujua ukweli uliofichika.
"Umeambiwaje?"
Mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani alikuwa kimya kama dakika mbili baada ya kuulizwa ndipo anaongea.
"Mtu wa mwisho kuongea nae sehemu alipokuwa hadi anapiga simu ni tofauti na sehemu alipoenda Job baada kupigiwa simu"
"Kwa sehemu zote si wamekutajia?"
"Ndio!"
"Wapi na wapi?"
"Aliepiga simu alikuwa Buguruni na alipoenda Job baada ya kupigiwa simu ni Makuburi"
"Kwa hiyo tunaanzia wapi"
"Hata tukienda tutasumbuka bila kujua eneo alipo kwa hiyo lazima tutumie Gprs ili kujua sehemu alipo"
Muona aliposikia kuhusu kutumia Gprs ili kujua sehemu alipo mpelelezi alipata wasi wasi kuwa mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani anaweza kugundua mpelelezi yupo hospitali ya Amana hivyo anaweza kugundua mpelelezi ni askari. Alitafakari cha kufanya ili mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani asitumie Gprs kumtafuta mpelelezi sehemu alipo maana simu yake na simu ya ofisi anazo mpelelezi.
"Ila hii kazi nitaifanya nikiwa mwenyewe maana ina mzunguko mrefu"
Mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani kama alikuwa katika mawazo ya Muona, Muona baada ya kuambiwa hivyo kimoyo moyo alifurahi sana ili aondoke aende hospitali Amana ili akazichukue simu zote na kuzitoa hapo hospitali ili asigundulike mpelelezi kama yupo hospitali ya Amana.
"Sawa! aina shida naomba unipeleke na gari hadi Tazara"
"Sio uende ofisini ili nikirudi nikuambie kilichojiri"
"Hapana! sipo sawa nahitaji nikapumzike hivyo utanipigia simu baada ya kufanikiwa"
"Ok!"
Mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani aliwasha gari wanaondoka. Mwendo wa dakika kumi wanafika Tazara kutokana na foleni ya kutoka vetinary hadi tazara. Baada ya kufika Tazara mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani alimpa Muona elfu hamsini, Muona alipokea huku akishukuru. Baada ya kuagana Muona alishuka katika gari na mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki aliondoka na kuelekea mjini njia ya moja kwa moja kuelekea Posta. Muona alisimama hapo Tazara hadi akahakikisha gari ya mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani inapotea machoni mwake. Baada ya kuhakikisha imepotea machoni kwake gari ya mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani, alisimama hapo kama dakika kumi.
Dakika kumi na moja, alipanda pikipiki hadi vingunguti, alipofika vingunguti alishuka anamlipa huyo dereva pikipiki anaachana nae. Alisimama hapo hadi huyo dereva pikipiki anaondoka. Alipohakikisha kashafika mbali anachukua pikipiki nyingine hadi vingunguti kwa perapera anashuka anapanda daradara inayoelekea Mnazi Mmoja.
Mwendo wa nusu saa, anafika hospitali ya Amana, anashuka katika daradara anaelekea ndani ya hospitali ya Amana. Anakutana na O.S.S mkuu wake wa upelelezi, lakini kabla ya yote hata kupewa taarifa juu ya mpelelezi, Muona alimwambia mkuu wake wa upelelezi O.S.S ampeleke wodi aliolazwa mpelelezi. O.S.S mkuu wa upelelezi alimpeleka Muona hadi wodi aliolazwa mpelelezi. Walipofika, Muona alimfunua shuka la wagonjwa alilofunikwa mpelelezi lakini alichokiona alikata tamaa ndipo anamuuliza mkuu wake.
"Nguo za Job zipo wapi?"
"Nahisi zimeifadhiwa na madokta baada ya kumbadilisha nguo kutoka,nguo zake zilitapakaa damu"
"Madokta wao si ndiyo waliombadilisha nguo?"
"Ndio!"
"Awakuwapatia simu mbili?"
"Hapana! hata na sisi ndiyo tulioenda kubeba mwili wake eneo la tukio lakini atukumkuta na kitu chochote mfukoni"
Muona anafikiria kwa muda.
"Kuna nini?"
O.S.S mkuu wake wa upelelezi aliuliza.
"Simu moja ya kile kitengo cha wizi wa pikipiki na nyingine ya Job sasa nahofia wanaweza kuitafuta kwa Gprs wakagundua sehemu alipo Job"
"Kweli! lakini kwakuwa hana simu aiwezi ikawa hivyo"
Muona anaelewa ndipo anauliza kuhusu mpelelezi imekuwaje hadi yupo katika hali hiyo, ndipo O.S.S mkuu wake wa upelelezi anamwambia mpelelezi amepigwa na watu wasiojulikana hadi kufika hapo hospitalini ni msaada wa msamalia mweme aliekwenda katika jengo la gorofa hapo buguruni Skita kwa ajiri ya kufanya mazoezi katika ilo jengo.
Muona anakumbuka maelezo ya Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani anagundua amemdanganya, alipomwambia aliepiga simu alikuwa Buguruni na alipoenda mpelelezi baada ya kupigiwa simu ni Makuburi. Moja kwa moja alihisi kitu kutoka kwa Scorpion ndipo alipomuuliza O.S.S.
"Matatizo hayo yamemkuta akiwa peke yake au na watu wengine"
"Akiwa peke yake'
Ndipo hapo anagundua kuwa mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki atakua anajua waliohusika na kumpiga mpelelezi kwa sababu simu aliopigiwa mpelelezi hadi kwenda huko Buguruni Skita ni simu ya ofisini. Aliempigia hadi kumwita huko anaijua hiyo simu ya hapo ofisini katika kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani kwa hiyo ni muhusika wa hapo hapo katika kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani.
Kama angekua sio muhusika au aijui hiyo namba ya hapo katika kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani angepiga katika namba ya mpelelezi lakini mpaka amepiga katika namba ya kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani, aliehusika na kumpiga mpelelezi mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani anamjua na anatoka hapo hapo katika kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani.
"Mkuu tayari mambo yameshaharibika, sijui nifanye nini?"
"Kwa nini Muona?"
"Watu waliompiga Job ni kwa lengo la kumuua kwa hiyo hata mimi nitakua hatarini kwa sababu katika kile kitengo cha wizi wa pikipiki wameshagundua kama mimi na Job ni wapelelezi"
"Kwa hiyo unataka tufanye nini?"
"Ni kuwatia nguvuni kabla awajachukua maamuzi juu yangu"
"Ok! mimi nakusikiliza wewe tu"
Walikubaliana kuvamia katika kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani na kuwatia nguvuni wezi wote na kuwafikisha katika mikono ya sheria ili kuwafungulia mashtaka. Baada ya kukubaliana hayo kwa usalama kwa upande wa mpelelezi wanamuhamisha mpelelezi kimya kimya hospitari hiyo ya Amana wanampeleleka hospitali ya Lugalo. Ilikuwa ni siri ya Muona na mkuu wake wa upelelezi O.S.S.
Hospitali hiyo ya Lugalo mpelelezi aliendelea kupatiwa matibabu. Muda wote alikuwa chini ya uangalizi wa madaktari kwa kupatiwa matibabu ili kuhakikisha wanaokoa maisha yake. Baada ya Muoana kuhakikisha mpelelezi yupo sehemu salama na anaendelea na matibabu, siku hiyo hiyo baadaye, alienda katika kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani hadi ofisini kwa mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani kwa lengo la kuweka mambo sawa ili kuwatia nguvuni wezi wote.
Lakini alipofika karibu na mlango wa kuingia ofisini kwa mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani anamsikia Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani anaongea na simu, maongezi yake ya kuomba msamaha. Muona akuweza kuelewa msamaha anaouomba wa nini, haraka haraka aliandika katika simu yake siku, tarehe, mwezi, mwaka na muda huo mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki anaongea na simu. Baada ya kumaliza kuandika alifungua mlango anaingia ofisini kwa mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki bila kupiga hodi.
na anamsikia anauliza kwa mshangao.
"Akufa?"
Ndilo swali alilolisikia Muona anatamka mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani, mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani alishtuka baada ya kumuona Muona anaongea kwa wasi wasi huku akichanganya la nyuma mbele la mbele nyuma.
"Ajari akitibiwa mbaya atapona"
Muona anakaa katika kiti. Mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki anakata simu anaiweka simu yake katika ndroo.
"Karibu Muona"
"Ahsante!"
"Ulifanikiwa Gprs?"
"Yeah! Gprs inasoma eneo la Lugalo"
"Lugalo?"
Lisa aliuliza kwa mshangao.
"Ndio! inaposoma system ya simu"
"System! system ya simu kwa maana Gprs inaonesha simu aliokua nayo Job ipo Lugalo au Job yupo Lugalo"
"Kama system ya simu inasoma katika Gprs simu ipo Lugalo basi hata Job yupo Lugalo"
Muona alishtuka baada ya kuambiwa hivyo, ghafla mapigo ya moyo yalibadilika na kudunda mara mbili yake.
"Ok! sasa umechukua uhamuzi gani baada ya kugundua hayo?"
"Tulifika hadi Lugalo lakini ndani ya hospitali ya Lugalo, tulishindwa kuingia kwa sababu sijajua Job mpaka yupo Lugalo hospitali kwa nini na kipi kimemfanya yupo ndani ya hospitali maana ni mazingira ya kutatanisha"
"Ni kweli ila ngoja nifatirie mimi nitajifanya kama mume wangu, naweza kufahamu ukweli"
"Ni hatari kwako"
"Kwa nini?"
"Sote atujui kipi kimemkuta hadi yupo hospitali ya Lugalo"
"Vijana wote si wamerudi salama jana kutoka katika kazi"
"Ndio"
"Basi hakuna baya yawezekana ni ajari tu"
Mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki akuwa na la kusema alibaki kimya anamwangalia Muona, Muona anaaga anaondoka. Mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki alibaki njia panda juu ya Muona na mpelelezi nini afanye maana tayari amesemwa na huyo mtu anaemuita Mheshimiwa na anaempa taarifa kutoka serikalini kwa kukaa na mpelelezi na Muona bila kuwachukulia hatua wakati wao ni wapelelezi wamejiunga katika hicho kitengo cha wizi wa pikipiki kwa lengo la upelelezi.
**********
Safari ya Muona iliishia makao makuu ya kituo cha polisi anapofanyia kazi anakutana na mkuu wake wa upelelezi O.S.S anamwambia mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani amegundua mpelelezi yupo hospitali ya Lugalo kwa matibabu.
"Nani amewapa taarifa hizo"
"Gprs"
"Gprs?"
"Ndio"
"Kivipi?"
"Kuna simu ya ofisi katika kile kitengo cha wizi wa pikipiki aliondoka nayo Job kabla ajapata tatizo ndio hiyo wanayotumia kujua sehemu alipo"
"Sio kweli kwa sababu kama nilivyokwambia Job tumemkuta hana simu wala kitu chochote nahisi wasamalia waliomsaidia ndio wamechukua vitu hivyo"
"Kweli?'
"Ndio! kwanini nikudanganye"
Muona anafikiria.
"Akili ya ziada inahitajika"
"Kwanini?'
"Job amjamkuta na simu mfukoni wala kitu chochote, lakini Gprs imesoma yupo Lugalo sasa kipi hapa kipo sahihi?"
Kila mmoja anafikiria kwa kina, ndipo Muona anamwambia mkuu wake wa upelelezi.
"Ndio maana nimesema akili inahitajika la sivyo wote tutaangamia kwa ajiri ya hii kesi"
Mkuu wa upelelezi O.S.S alibaki kimya bila kuwa na cha kuongea. Muona aliaga anaondoka, njia nzima alitawariwa na mawazo mengi ndipo anakumbuka walivyomuhamisha mpelelezi kumtoa hospitali ya Amana kumpeleka Lugalo ni siri ya yeye na O.S.S, sasa iweje Gprs isome Lugalo wakati amesema wamemuokota mpelelezi awakumkuta na simu wala chochote. Sasa Gprs imesomaje Lugalo na mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani amejua kama mpelelezi yupo hospitali ya Lugalo. Alishindwa kuelewa ukweli wa mambo hayo ndipo imani yake iLIsadiki kuwa O.S.S mkuu wake wa upelelezi anashirikiana na waarifu.
**********
Siku iliyofuata Muona alikwenda hospitalini Lugalo na kukuta mpelelezi bado hajitambui ingawa mapigo yake ya moyo yalikuwa yakipiga vizuri. Hakuwa na matumaini ya mpelelezi kupona. Muona alilia sana, daktari anaemuhudumia mpelelezi alimbembeleza bila mafanikio yeyote.
"Usilie sana, hii yote ni mipango ya Mungu"
"Sawa daktari, lakini inauma, wenyewe wanatupa kazi tuondoe uhalifu lakini hao hao ndio wanatuzuru ili kuficha uhalifu"
Kwa wiki nzima, Muona aliendelea kuwa katika hali hiyo na madaktari walidai angekuwa hivyo kwa siku nyingi, wakati ubongo wake ukipona taratibu. Walitoa jibu hilo baada ya kumfanyia operesheni na kutoa damu iliyoganda kichwani mwake. Kwa Muona siku zote zilikuwa huzuni tupu, alilia usiku na mchana mpaka machozi yakamkauka. Mwisho wauguzi walimzuia kuingia wodini kwa sababu kila alipomwona mpelelezi kitandani akiwa amefungwa na mashine ya kuhemea alilia zaidi. Kila siku alifikiri ni kwa jinsi gani angeweza kumwamsha mpelelezi kutoka katika usingizi mzito wa mauti, aliolala.
Mawazo hayo yalimsababishia kukumbuka kitu ambacho aliamini kingemuamsha mpelelezi. Badala ya kutumia madawa, alikumbuka kuwa mpelelezi alikuwa akiwa ofisini chumba cha upelelezi kituo cha polisi alikuwa anapenda kuvua vitu na kubaki na soksi. Muona alikuwa anamwambia kuwa avae viatu vyake vinatoa harufu lakini mpelelezi alikuwa anamwambia Muona kuwa viatu vyake avitoi harufu na kumthibitishia kwa kumnusisha lakini Muona alikuwa anamtekenya unyayoni. Mpelelezi akitekenywa hata kama alikuwa anafanya kazi gani, aliacha na kushtuka na haraka alivaa viatu vyake.
"Nikimtekenya tu, naamini ataamka!"
Aliwaza Muona kisha akasogea hadi katika miguu ya mpelelezi akafunua shuka aliofunikwa ambako alianza kushika nyayo zake za miguu na kuanza kumtekenya taratibu mithili kama anamfanyia masaji. Alimtekenya unyayoni hadi katika vidole vyote vya miguu, taratibu msisimko ulianza kumsisimua mpelelezi.
"Haah! Katabasamu!"
Alipiga kelele Muona baada ya kumuona mpelelezi ametabasamu na meno yake kuonekana.Aliruka juu na kushangilia ikabidi aongeze kumtekenya zaidi ili kumzindua mpelelezi kutoka katika usingizi wa kifo. Sauti ya Muona iliwafanya madaktari waliopo ofisini walikuja mbio mbio hadi chumbani na kushuhudia hali ya mpelelezi. Hakuna aliyekuwa tayari kuamini kwamba, kweli mpelelezi alitabasamu, ilikuwa ni kama ndoto! Muona aliruka akishangilia na kujiona mshindi, wazo lake lilikuwa limezaa matunda. Kumtekenya kumemfanya mpelelezi kurejea duniani.
Aliongeza kumtekenya. Aliamni kwamba badala ya kutabasamu angenyanyuka kitandani na kukaa na huu ndio ungekuwa mwisho wa mateso na maumivu yake. Madaktari waliamini bila ya Muona kutoa wazo la kumtekenya, mpelelezi asingetabasamu. Mpelelezi alionyesha tabasamu lake vizuri. Vishimo katika mashavu yake vilionekana na meno yake meupe yaliong'ara na kupangwa vizuri yalionekana.
Ilikuwa furaha kubwa mno kwa Muona ndani ya chumba hicho. Madaktari walimwambia Muona atoke nje, Muona alitii lakini muda wote akimuomba mungu mpelelezi afumbue macho. Madaktari wote walianza kumpa huduma ili kumfanya aweze hata kufumbua macho ili awe katika hatua nyingine nzuri zaidi, pengine angekuwa hata na uwezo wa kuongea maneno machache.
Walijitahidi kwa uwezo wao wote, mpelelezi alianza kuchezesha kidole cha mkono hatimae mpelelezi alitingisha mwili wote ndipo hapo tumaini lingine la kuinuka mpelelezi lilionekana kwa mpelelezi. Siku hiyo hiyo baadaye, jitihada za kuokoa uhai wa mpelelezi ziliwezekana na mpelelezi aliweza kuzinduka kutoka katika usingizi mzito wa kifo. Muona alirukaruka kwa furaha, hadi machozi yalimtoka! Alijisikia yu kama malaika kwa kuweza kumzindua mpelelezi kutoka katika usingizi mzito.Hakuamini kuwa tayari alikuwa amezinduka mpelelezi.
**********
Baada ya siku kadhaa, mpelelezi alipona kabisa na alirudiwa na afya yake kama zamani. Alikukutana na Muona, O.S.S mkuu wa upelelezi kituoni na R.C.O mkuu wa upelelezi ngazi ya juu kila mmoja anampa pole kutokana na kuumwa kwa muda mrefu. Walijadiri juu ya kitengo cha wizi wa pikipiki juu ya kuvamia ili kuwatia nguvuni wezi wote na kusambaratisha hicho kitengo. Walipanga kwa pamoja siku ya kuvamia lakini mpelelezi anaomba iwe siri hata askari watakao tumiwa washtukizwe.
“Kwanini iwe ivyo”
Ni swali lililoulizwa na R.C.O mpelelezi ngazi ya juu.
"Kwa sababu, nikiwa nimetekwa nimeshapigwa nipo hoi hoi nilisikia sauti ya mtu ambae sauti naijua kabisa lakini sikumbuki ni sauti ya nani?”
“Aukuweza kumuona sura?”
“Nilijitaidi kuangalia ili nione sura yake, lakini sikuweza kumuona vizuri kwa sababu nilikuwa hoi hoi halafu alikua mbali na nilipokuwa mimi ila alikuwa amevaa vazi la polisi”
Wote walishtuka, mpelelezi anaendelea kutoa maelezo la tukio lake.
“Ili tukio niliwai kuliota na limenitokea kweli sasa kuna asilimia mia moja kuna askari wanatuzunguruka kwa hiyo tusipokuwa makini yatatokea mengine yatabaki majina”
“Kama ni hivyo wapelelezi wote wanaojua hii kesi waitwe waifanye hii kazi washirikiane na wewe kama miongoni wa hao wapelelezi yupo huyo msaliti ni rahisi kumjua na kumtia nguvuni”
R.C.O mkuu wa upelelezi ngazi ya juu alimwambia mpelelezi lakini O.S.S mku wa upelelezi wa kituo anadakia haraka haraka.
“Aina haja ya kuita wapelelezi wote maana wapo mbali kikazi, hata hivyo kazi ishaisha tunachopanga siku ya leo ni lini kuvamia ili kuwatia nguvuni maana orodha yote ya watuumiwa wa hicho kitengo wanajulikana na wanapokaa na picha zao tunazo”
“Kazi nzuri! wote majina yao mnayo?”
“Ndiyo tunayo”
O.S.S alifungua komputa na kuanza kumuonesha, R.C.O mkuu wa upelelezi ngazi ya juu picha moja baada ya nyingine.
“Kwa hiyo mkuu kazi imeisha kilichobaki kuvamia na kuwakamata mmoja baada ya mwingine ila atujapanga siku ya kuvamia”
“Sawa! ila siku ya kuvamia mnijulishe”
“Hakuna shida”
Wanamaliza kikao chao kila mmoja anaondoka katika majukumu yake ya kikazi lakini Muona na mpelelezi waliondoka kwa pamoja, wakiwa njiani.
"Ukweli wazi japo tumepanga mpango wa kuvamia kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani lakini sina imani na mkuu"
"O.S.S au R.C.O?'
"Mkuu wetu ambae kila kitu tunachopanga na kukifanya tunamwambia yeye"
"Kwa nini auna imani nae?"
"Wakati unaumwa ilikua siri kukutoa hospitali ya Amana kukupeleka hospitali ya Lugalo sasa mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani amefahamu sasa unatakiwa ujiulize je kaambiwa na nani"
Mpelelezi alishtuka baada ya kupewa taarifa hiyo ndipo anamuuliza tena Muona, Muona anarudia maelezo mwanzo hadi mwisho.
"Nani kamwambia?"
"Hata mimi nilijiuliza nani kamwambia kama wewe unavyoniuliza mimi?"
"Unachosema ni kweli au unatengeneza mazingira niamini O.S.S anashirikiana na watu baya"
"Najua uwezi kuamini, hata mimi sikuweza kuamini ila ukweli ndio huo"
"Hakuna! kitu kama hicho Muona, O.S.S awezi kufanya hivyo hata mara moja"
"Utakapomshuhudia kwa macho yako ndiyo utaamini"
"Muona sitaki kuamini sauti ninayoifananisha nikiwa napigwa ni ya O.S.S"
"Funika kombe mwana haramu apite"
Muona aliongoza njia anatembea kusogea kituo cha daradara Tabata Shule, mpelelezi anafuata nyuma,wanafika kituoni wanapanda gari la temeke wanaondoka. Safari yao iliishia katika kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani. Walipofika hapo makao makuu ya kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani kila mwanachama alipomuona mpelelezi anampa pole huku akimwambia ndio majukumu ya kikazi maana raia wana hasira kali. Mpelelezi imani yake ilisadiki kuwa taarifa imefika hapo makao makuu matatizo yaliomkuta na kila mwanachama alijua amepata matatizo kutoka kwa raia wenye hasira kali ndio maana wanampa pole.
Alishukuru pole zote alizopewa na wezi wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani, baada ya muda kumaliza kuongea nao mawili matatu, aliongozana na Muona walielekea moja kwa moja ofisini kwa Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani. Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki alipomuona mpelelezi alifurahi sana na anampa pole kwa matatizo yaliomkuta huku akijifanya ajui chochote na kumuuliza ilikuwaje. Mpelelezi alihadithia ilivyokua mwanzo hadi mwisho lakini anasema akuweza kuwafahamu waliomfanyia yote hayo. Mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki anamwambia mpelelezi kwakuwa amepona amshukuru mungu hayo mengine amuachie mungu.
Masaa mawili baada ya mazungumzo kati ya mpelelezi, Muona na Scorpion mkuu wao wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani wanatoka ofisini kwake wanaenda kuendelea na kazi kama kawaida ya kuwapangia kazi wezi wa pikipiki mitaani. Ujio mpya na wa kishindo wanaweka mazingira ya kuwatia nguvuni wezi wote wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani ili kukiteketeza hicho kitengo chote kwa sababu wameingia katika kitengo hicho ili kumjua muuaji wa dereva pikipiki alieuliwa Segerea kwa kuchinjwa kichwa.Endapo wakimjua huyo itakua rahisi kumjua mtu aliehusika katika tukio la Imamu Shafii na dereva bodaboda Tabata Mawenzi kwa sababu pikipiki iliotumika ni moja.
Siku ya siku ilifika, walianza kumpigia simu mwizi mmoja mmoja wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani na kuupa taarifa ya kikao na kukutana katika bar moja maarufu katika wilaya ya temeke inayoitwa Sugar Rey ili kujadili utendaji wa kazi na mambo mengine ya maendeleo kuhusu kitengo chao cha wizi wa pikipiki mitaani. Kila mwizi alipopata taarifa hiyo aliahidi kufika.
Dakika mia moja na kumi baadaye, kila mwizi wa pikipiki aliyopata taarifa ya kikao alifika katika hiyo bar Sugar Rey wanaanza kikao. Ghafla na bila kutegemea, walishtukia gari la polisi linafika likiwa na askari wengi wanawaweka chini ya ulinzi. Wezi wote walipatwa na mshtuko wa ajabu na kujikuta wakiweka mikono juu kutii sheria bila shuruti. Ilikuwa ni ngumu kukimbia wala kufanya chochote kwa sababu askari walijiandaa na siraha za moto. Walikamatwa wezi wote na mpelelezi walijifanya kama awamtambui na kumjumuisha nao. Waliingizwa katika gari la polisi kubwa aina ya Leland na kupelekwa kituo cha polisi Tabata Shule. Japo ilikua ni Wilaya mbili tofauti, walipelekwa kituo cha Tabata Shule. Walipofikishwa kituoni waliwekwa sero tofauti tofauti na mpelelezi aliachiwa.
Yaliyotokea nusu saa baadaye, alitolewa sero mwizi mmoja mmoja wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani na kufanyiwa mahojiano, mahojiano yaliambatana na kipigo kikali ili kusema wanaoshirikiana nao, matukio mangapi walioyafanya, pikipiki walizoiba na mauaji waliyoyafanya na maeneo waliofanya hayo matukio. Kila mwizi aliehojiwa alisema ukweli wote kutokana na mateso makali, ndipo mmoja anasema alifanya tukio maeneo ya Tabata Segera na mwenye pikipiki akamchinja shingo. O.S.S baada ya kusikia tukio ilo na analijua ambalo ni tukio lililotokea Tabata Mawenzi wanamshikiria huyo jamaa na wanajua ndie aliehusika katika hilo tukio.
Walimpa kipigo zaidi ili aseme mengi juu ya pikipiki hiyo alioiba Segerea ndipo akaanza kusema akuwa peke yake, alikuwa na wenzake baada ya kuiba hiyo pikipiki waliipeleka makao makuu. Lakini huko makao makuu akujua aliuziwa nani maana wao kazi yao kuiba pikipiki na kuzifikisha makao makuu yao, maswala ya kuuza anajua bosi wao.
O.S.S mkuu wa upelelezi alimuuliza huyo mwizi anapopatikana huyo mkuu wao. Mwizi alisema anapopatikana huyo mkuu wao. O.S.S anatoa hoda akamatwe mara moja, anamtumia Muona afanye hiyo kazi, Muona akupoteza muda anaenda. Muona kwakuwa Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki ni mpenzi wake alimpigia simu.
"Mwanaume upo wapi?'
"Nyumbani mwanamke"
"Ok! nakuja sasa hivi nimekumiss sana"
"Sawa! utanikuta"
Muona alikata simu, anaambatana na askari wenzake wanaingia katika gari la polisi wanaelekea nyumbani kwa mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani. Safari ya kutoka kituo cha polisi hadi nyumbani kwa mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani, mwendo wa dakika ishirini wanafika nyumbani kwa mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki. Gari la polisi lilisimama mbali na hapo nyumbani kwa mkuu wa kitengo wizi wa pikipiki mitaani.
Muona aliingia ndani ya nyumba ya mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani na askari wengine wanaizunguruka nyumba yote. Chakushangaza Muona alipoingia ndani alikuta milango yote ipo wazi na nyumba imetawariwa na ukimya. Aliingiwa na wasi wasi na alijiandaa kukabiliana na hatari yeyote itakayotokea mbele yake lakini alipofika sebuleni.
"Haah! Mungu wangu!"
Alishtuka baada ya kumuona Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani ameuliwa kinyama na ametobolewa macho. Alipiga simu kwa askari wenzake waliopo nje na kuwaita haraka ndani. Askari walifika haraka haraka huku wakiwa na taadhali kubwa, walishtushwa baada ya kumuona Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani ameuliwa kikatili sana. Hakuna aliyekuwa tayari kuamini kwamba, kweli Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani amekufa, wakati muda mfupi uliopita Muona ametoka kuongea nae, ilikuwa ni kama ndoto! Muona aliishiwa nguvu na kujiona mpumbavu, mpango wake wa kuanzisha mahusiano na Scorpion ili kumtia nguvuni umeferi.
Alijiona mpumbavu wa wapumbavu kwa kumkabidhi Scorpion mwili wake akauchambua kama karanga mwisho wa siku, Scorpion amekufa bila kutimiza lengo la kumkamata kwa mikono yake. Alijilaumu tena na tena na kujitoa thamani kama mwanamke yeyote duniani kote, aliamini kumpa penzi Scorpion ndio njia ya kumkamata na ndio ungekuwa mwisho wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani lakini sivyo alivyotarajia.
Scorpion amekufa, askari wanafanya uchunguzi eneo lote la nyumba ya Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani bila kupata ushahidi wowote. Taarifa ilifika kwa O.S.S na wanaibeba maiti ya mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani na kuifikisha hospitali ya Amana.
**********
Msaidizi wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani akiwa makao makuu akiendelea na kuboa pikipiki na kutoa injini bila kujua kinachoendelea kama vijana wake wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani wamekamatwa na Scorpion mkuu wake ameuliwa kinyama na watu wasiojulikana. Simu yake ya mkononi inaita anaitoa mfukoni anaangalia ni namba 0764 07 07 97 ni namba ngeni katika simu yake, anapokea.
"Bila shaka assistance director Scorpion Gereji?"
"Ndio"
"Mimi ndio bosi wa injini za pikipiki hapo Scorpion Gereji sasa naomba tukutane kwa ajiri ya kufanya biashara za injini"
"Sawa! lakini vizuri zaidi ungekuja ofisini hapa"
"Nilitaka nije lakini nahofia foleni sasa naomba chukua pikipiki uje wewe Kurasini shimo la udongo"
"Sehemu gani?"
"Ukifika katika ofisi ya Camel Oil nijulishe nitakuelekeza kwa kuja"
"Sawa! bosi"
Simu ilikatwa, msaidizi anampigia simu mkuu wake ili kumjulisha taarifa hiyo lakini simu ilikuwa inaita bila kupokelewa. Anatuma meseji kuwa anaenda kukutana na mnunuzi wa injini kwa ajiri ya kufanya mazungumzo ya biashara. Simu ilikuwa chini ya mikono ya askari, askari walipopata taarifa hiyo wanagundua kuwa huyo msaidizi anahusika katika kitengo cha wizi wa pikipiki na huyo bosi mnunuzi wa hizo injini za pikipiki ni muhimu kupatikana. Walituma meseji na kujifanya Scorpion na kumwambia kuwa anafika hapo makao makuu muda si mrefu.
Msaidizi baada ya kupokea taarifa hiyo kutoka katika simu ya bosi wake aliamua kusubiri hadi bosi wake afike. Akiwa anamsubiri bosi wake mara simu yake inaita, anatoa mfukoni anaangalia ni namba ya yule mnunuzi.
“Umefikia wapi mpaka muda huu?”
“Namsubiri bosi afike ili tuje wote maana nimeongea nae sasa hivi, amese...."
Kabla ajamaliza kusema, simu ilikatwa. Msaidizi anashangaa kukatwa simu ghafla anampigia lakini simu aipatikani. Msaidizi anapiga simu katika simu ya bosi wake, lakini simu inaita bila kupokelewa. Muda huo huo anatumiwa ujumbe mfupi na simu ya bosi wake kuwa yupo njiani anaendesha gari.
Msaidizi baada ya kupokea ujumbe huo aliendelea kusubiri ghafla bila kutegemea, alishtukia askari wanaingia na kumuweka chini ya ulinzi. Msaidizi wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani alitii sheria bila shuruti ananyoosha mikono juu, wanampokonya simu na wanamkamata wanamtoa nje wanamuingiza katika gari, hawakupoteza muda eneo hilo wanawasha gari na kuondoka.
Walipofika kituoni walimuingiza selo kiongozi msaidizi wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani. O.S.S aliangalia katika simu ya huyo msaidizi wa kitengo cha wizi wa pikipiki mtu wa mwisho kuongea nae ni nani? ndipo wanagundua ni private namba ilikuwa ngumu kumjua, walipiga hiyo namba lakini simu ilikuwa aipatikani. Walienda hadi selo wakamtoa msaidizi na kumuingiza chumba cha upelelezi na kuanza kumpa adhabu kali ili aseme aliekuwa anaongea nae nani na yupo wapi?. Lakini msaidizi akuweza kumjua kwa jina huyo aliekuwa anaongea nae zaidi aliwaambia kuwa alijitambulisha kama mnunuzi wa injini za pikipiki na alitaka wakutane waongee kuhusu ununuzi wa injini za pikipiki.
O.S.S alitoa simu ya Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani na kupiga katika simu ya msaidizi wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani.
“Namba ya nani hiyo?”
Msaidizi anaangalia anaona namba ya bosi wake.
“Ni bosi wangu”
“Yupo wapi?”
“Aliniambia yupo njiani anakuja ofisini?”
Mkuu wa upelelezi alitoa picha za maiti ya mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipki anamuonesha huyo msaidizi.
“Ndiyo huyu?”
Msaidizi anaangalia hiyo picha anashtuka baada ya kumuona ameuliwa kinyama.
"Ndiyo huyo?"
"Ndiyo!"
“Ameshauliwa na watu wasiojulikana kwa hiyo tunataka kufahamu yote kuhusu yeye”
O.S.S baada ya kumwambia hivyo huyo kiongozi msaidizi wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani, anawaambia askari waletwe wale wezi waliohusika katika mauaji ya dereva pikipiki Segerea, askari walifanya kama walivyoambiwa, hao wezi waliletwa.
“Mnamfahamu huyu?"
Wezi walithibitisha wanamfahamu msaidizi wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani.
"Kama nani kwenu?”
“Kiongozi badala ya bosi hapo tulipokuwa tunafanya kazi”
Walijibu wote kwa pamoja.
“Vizuri! Hawa ndio waliohusika katika mauaji ya dereva pikipiki Tabata Segerea na kuiba pikipiki na hiyo pikipiki imehusika katika tukio lingine la mauaji Tabata Mawenzi na miongoni mmoja wapo aliokuwepo katika hilo tukio ni Imamu wa msikiti wa Almasjid Tidc Tabata Mawenzi kituo cha chama, sasa kama kiongozi wa genge lenu la wizi utakuwa unafahamu tukio hilo”
Kiongozi msaidizi wa kitengo cha wizi wa pikipiki alianza kukumbuka juu ya tukio hilo, anaanza kuelezea juu ya tukio ilo lilivyokuwa hadi kufika katika mauaji.
**********
Wakati wa tukio hilo kabla ya kutokea msaidizi alikuwa na muda wa miaka mitatu katika kitengo hicho cha wizi wa pikipiki mitaani na biashara ya madawa ya kulevya ilikuwa haiendi vizuri kwa sababu mtu wa kusafirisha hakuwepo. Scorpion alilazimika kumshawishi Imamu Shafii wa msikiti wa Almasjid Tidc, amtumie katika biashara ya madawa ya kulevya kwa kutumia mwavuli wa dini. Imamu Shafii wa Almasjid Tidc alikataa. Scorpion akagundua njia nyingine ya kumwingiza katika biashara hiyo Imamu Shafii. alimtumia kijana mmoja kutokea Tbata Kimanga eneo la Mandela juu ambae alijukana kwa jina Yahaya Salumu almaarufu Albata Dickson. Scorpion alimchagua kijana huyo kutokana na uwezo wake wa kumshawishi mtu.
Siku ya kwenda mitaani kuiba pikipiki, wezi wote walipangiwa kwa kwenda kuiba pikipiki lakini Albata akupangiwa aliambiwa kuna kazi nyingine anatakiwa apewe. Albata alisubiri hiyo kazi aliokuwa anatakiwa kupewa na bosi wake. Baada ya kusubiri kwa muda, aliitwa ofisini, alipofika ofisini alipewa kazi ya kwenda Tabata Mawenzi katika msikiti wa Almasjid Tidc kumshawishi Imamu ili wafanye nae miadhara mikoa mbalimbali na nje ya nchi.
Albata alikubali kuifanya hiyo kazi na aliahidi kuikamilisha ndani ya muda mfupi kutokana na uwezo wake wa kushawishi na kwakuwa huyo Imamu Shafii anafahamiana nae sana. Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani alimuahidi donge nono la pesa endapo Imamu huyo akikubali. Alipewa pesa ya matumizi akiwa katika hiyo kazi ya kumshawishi Imamu Shafii na ile pikipiki ilioibiwa Tabata Segerea ilitolewa preti namba yake, ikawekwa preti namba nyingine akapewa Albata kama usafiri wakati wa kwenda kumshawishi Imamu Shafii.
Siku iliyofuata, Albata anafika Tabata Mawenzi katika msikiti wa Almasjid Tidc, mishale ya saa saba mchana aliungana na waumini wa kiisalmu katika ibada ya saa saba. Dakika kumi baadaye, wanamaliza ibada. Albata anamuona Imamu anatoka ndani ya msikiti anaondoka, alimuwai alimuomba kuongea nae. Imamu kwa jinsi alivyomuona Albata akuweza kumtiria mashaka kwakua alikuwa amevaa kanzu safi vazi la waumini wa kiume wa kisalamu, kibarakashia na sendo nzuri kwa haraka haraka vitu vyote alivyo vaa thamani yake kama laki moja na nusu.
Imamu alijua Yahaya anataka kuoa, anatafuta shekhee wa kusimamia ndoa yake, bila kipingamizi anakubali kumsikiliza.Ndipo Yahaya alimwambia Imamu anataka kuambatana nae katika mikoa na nchi mbali mbali ili kufanya miadhara juu ya mafudisho ya dini ghalama zote kama usafiri, chakula na malazi atasimamia yeye. Imamu Shafii alikubali bila kipingamizi maana ndio jambo kila siku alikuwa anawaza juu ya kufanya muadhara kuhusu mafundisho ya dini ya kiislamu lakini tu pesa ndio ilikuwa tatizo.
Walipanga siku ya kukutana tena ili wapange mambo mengine ya mafundisho na wapi wataanzia. Walipeana namba za simu na wanaagana Imamu Shafii anaondoka hapo msikitini akiwa mwenye furaha sana baada ya kusogezewa fursa ambayo alikuwa anaitaka kuifanya lakini alikosa pesa na wafadhiri.
Yahaya aliondoka hadi ofisini kwao Scorpion Gereji. Alipofika alikutana na Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki alimpa taarifa ya kuwa Imamu Shafii amekubali. Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani alifurahi sana, imani yake ilisadiki mpango wake unakwenda kufanikiwa na mradi wake utakuwa sawa muda wowote.
Siku iliyofuata Yahaya alienda Almasjid Tidc, ndio siku waliopanga kukutana na Imamu Shafii, anakutana na Imamu Shafii, baada ya ibada ya saa kumi Imamu Shafii alimtambulisha Yahaya kwa waumini wote na akawaeleza juu ya ujio wake. Waumini walifurahi sana na kumshukuru kwa kujitolea kusambaza dini na kutoa mafundisho ya neno la mungu.
Siku hiyo hiyo baadaye, Imamu Shafii aliwachukua baadhi ya waumini aliowaona watafaa katika hiyo kazi ya muadhara, walikaa pamoja na Yahaya walianza kupanga mambo mengi juu ya muadhara na kwa kuanzia muadhara.
Dakika mia moja themanini, ziliwatosha kupanga mambo yote na kumaliza, Yahaya aliondoka, alirudi hadi ofisini na kukutana na mkuu wake na alimwambia maendeleo mazuri Imamu amewashirikisha baadhi ya waumini wake. Ilikuwa furaha ilioje kwa Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki aliamini kupiga hatua katika huo mradi wake maana Imamu Shafii akishirikiana na waumini wenzake ndio itakuwa vizuri atawatumia wote kuwabebesha madawa ya kulevya kutoka nchi zinazouza madawa ya kulevya na kusafirisha madawa ya kulevya wakiwa wanaenda katika hiyo miadhara.
Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani alimpatia pesa Yahaya na alimwambia akawanunulie kanzu, kofia ambazo watazitumia watakapoanza kazi ya miadhara na wakimaliza kununua hivyo vitu aende na huyo Imamu hadi hoteli ya Kilimanjaro ili wakale chakula cha mchana. Yote ni kumvuta Imamu Shafii katika kazi yao. Yahaya alifanya kama alivyoambiwa, alimpigia simu Imamu Shafii na kumwambia wakutane kariakoo, bila kipingamizi Imamu Shafii alikubali wito.
Imamu Shafii alipanda gari kituo cha chama, alielekea kariakoo. Alitumia kama nusu saa kufika kariakoo alikutana na Yahaya. Yahaya alimuongoza Imamu Shafii katika duka wanalouza kanzu, kofia na vitu vingine vya aina hiyo na kuanza kununua. Imamu alifurahi sana na alimshukuru Yahaya.
"Mungu akufanyie wepesi katika mambo yako ili ufanye makubwa zaidi ya haya"
"Inshallah!"
"Maana ni vijana wachache wenye nia kama yako, wengi wao pesa zao wanazitumia katika anasa'
"Ni kweli'
"Lakini wewe mungu amekupa ufahamu wa kufanya haya ni jambo kubwa sana, nakuombea maisha marefu ufanye makubwa"
"Inshallah!"
Walimaliza kununua vitu vyote, walitumia usafiri wa gari aliokuja nayo Yahaya na walielekea hadi hotel mashuhuri hapo mjini inayojulikana kama HYAUPEGENCY DAR ES SALAAM THE KILIMANJARO. Kwa mara ya kwanza Imamu anaingia ndani ya hoteli hiyo kila kitu kwake kilikuwa kigeni. Yahaya alimuongoza hadi ndani ya hiyo hoteli hadi sehemu ya chakula lakini cha kushangaza Imamu aliwaona mashekhee wengi lakini wengi wao ni vijana wazee wachache.
Yahaya alimuelekeza sehemu ya kukaa Imamu Shafii baada ya hapo alienda kwa kila shekhee na kuanza kumsalimia na kumkaribisha. Imamu shafii alikuwa katika hali ya mshangao huku imani yake ilisadiki kuwa ni mtu mashuhuri na mwenye pesa ila ni muda gani ameanza kuwa na pesa kiasi hicho cha kuweza kuwapeleka watu wengi kiasi hicho hoteli hiyo kubwa kwa sababu anamfahamu Yahaya pamoja na familia yake.
Yahaya alimaliza kumsalimia kila shekhee alirudi kukaa na kwa pamoja wakapata chakula na wageni wake wote. Walipomaliza kula kila shekhee alijitambulisha sehemu anayotoka, wengi walikuwa wanatoka mikoani. Walipata kufahamina mashekhee wote, Imamu Shafii peke yake ndio anatoka mkoa wa Dar es salaam. Baada ya utambulisho, Yahaya alijitambulisha kwa mashekhee wote na kuwaeleza kazi itakapoanzia ya miadhara na mafundisho ya dini. Kila shekhee alielewa na kuahidi kutoa elimu kubwa juu ya mafundisho ya dini sehemu zote.
Dakika ishirini na tano baadaye, walifika watu walimpa kila shekhee bahasha yake, baada ya hapo kikao kiliisha na kila mmoja alipata nafasi ya kuondoka. Yahaya na Imamu Shafii waliingia ndani ya gari waliokuja nayo na kuondoka hotelini hapo, walielekea hadi Tabata Mawenzi msikiti wa Almasjid Tidc. Walipofika Imamu aliweka ndani hivyo vitu, baada ya kuhakikisha vipo sehemu salama aliingia ndani ya gari na Yahaya alimpeleka Imamu hadi nyumbani kwake, baada ya hapo Yahaya aliondoka zake.
Siku hiyo hiyo jioni, Imamu alipata nafasi aliichukua ile bahasha aliopewa akaanza kuifungua, cha kwanza alikutana na kibunda cha pesa alishukuru mungu maana ni mwanzo mzuri wa mafanikio lakini alipofungua zaidi hiyo bahasha alikutana na barua. Taratibu aliifungua na kuanza kuisoma lakini hapo hapo muonekanao wake wa sura ulianza kubadirika baada ya kusoma kilichoandikwa ndani ya hiyo barua akutaka kuendelea kusoma hiyo barua aliikunja na kuirudisha ndani ya hiyo bahasha pamoja na zile pesa alizozikuta ndani ya hiyo bahasha.
Muda huo huo Imamu Shafii alitoka nyumbani kwake alienda hadi msikitini akaweka hiyo bahasha katika vitu alivyonunuliwa, baada ya hapo alimpigia simu Yahaya wakutane msikitini. Yahaya aliitikia wito, alifika msikitini alikutana na Imamu Shafii. Imamu Shafii cha kwanza alimkabidhi Yahaya vitu vyote alivyonunua kwa ajiri yake na waumini wengine.
"Aiwezekani, aitowezekana na kama utaendelea kuja hapa msikitini kwa ajiri ya ibada na si vinginevyo"
Imamu akutaka hata jibu taratibu aliondoka na kumuacha Yahaya hapo eneo la msikitini. Yahaya alibaki katika mshangao kwa kile alichojibiwa na Imamu Shafii, kutokana na muonekano aliomuona nao Imamu, akutaka kumwita ili afahamu nini kimetokea mpaka amerudisha hivyo vitu, alipanga kurudi siku nyingine baada ya hasira zake kuisha hivyo alichukua hivyo vitu na kuondoaka.
Njiani alijiuliza mengi juu ya uhamuzi aliochukua Imamu Shafii wa kukataa wakati kamwambia jambo zuri la miadhara juu ya mafundisho ya dini. Hadi anafika nyumbani kwake akuweza kutambua nini hasa Imamu Shafii kimembadilisha mawazo yake. Anafika nyumbani kwake alishusha huo mzigo wa vitu aliourudisha Imamu Shafii lakini akiwa ameubeba anapeleka ndani ghafla inaanguka bahasha chini anaiyokota anaingia ndani.
Alipofika ndani aliweka hivyo vitu alikaa chini akaanza kufungua hiyo bahasha, alianza kukutana na pesa katika kibunda aliziesabu kwa haraka haraka aligundua ni taslimu laki tano. Alipoangalia vizuri ndipo alipoona karatasi nyeupe, aliitoa hiyo karatasi na kuanza kuisoma. Alichokisoma katika hiyo barua akutaka kundelea tena kusoma hata nguvu ya kuiweka hiyo barua katika bahasha yake alishindwa alijiraza hapo katika kochi mpaka usingizi ukampitia.
Masaa mawili yalikatika mpaka kuja kuzinduka, ilikuwa ni saa sita na dakika ishirini, alichukua maji aliweka katika ndoo ya chooni aliingia bafuni na kuanza kuoga. Alitumia dakika tano kuoga alipomaliza alijiandaa kwa vazi lake la kanzu aliondoka hadi msikitini. Hadi anafika hapo msikitini muda wa ibada ulikuwa ushawaidia hivyo aliungana na waumini wa kiislamu waliingia katika ibada. Sala iliongozwa na Imamu Shafii mpaka anamaliza. Muda wa kutoka Yahaya alionana na Imamu Shafii, alimuomba kuongea nae.
Imamu Shafii akutaka kuongea wala kumsikiliza Yahaya, Yahaya alijitetea akuja na yale yale ila amekuja kwa kuhitaji msamaha kwa kile kilichotokea kwa sababu hata yeye alikuwa ajui. Imamu Shafii akuweza kumuelewa maana yeye ndie aliejitambulisha kama ndio kila kitu katika mpango huo wa kufanya miadhara mikoani na nje ya nchi na ghalama zote atazisimamia yeye mwenyewe sasa leo hii iweje aseme hata yeye alikua ajui.
Yahaya alimuomba sana Imamu, akasababisha Imamu kuchukia na kuanza kongea kwa ukali akimsisitiza ataki kuongea nae, Imamu Shafii hasira zilimpanda hadi alitaka kumpiga Yahaya lakini waumini waliokuwepo hapo msikitini walimzuia Imamu na kummtuliza. Wengine walimwambia Yahaya aondoke ili kuepusha matatizo. Yahaya alitii kauli ya waumini aliingia ndani ya gari aliondoka. Yahaya akupenda kwa kile kilichotokea maana huyo Imamu wanafahamiana sana na anamuheshimu sana. Njia nzima alisikitika sana kwa kumkosea bila kujua, alishindwa kujizuia machozi yalimtiririka na kuanza kulia kwa uchungu.
Waumini walitaka kufahamu nini hasa mpaka wanakosana na Yahaya lakini Imamu akutaka kueleza chochote kilichotokea ila tu aliamua kuondoka msikitini hapo na kuelekea nyumbani kwake. Alipofika nyumbani kwake akuwa na furaha, mkewe aliigundua hali hiyo alimuuliza lakini Imamu akutaka hata kumueleza kilichotokea zaidi tu alimwambia mke wake kuna mtu wamekosana kikauli. Mke wa Imamu akutaka kufatiria sana.
Safari yake Yahaya iliishia hadi nyumbani kwake. Alichukua ile bahasha na kuondoka hadi makao makuu ya kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani. Alipofika makao makuu moja kwa moja hadi ofisini kwa bosi wake alimkuta mkuu wake na msaidizi wake ambae ni fundi wa pikipiki katika hicho kitengo cha wizi wa pikipiki. Bila salamu aliaanza kumwambia ameshindwa kumshawishi Imamu. Mkuu wake alimuuliza sababu ya kushindwa kwake, Yahaya alitoa ile bahasha na kuibwaga mezani.
“Kama ningejua kuwa ni kumshawishi kwa ajiri ya kumtumia katika kufuata madawa ya kulevya na kusafirisha madawa ya kulevya, nisingethubutu kumwambia maana yule kama mzee wangu pia namuheshimu sana na yeye ananiheshimu ndiyo maana nilipomshawishi juu ya kufanya miadhara alikubali haraka”
“Sikiliza kama uliamua kuingia katika kazi ya wizi wa pikipiki tena unaua vipi unashangaa kusambaza madawa ya kulevya”
“Mkuu bora ingekuwa mimi lakini sio wale viongozi wa dini na kubwa zaidi ananijua mimi hadi familia yangu unafikiri itakuwaje kama akienda kutoa ripoti kituo cha polisi?”
“Hana ushahidi wala kidhibiti vizuri barua hii imerudi”
“Sawa! nimefanya kosa kubwa sana ila naomba asichukue hatua yeyote ila kwa sasa nimeshindwa tena hiyo kazi”
Aliondoka na kumuacha mkuu na msaidizi wake humo ofisini kwake lakini kabla Yahaya ajatoka mlango mkubwa wa kutoka nje msaidizi alimuwai na kumsimamaisha.
“Bosi anakuhitaji ili muyamalize mjue mnafanya nini ili kuifanya siri ili lililotokea”
“Siitaji tena maana nimesababisha nimegombana na Imamu wa mtaani kwangu unafikiri uso wangu nauweka wapi?”
“Ndio maana anakwita ili mjue mnafanyaje kumaliza ili tatizo maana sio tatizo kwako hata kwake endapo huyo Imamu akitoa ripoti polisi itakuwaje?”
“Angekuwa analijua ilo angeniweka wazi juu ya huo mpango mapema lakini akaniambia kuwa nimshawishi ili tumtumie katika miadhara juu ya mafundisho ya dini ili kupata Baraka kutoka kwa mungu lakini kumbe sivyo kumbe anataka kumtumia kusafirisha madawa ya kulevya?”
“Yameshatokea mnatakiwa kuyamaliza”
“Nitalimaliza mwenyewe sio na yeye tena”
Yahaya aliondoka, msaidizi anabaki kumuangalia mpaka anapotea machoni mwake, taratibu anarudi ndani alipofika kwa mkuu anamwambia amekataa.
“Tutajua cha kufanya kila kitu kitaenda sawa!”
**********
Siku iliyofuata ilikuwa ni siku ambayo sherehe katika kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani, baada ya kila kijana kufanikiwa kurudi salama usalimini kutoka mitaani kuiba pikipiki na kufanikiwa kuiba pikipiki nyingi na kuzidi kuiingizia pesa kampuni hiyo ya Scorpion gereji.
Waliandaa tafrija fupi humo humo ndani ya kitengo chao cha wizi wa pikipiki mitaani, walikunywa na kufurahi, waliokoseana waliitumia siku hiyo kuombana msamaha na kuyasahau yote yaliopita. Yahaya ni miongoni aliekosana na bosi wake Scorpion. walitumia siku hiyo kuombana msamaha na kumaliza tofauti zao.
Kwa pamoja walikunywa na kufurahi mpaka kila mmoja alilewa hasa hasa bosi ndio alikuwa amelewa sana hadi kushindwa kuendesha gari lake kurudi nyumbani kwake. Aliteuliwa Yahaya ampeleke bosi nyumbani kwake. Bila kipingamizi Yahaya alikubali, akachukua funguo ya gari ya bosi wake akawasha gari, bosi akapanda wakaanza safari ya kuelekea nyumbani kwa bosi wake Scorpion Kijichi.
Muda wote wa safari bosi Scorpion alikuwa amelala siti ya nyuma katika gari, kutokana na pombe kumzidi sana bosi Scorpion alitapika ndani ya gari. Yahaya ikabidi asimamishe gari maeneo ya hospitali ya Mission. Bosi Scorpion alishuka ndani ya gari na kuanza kutapika, alitumia kama dakika tatu kutapika alipomaliza akaingia ndani ya gari na akamwambia Yahaya aendeshe gari.
Yahaya akafanya kama alivyoamrishwa na bosi Scorpion lakini Yahaya kabla ajaweka gea ili kuruhusu gari kuondoka ghafla kilitua kitu kizito kichwani kwake kilichosababisha kupata mshtuko hadi anadondokea katika usukani wa gari. Muda huo huo alipata kizunguzungu na kuishiwa nguvu hata gari alishindwa kuendesha. Kutokana na maumivu makali aliyokuwa anayasikia alianza kukoloma kwa sauti huku akijitaidi kuinua kichwa hapo katika usukani wa gari lakini akuweza kutokana akuwa na nguvu kabisa.
Hapo hapo bosi Scorpion aliinuka kutoka nyuma ya siti ya gari na kusogea hadi alipo Yahaya akavua tai yake na kumzingiriza shingoni na kuanza kumnyonga, aliona haitoshi tai peke yake kumaliza uhai wa Yahaya akatoa sindano ambayo ilikuwa na dawa kabisa kwa jinsi ilivyo ilikuwa imeandaliwa mapema na kumchoma ya shingo Yahaha mpaka kumkatisha uhai wake. Hapo ndio ulikuwa mwisho wa Yahaya wa maisha yake duniani. Bosi Scorpion baada ya kuhakikisha ameshammaliza Yahaya alitoa simu yake mfukoni alipiga.
“Nishamaliza kazi, kama dakika tano nitakuwa hapo”
Alimtoa Yahaya mbele ya siti ya dereva alipokuwa akamuweka siti ya nyuma, hapo hapo aligeuza gari alirudi alipotoka. Kutokana ulikuwa muda wa usiku, mwendo wa dakika kumi alifika makao makuu ya Scorpion Gereji. Alikutana na msaidizi wake akiwa na watu watatu wenye miili minene waliovalia vazi la suti nyeusi. Haraka haraka waliishusha maiti ya Yahaya katika gari ya bosi Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani, waliingiza katika gari nyingine ndani ya gari hilo iliyowekwa maiti ya Yahaya kulikuwa na rundo la vitabu vya biblia.
**********
Siku hiyo hiyo saa kumi usiku, kiongozi msaidizi wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani na wavaa suti watatu walitoka hapo makao makuu ya kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani kwa kutumia gari lakini Gari waliyoitumia ilikuwa ndogo, awakuweza kutosha wote, msaidizi wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani aliamua kuitumia pikipiki aliokuwa anaitumia Yahaya kwenda msikitini kwa Imamu Shafii.
Uzuri wa wa muda huo wa usiku kulikua hakuna foleni wala trafki, ikapelekea walitumia muda mchache kufika Tabata Mawenzi katika msikiti wa Almasjid Tidc, msikiti unaoongozwa na Imamu Shafii. Walipofika hapo msikitini kiongozi msaidizi wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani alibaki ndani ya gari. Walishuka hao wavaa suti watatu waliangalia mazingira ya eneo hilo la msikiti waliona usalama upo wa kutosha. Walishusha maiti ya Yahaya wakaibeba mkukumkuku na kuelekea ndani ya msikiti na mvaa suti mwingine alibeba rundo la vitabu alielekea ndani ya msikiti walipoelekea wenzake.
Walipoingia ndani walikaa kwa muda mrefu bila kujua kilichowachelewesha maana kilikua kitendo cha dakika chache tu kuiacha maiti ya Yahaya na hivyo vitabu hapo msikitini. Ndipo kiongozi msaidizi wa kitengo cha wizi mitaani alishuka ndani ya gari alielekea ndani ya msikiti. Alipoingia ndani ya msikiti alikuta hao wavaa suti wanapigana na huyo Imamu Shafii. Alipiga hesabu za haraka haraka afanye nini maana muda unaenda wanaweza kukutwa na waumini wa kiislamu wanaokuja msikitini kwa muda huo ikawa tatizo. Akapata wazo la haraka, alienda hadi katika gari. Alipofika ndani ya gari alifungua buti la gari,alichukua nyundo ya kupasuria kokoto akaibeba na kuingia ndani ya msikiti.
Alipofika ndani ya msikiti alikuta hao wavaa suti wamemdhibiti Imamu Shafii ndipo hapo roho ya huruma ilipotoweka moyoni mwake kiongozi msaidizi wa kitengo cha wizi mitaani, alisogea akanyanyua nyundo akampiga ya kichwa Imamu Shafii, Imamu Shafiialipiga kelele kali za maumivu na kichwa kilipasuka damu zilitapakaa eneo hilo, akuweza tena kuwa na nguvu taratibu aliishiwa nguvu alianguka chini alikata roho hapo hapo, wote walitulia wakimungalia.
“Itakuwaje na kazi iliotuleta atujaifanikisha”
Mmoja wa wavaa suti aliwaambia wenzake.
“Aina haja tena, lengo maiti hile kuiterekeza ili kesi ya mauaji iende kwa Imamu na waumini wake kwa hiyo zoezi lile tusitishe, tuondoke na huyu ili zoezi liishie kwake maana muda umeenda?”
Walikubaliana hao wavaa suti na kiongozi msaidizi wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani haraka haraka wanambeba Imamu Shafii na kutoka nae huku damu zikiwa zinachuruzika kutoka kichwani na puani. Wanafika katika gari yao waliokuja nayo wanauweka mwili wa Imamu Shafii, wanairudia maiti waliokuja nayo wanaibeba wanaenda kuiingiza ndani ya gari wanaondoka zao.
Safari yao iliishia hadi darajani maeneo ya Tabata Chama karibu na Shule ya msingi wanasimamisha gari yao wanashuka wanaangalia mazingira wanaona hakuna mtu anaeonekana wala kupita au kusogea eneo hilo. Wanashusha pikipiki wanaiweka barabarani, wanashusha maiti ya Yahaya wanaisogeza hadi ilipo pikipiki na wanaipakiza katika pikipiki. Mmoja wa wavaa suti anachukua petrol katika gari wanaimwagia mafuta pikipiki yote na hiyo maiti. Baada ya hapo wanaushusha mwili wa Imamu Shafii wanamuweka katikati ya barabara hatua chache na maiti iliopakizwa katika pikipiki ya Yahaya.
Baada ya kumaliza kufanya hayo yote, ndipo wanaiwasha moto maiti ya Yahaya inaungua pamoja na pikipiki, wanaingia ndani ya gari wanaondoka eneo hilo.
**********
Kiongozi msaidizi wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani Scorpion Gereji anamaliza kuhadithia. Ukweli wote unajulikana juu ya tukio la Tabata Mawenzi eneo la Almasjid Tidc na darajani. Kwakuwa Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani ameshakufa, kiongozi msaidizi wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani na vijana wake wote wanaonekana ndio watuhumiwa wa tukio la Tabata Mawezi eneo la Almasjid Tidc na darajani wanafunguliwa kesi ya mauJI.
Mpelelezi na Muona waliamini Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani ameuliwa kwa lengo la kupoteza ushahidi, ndipo wanaamua kufatiria ili kumjua muuaji wa Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani. Muona imani yake ilisadiki kuwa O.S.S mkuu wake wa upelelezi ndio yupo nyuma wa haya yote kulingana na baadhi ya mambo kuvuja kwa watu wabaya wakati ilikua siri yao, hivyo anamwambia mpelelezi wasishirikishe O.S.S mkuu wao wa upelelezi, mpelelezi anakubali wazo la Muona.
"Kwanza tuwasiliane na makao makuu ya mtandao wa simu baada ya hapo tufatilie Gprs"
Muona alimwambia mpelelezi.
"Kwa lengo gani?"
"Kujua mawasiliano ya simu ya mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki na wote aliowasiliana nao baada ya wewe kupata matatizo"
"Vizuri! Muona"
Wanakubaliana kupiga simu katika mtandao wa simu, kwakua namba ya mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki kila mmoja anayo ilikua kazi rahisi. Muona anakumbuka siku aliyopata tatizo mpelelezi, Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani alituma namba ya ofisi ya kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani, makao makuu ya mtandao wa simu na kuwaambia anataka kujua mara ya mwisho namba hiyo ni namba hipi ya mwisho kuwasiliana nayo na siku aliokwenda ofisini kwa mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani, alipofika karibu na mlango alimsikia mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani anaongea na simu, maongezi yake ya kuomba msamaha. Baada ya kukumbuka hayo yote, anakumbuka aliandika katika simu yake siku, tarehe, mwezi, mwaka na muda huo mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki aliokua anaongea na simu
"Kazi imeisha"
Muona alimwambia mpelelezi huku anaandika namba za kuongea na mtu wa makao makuu ya mtandao wa simu.
"Kazi imeisha kivipi?"
"Nishajua kwa kuanzia"
Alimuelezea mpelelezi, mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki alivyopiga simu katika mtandao wa simu na hadi alivyomsikia mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani ofisini kwake anaongea na simu akiomba msamaha.
"Vizuri! sasa jambo zuri ni kwenda makao makuu ya huo mtandao wa simu na sio kupiga simu"
Mpelelezi alimwambia Muona, Muona aliunga mkono wazo la mpelelezi na anaacha kupiga simu kwa pamoja wanaenda makao makuu ya huo mtandao wa simu.
Walichukua gari kituo cha Tabata Shule wanaelekea makumbusho. Mwendo wa lisaa limoja kutokana na foleni wanafika makumbusho makao makuu ya huo mtandao wa simu. Wanaenda moja kwa moja hadi makao makuu, wanajitambulisha kama askari huku wakionesha vitambulisho vyao na walieleza shida iliowaleta. Walisikilizwa na kuanza kushughulikiwa tatizo lao. Ndipo Muona alimpa huyo muhusika wa mtandao wa simu namba ya mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani.
"Naomba kujua maongezi yaliofanyika kati ya namba hii na muhudumu wa ofisini kwenu"
Alimtajia siku, tarehe, mwezi na mwaka, huyo muhusika wa mtandao aliingiza hiyo namba katika mashine na kutafuta mawasiliano ya siku, tarehe, mwezi na mwaka kati ya mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani na muhudumu wa mtando huo ndipo anagundua maongezi yao wanayasikiliza mwanzo hadi mwisho na wanaiyona namba aliotumiwa mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani. Mpelelezi anaiandika katika simu yake lakini mpelelezi anaikumbuka hiyo namba.
"Muona hii namba ndio ilyonipigia na kuniita niaende Buguruni Skita nikabebe pikipiki"
"Kweli Job"
"Ndio"
Muona anamwambia huyo muhusika wa mtandao wa simu ahangalie mawasiliano yote kuanzia siku hiyo mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani alipotumiwa namba hiyo na muhudumu wa mtandao wa simu. Muhusika aliangalia na aliona maongezi yote na kuanza kupitia mawasiliano yote na kuyasikiliza ndipo wanagundua kuwa mawasiliano alioyafanya mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani akiwa ofisini kwake akiomba msamaha juu ya kuwachukulia hatua askari mpelelezi Job na Muona.
Pia namba hiyo hiyo ilitumika kumpigia simu kiongozi msaidizi wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani ili wakutane wafanye maongezi ya biashara na ni namba hiyo hiyo aliotumiwa na muhudumu wa mtandao wa simu lakini walishindwa kugundua huyo mtu ni nani bali tu alisikika mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani akisema samahani mheshimiwa ndipo mpelelezi na Muona kila mmoja aliuliza mheshimiwa yupi? Lakini hakuna alieweza kumjua huyo mheshimiwa, ni mheshimiwa yupi hata walipojitaidi kusikiliza sauti ili kujua sauti ilikua bado aitoshi kumfahamu huyo mheshimiwa ni mheshimiwa yupi?.
Muhusika wa mtandao alipoangalia katika usajiri hiyo namba ilikua aijasajiriwa. Mpelelezi na Muona walipata wakati mgumu sana wa kumjua huyo mheshimiwa. Awakuwa na muda wa kupoteza hapo makao makuu ya mtandao wa simu, walimshukuru muhusika wa mtandao kwa kuwasaidia kufahamu baadhi ya mambo waliaga na waliondoka.. Njia nzima si mpelelezi wala Muona wote walitawariwa na mawazo lakini Muona anakumbuka Gprs.
"Nimekumbuka kitu"
"Kipi?"
"Tulipokuamisha kutoka Amana kukupelekea hospitali ya Lugalo, mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki alifahamu wakati ilikua siri lakini yeye alisema alifahamu kupitia Gprs"
"Gprs"
"Ndio Gprs lakini kwa maelezo ya mkuu wetu walipokuokota ukiwa hoi hoi aukuwa na kitu chochote si simu yako wala ile simu ya ofisi ya kitengo cha wizi wa pikipiki"
"Kwa hiyo?"
"Sasa simu yako na simu ya ofisi ya kitengo cha wizi wa pikipiki atakua kachukua nani?"
"Hapo ndio tunatakiwa kujua kama msamalia alienisaidia au nani"
"Msamalia nakataa kwa sababu Gprs ilisoma mimi nipo hospitali ya Lugalo aliyakua sina simu yeyote"
"Hapo ndio kuna ukweli"
"Kwa hiyo?"
"Tufatilie Gprs tunaweza kufahamu ili kupitia hizi simu"
"Kweli!"
Walikubaliana kuitafuta simu kwa Gprs ili kujua simu yake mpelelezi na simu ya kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani. Walizitafuta simu zote kwa Gprs, walifanikiwa na simu ilisoma na kuonesha eneo ilipo, ni eneo la Kinondoni maeneo ya Leaders Club, nyumba iliopakana na Leaders Club.
Walichukua pikipiki hadi Leaders Club kwa muelekeo wa Gprs, Gprs inasoma katika nyumba ambayo ilisababisha askari mpelelezi Job na Muona washtuke baada ya kugundua ni kiongozi wao mkubwa wa upelelezi Tanzania. Awakuweza kuamini kama kiongozi huyo wa serikali ndio yupo nyuma ya matukio yote wizi wa pikipiki mitaani, tukio la darajani na madawa ya kulevya. Dakika ya mwanzo walihisi labda Gprs imekosea kusoma lakini iliwahakikishia ni hapo hapo. Ndipo mpelelezi akapata nguvu ya ufahamu na kukumbuka tukio la kupigwa, anagundua huyo kiongozi ndio alihusika na sauti aliokuwa anaifananisha wapi aliwai kuisikia kumbe ya huyo kiongozi wa serikali na alikumbuka mara ya mwisho wanapanga kumkamata mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki lakini ghafla wakasikia mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki amekufa. Moja kwa moja aligundua huyo kiongozi ndio amehusika kumuua Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani ili kupoteza ushahidi.
Baada ya kufahamu hayo awakupoteza muda haraka haraka wanachukua pikipiki hadi kituoni kwao Tabata Shule wanatoa taarifa kwa mkuu wao O.S.S kuwa washamjua muhusika alienyuma ya tukio la darajani, wizi wa pikipiki mitaani na maauji ya Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani. O.S.S alimwambia mpelelezi na Muona waandae askari ili kuvamia sehemu alipo ili kumtia nguvuni. Mpelelezi na Muona walifanya kama walivyoambiwa walichukua askari, askari walichukua siraha za kutosha waliambatana na O.S.S,mpelelezi na Muona waliingia ndani ya gari na kuelekea Kionondoni maeneo ya Leaders Club.
Mwendo wa dakika arobaini na saba, walifika Leaders Club katika hiyo nyumba iliombatana na Leaders Club. Walipofika hapo askari walishangaa kuona mpelelezi anasimamisha gari katika nyumba ya R.C.O.
"Mtuhumiwa mwenyewe yupo hapa?"
O.S.S aliuliza ili kupata uhakika.
"Ni R.C.O"
O.S.S akuweza kuamini baada ya kuambiwa kuwa R.C.O ndio mtuhumiwa mwenyewe. Walipiga honi ya gari getini mlango ulifunguliwa na gari la polisi liliingia ndani na walifanikiwa kumkuta R.C.O. Wanamuweka chini ya ulinzi ndipo R.C.O anataka kufahamu kwa kosa gani, mpelelezi anatoa maelezo, O.S.S anaruhusu wasachi ndani kwa R.C.O, walianza kusachi nyumba yote ndipo walifanikiwa kukuta simu ya mpelelezi, simu ya ofisi ya kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani na pamoja na madawa ya kulevya. Wanamuweka chini ya ulinzi R.C.O, R.C.O hakuwa na kipingamizi wanamkamata na kumfunga pingu wanaondoka nae kuelekea kituoni. Alipofikishwa kituoni anawekwa selo anafunguliwa kesi ya mauaji ya tukio la Tabata Mawenzi, mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani, kuchochea wizi wa pikipiki mitaani na kuuza madawa ya kulevya.
**********
Baada ya ushahidi kukamilika mpelelezi alienda hadi hospitali ya jeshi Lugalo anachukua vipimo vyote vilivyopatikana katika maiti ya dereva bodaboda ambae ni Yahaya ambae ni mwizi wa kitengo cha wizi wa pikipiki katika gereji ya scorpion na anauchukua mwili wa Yahaya anarudisha Amana. Baada ya kurudisha mwili wa Yahaya Amana, mpelelezi anaonana na daktari mkuu anaomba kuonana na daktari msaidizi wa daktari Mbaga. daktari mkuu anamwita daktari msaidizi wa daktari Mbaga kitengo cha uchunguzi wa maiti. daktari msaidizi wa daktari Mbaga alipofika, mpelelezi anamuwekwa chini ya ulinzi, anamkamata anaingizwa katika gari la polisi anapelekwa kituoni.
“Dokta wewe kama dokta msaidizi wa dokta Mbaga sasa baada ya dokta mbaga kutoa vipimo tofauti na hivyo vipimo vilikuwa vya uongo vikapelekea dokta Mbaga kuwa hatiani na kufunguliwa mashtaka ya kutoa vipimo vya uongo sasa wewe kama msaidizi ukatoa vipimo vyako ndio hivi”
Alimuonesha faili la vipimo vya dereva bodaboda na Imamu Shafii.
“Vipimo vyako vinaonesha Imamu Shafii amekufa na dereva bodaboda amekufa kwa ajari ya pikipiki sawa sawa?”
Daktari msaidizi wa daktari Mbaga kimya akiwa mwenye kihemo kwa mbali, ndipo daktari msaidizi wa daktari Mbaga alitoa maelezo yake baada ya vipimo vyake ambavyo alivipima baada ya mkuu wake daktari Mbaga kufunguliwa kesi. Maelezo yake yalijirudia yale yale ya Imamu Shafii na dereva bodaboda walikufa kwa ajari ya pikipiki, mpelelezi aliandika maelezo yake na anamaliza kumfanyia mahojiano anampeleka selo.
Kutoka hapo kituoni Tabata Shule, mpelelezi alienda hospitalini alikutana na daktari Mbaga akiwa katika umbo lile lile la Imamu Shafii alimfikishia taarifa ya kukamatwa kwa watuhumiwa wote wa kesi yake na alimtajia siku ya mahakama. Daktari Mbaga akiwa katika muonekano wa Imamu Shafii alimshukuru sana mpelelezi. Mpelelezi akukaa sana baada ya kumfikishia taarifa hiyo Daktari Mbaga aliaga na kuondoka. Daktari Mbaga alikuwa katika wakati mgumu kwakuwa katika umbo la Imamu Shafii. Alifikiria itakuwaje yupo katika umbo la Imamu Shafii wakati kesi hiyo inamkabiri yeye kwa kutoa vipimo vya uongo na kupokea rushwa. Lilikuwa ni fumbo lililotanda mawazoni mwake na kushindwa kulifumbua. Alitawariwa na mawazo na kupoteza unene wa umbo lake alilozoeleka akiwa katika kazi yake ya uchunguzi wa maiti katika hospitalli ya Amana.
**********
Agosti 19, ilikuwa ni siku ya mahakama ya kesi inayomkabili daktari Mbaga, daktari Mbaga aliamshwa na askari saa 07:30. Alitambua muda wa kwenda mahakamani umefika hivyo Mwili wake ulikuwa dhaifu na alikuwa anatetemeka juu ya muonekanano wa Imamu Shafii kuwepo katika mwili wake. Askari walifika hadi wodi aliokuwa daktari Mbaga walimchukua na kutoka nae nje wakamuingiza ndani ya gari wakaondoka nae.
Kutokana na foleni ya kutoka hospitali ya Amana kuelekea Mnazi mmoja, walitumia mwendo wa dakika kumi na tano kufika mahamakani. Gari aliyobebwa daktari Mbaga akiwa katika muonekano wa Imamu Shafii iliingia ndani ya jengo la mahakama inapaki na kushushwa daktari Mbaga akiwa katika umbo la Imamu Shafii.
Walimkokota taratibu na kuelekea zilipo vyumba vya mahakama lakini daktari Mbaga akiwa anakaribia moja ya vyumba vya wapelelezi, alipishana na mtu akiwa chini ya ulinzi wa askari magereza na mikononi amefungwa pingu. Daktari Mbaga akuweza kuamini alichokiona alihisi anaota lakini alipobaini hakuwa katika ndoto yeyote alisimama na kumuangalia huyo mtu hadi anafikishwa moja ya selo na kuingizwa ndani.
Daktari Mbaga alikuwa katika mshangao wa huyo mtu iweje kafanana nae, na ni nani amefanana nae na amekubali kusimama katika upande wa kesi yake. Alikuwa bado amesisimama hapo anafikiria lakini askari walimwambia waende, daktari Mbaga akiwa katika muonekano wa Imamu Shafii alitii kama alivyoanbiwa na hao askari hadi anafikishwa katika chumba cha peke yake cha wapelelezi alikuwa bado anamfikiria huyo mtu aliyofanana nae kila kitu.
Askari walimuacha hapo ndani na kutoka nje kudumisha ulinzi kwa upande wake. Lakini daktari Mbaga akiwa humo ndani alikuwa bado ametawariwa na mawazo kichwani mwake juu ya kumuona mtu amefanana nae tena, amefungwa pingu. Akiwa katika kutafakari ni nani aliefanana nae ghafla daktari Mbaga aliona mwanga mkali ukija chumba alichowekwa katikati yake, alikuwa mtu kavaa kanzu nyeupe mithili mwarabu wa dubai, sura na kichwa kimezibwa na kitambaa alichojifunika. Alisogea hadi katika kiti karibu na daktari Mbaga. Daktari Mbaga alikuwa aelewi mtu huyo ni nani na katokea wapi. Akiwa anajitaidi kumuangalia japo amuone hata sura, huyo mtu alianza kwa kumuuliza kana mawazo ya nini?
Daktari Mbaga akuweza kujibu na akili yake ilikuwa inatafakari anaweza kujibu juu ya mawazo yake amemuona mtu amefanana nae halafu kumbe anaemwambia ni askari mpelelezi amevaa kiraia. Akuweza kumwambia anachowaza zaidi alijitaidi kumuangalia japo aone sura yake. Mtu huyo aliyagundua mawazo yake mapema daktari Mbaga, alitoa kitambaa na kuonekana sura. Ndipo daktari Mbaga alimuona huyo mtu kumbe ni Imamu Shafii, Imamu Shafii alimuuliza daktari Mbaga.
"Unaelewa maana ya maono yale"
"Sielewi"
Daktari Mbaga alijibu haraka haraka Ndipo Imamu Shafii alimfafanulia.
“Maono haya yanamaanisha kuwa kila kitu kinawezekana ukiwa na imani"
Daktari Mbaga akuweza kumuelewa lakini akusubiri amuulize kwanini, Kivuli cha Imamu Shafii kilipomaliza kusema maneno yale, kiligeuka kikaondoka. Daktari Mbaga alimwita ili amuulize juu ya sura yake kubadilika badirika mara kuwa katika muonekano wake kama Daktari Mbaga mara kuwa katika muonekano wa Imamu Shafii lakini akuweza kusimama aliondoka. Daktari Mbaga alibaki katika dibwi zito la mawazo asijue cha kufanya huku akitafkari tamati ya kesi yake na huo muonekano wa Imamu Shafii.
Muda huo huo walifika askari magereza wakiwa pamoja na wale askari aliokuja nao hapo mahakamani walimchukua na walielekea mahakamani, njiani daktari Mbaga alikuwa anajitaidi kujiangalia sura yake ipo katika muonekano upi lakini alishindwa kujiona, hofu ilizidi kumtawara alipokaribia katika mlango wa kuingia ndani ya mahakama. Uvumilivu ulimshinda ikambidi asimame na kugoma kuingia ndani ya mahakama, askari magereza na askari wa kawaida walishangaa hali hiyo kwa upande wake.
"Naomba kwenda chooni nikajisaidie haja ndogo"
Hakukuwa na kipingamizi katika hilo askari magereza na askari wa kawaida walimuongoza hadi vyoo wanavyotumia wapelelezi hapo eneo la mahakama, walipofika hapo chooni walimuacha akaingia ndani ya choo. Awakuwa mbali muda wote walikuwa karibu na choo wakidumisha ulinzi juu yake, walikuwa wanamlinda kama Raisi. Daktari Mbaga alipofika chooni akuwa hata na shida ya kujisaidia haja ndogo bali alikuwa na shida ya kupata kioo ili kujitazama muonekanao wa sura yake. Aliangaza huku na huko ndani ya choo bila kuona kioo ukutani, alitoka akiwa akili yake imevurugika kabisa, akuwa na imani na sura yake hipo katika muonekano wa daktari Mbaga au Imamu Shafii.
Askari walipomuona ametoka chooni wakasogea karibu yake wakasimama askari wa kawaida mbele na askari magereza nyuma, wakaanza safari ya kuelekea jengo la mahakama. Awakuweza kupita tena njia ile waliokuja nayo wakati wanaenda chooni, walibadirisha na kupita njia nyingine. Njia hiyo waliopita wazipita selo za hapo mahakamani lakini selo ya mwisho, daktari Mbaga aliweza kumuona yule mtu ambae amefanana nae kama daktari Mbaga. Hapo ndio aliweza kumuona kwa uzuri yaani amefanana nae kila kitu aswaaa lakini chakushangaza daktari Mbaga akiwa katika muonekano wa Imamu Shafii alipatwa na mashaka. Alisimama na kumuangalia kwa muda na huyo mtu akiwa katika umbo la daktari Mbaga yeye alikuwa anamungalia kama anamfananisha kuna sehemu aliwahi kumuona hivyo wakawa wanaangaliana.
Askari waliangalia alipokuwa anaangalia daktari Mbaga lakini chakushangaza awakuweza kuonesha mshangao wowote kati ya daktari Mbaga na huyo mtu aliefanana na daktari Mbaga aliekuwa selo. Zaidi walimuamuru kuondoka kwakua muda wa kuanza kesi mahakamani ulikaribia, daktari Mbaga akiwa katika muonekano wa Imamu Shafii akubisha alipiga hatua na kuelekea mahakamani.
Njia yote daktari Mbaga alikuwa anafikiria ni nani ambae kafanana nae, ni pacha wake. Alifikiria sana lakini akuweza kupata jibu la haraka hadi wanafika jengo la mahakama. Alipokaribia mlango wa kuingia ndani ya mahakama mwanga ulipiga usoni alikinga uso kwa mikono na kusimama na kuangalia unapotoka huo mwanga. Ni katika gari iliopaki hapo eneo la mahakama, alipoangalia vizuri, ndipo aliona ni mwanga wa kioo cha gari. Alipoangalia hicho kioo ndipo alijiona yupo katika muonekano wa Imamu Shafii alishtuka sana. Mwili wake ulikuwa dhaifu na alikuwa anatetemeka juu ya muonekanano wa Imamu Shafii kuendelea kuwepo katika mwili wake, aliishiwa hadi nguvu akataka kudondoka lakini askari walimuwai haraka haraka wakamzuia na kumuingiza ndani ya mahakama na kumfikisha kizimbani.
Japokuwa alikuwa ameishiwa nguvu lakini aliweza kuona umati wa watu waliofurika hapo mahakamani. Wingi wa watu hao ulitokana baada ya kesi hiyo kutangzwa katika vyombo mbali mbali vya habari. Ilisababisha mamia ya watu kufurika mahakamani hapo, wakiwemo waandishi wa habari kufatiria kwa umakini kesi hiyo iliyogusa hisia za watu wengi. Waandishi wa habari walianza kumpiga picha daktari Mbaga ambae wanamuona akiwa katika sura ya Imamu Shafii na kila mtu humo ndani ya mahakama imani yake ilisadiki huyo ni Imamu Shafii.
Kila mmoja alibaki na mshangao kwa sababu walifahamu Imamu Shafii amekufa kwa ajari ya pikipiki lakini anaonekana akiwa hai, hali ya minong’ono ilitawara umo ndani ya mahakama huku shahuku ya kesi ilizidi kuongezeka ili kesi iyanze. Mwanga wa kamela nyingi uliendelea kummulika, akabaki amepigwa na butwaa kwa jinsi mahakama ilivyokuwa imefurika siku hiyo. Minong’ono iliendelea kutawala mahakamani hapo, kila mtu akizungumza lake lakini mwenyewe hakujari.
Kwa macho yaliyokosa matumaini, alianza kuwatazama watu waliokuwa wamefurika mahakamani hapo. Macho yake yalitua kwa daktari mwenzake aliekuwa anafanya kazi hospitari moja ya Amana ambae ni msaidizi wake katika kitengo cha uchunguzi wa maiti alishangaa kumuona yupo kizimbani, akuweza kuelewa kama shahidi au mtuhumiwa lakini akutaka kujua zaidi. Akiwa katika kutizama huku na huko anamuona wakiri aliyekuwa anataka kumtetea katika kesi hiyo Nana Samweli, macho yao yaligongana na kwa sekunde kadhaa walibaki wakitazamana lakini alipogeuzu sura kushoto mbele kabisa macho ya daktari Mbaga akiwa katika muonekano wa Imamu Shafii uso kwa uso na mkewe walitazamana huku uso wa mwanamke huyo ukiwa na huzuni na hali ya mwili wake ulidhoofika kwa kukonda.
Kutokana na jinsi alivyokuwa anajisikia ndani ya moyo wake, mwanamke alishindwa kuendelea kumtazama kwa sababu aliamini huyo ndio aliesababisha mumewe kuwa katika matatizo bila kujua kuwa huyo ni mumewe daktari Mbaga ili kivuli cha Imamu Shafii kipo ndani ya mwili wake, akajiinamia chini huku machozi yakimtiririka. Machozi mengi yaliyokuwa yakimtoka, yalikuwa yakichuruzika na kumlowanisha brauzi yake aliovaa lakini mwenyewe hakujari aliendelea kutokwa na machozi ya uchungu huku akitamka maneno ambayo hakuna aliyekuwa anayaelewa.
Daktari Mbaga akiwa katika muonekano wa Imamu Shafii alimuona mke wake akiwa katika hali hiyo alimuonea huruma sana. Hali ya huzuni ilimtawara usoni mwake. Muda huo huo anaingizwa mahakamani hapo R.C.O akiwa katika ulinzi mkali, waandishi wa habari waliacha kumpiga picha daktari Mbaga akiwa katika muonekano wa Imamu Shafii na kumgeukia R.C.O na kuanza kumpiga picha hadi anafikishwa kizimbani, anafunguliwa pingu. Watu wote waliodhuria mahakamani walishangaa kumuona R.C.O mkuu wa upelelezi ngazi ya juu akiwa chini ya ulinzi, kila mmoja alikuwa anajiuliza R.C.O nae anahusika na kesi hiyo, waandishi wa habari waliendelea kumpiga picha R.C.O kwa ajiri ya kuandaa habari watakazozirusha katika media mbalimbali.
Dakika kumi na tano, alifikishwa hapo mahakamani mtu aliefanana na daktari Mbaga akiwa amedhoofika sana na kubadilika kutokana na kukaa kwa muda mrefu mahabusu.Askari walimuongoza mpaka kizimbani akawekwa kizimba kimoja na R.C.O mkuu wa upelelezi ngazi ya juu, akafunguliwa pingu na kuachwa uhuru.Waandishi wa habari walianza kumpiga picha huyo mtu aliofanana na daktari Mbaga huku mamaia ya raia waliokuja kusikiliza kesi hiyo wengi wao walijua huyo ni daktari Mbaga, walijawa na simanzi baada ya kuona hali ya mwili wake ulivyokonda na kupoteza muonekano wake halisi. Mke wa daktari Mbaga alishindwa kuvumilia machozi yalianza kumtiririrka, daktari Mbaga akiwa katika umbo na muonekano wa Imamu Shafii alimuona mke wake akiwa katika hali hiyo alimuonea huruma sana.
“Kooooorti”
Sauti nzito ya askari aliyekuwa anamaanisha hakimu anakaribia kuingia ndiyo iliyomshtua kila mmoja aliyokuwepo hapo mahakamani. Watu wote walitulia na waandishi wa habari waliokuwa wakiendelea kumpiga picha mtu ambaye amefanana naa daktari Mbaga walitulia. Ukumbi mzima wa mahakama ulikuwa kimya kabisa, watu wote walitulia, hakukuwa na kelele zozote zilizosikika zaidi ya vishindo vya hakimu na jopo lake ambao waliingia na kwenda kuketi sehemu yao.Muda mfupi baadae, taratibu za kesi zilianza kufuatwa kama kawaida. Mwendesha mashtaka wa serikaili alisimama na kuanza kumsomea mashataka yaliyokuwa yanamkabili daktari Mbaga.
Watu wote walikuwa kimya kabisa wakifuatiria kwa makini kila kilichokuwa kinaendelea, waandishi wa habari nao walikuwa bize kuandika kwenye ‘notebook’ zao kila kilichokuwa kinaelezwa.Baada ya mwendesha mashtaka wa serikali kumaliza kusoma mashtaka yaliyokuwa yanamkabili daktari Mbaga, jaji aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo, alianza kusoma mwenendo wa kesi hiyo, ukiwemo utetezi wa mshtakiwa.
Baada ya kuzungumza kwa dakika kadhaa mfululizo, ilikuwa zamu ya daktari msaidizi wa daktari Mbaga kutoa maelezo yake huku yasiotofautiana na yaliondikwa katika faili la uchunguzi wa maiti ya dereva bodaboda. Ndipo daktari msaidizi wa daktari Mbaga alianza kutoa maelezo yake lakni mwisho wa maelezo alionekana si mkweli kwa sababu vipimo vinathibitisha amechunguza mwili wa Imamu Shafii baada ya daktari Mbaga kutoa vipimo vya uongo na akathibitisha Imamu Shafii amekufa kwa uthibitisho wa vipimo lakini kwanini yupo hai pia dereva bodaboda aliandika amekufa kwa ajari ya pikipiki wakati ni sumu ndiyo iliokatisha uhai wake. Daktari msaidizi wa daktari Mbaga hakuwa na cha kujitetea dhaili alionekana yeye si mkweli katika vipimo vyake na hakuwa na msaada kwa mkuu wake aktari Mbaga.
Ilifuata zamu ya mpelelezi aliefanya upelelezi wa kesi hiyo ndipo mpelelezi alianza kuelezea mwanzo hadi mwisho wa upelelezi wake hadi kufika mwisho wa kuwabaini watuhumiwa wote na kuwatia nguvuni. Baada ya kuthibitisha upelelezi wake mbele ya mahakama ndipo wakaulizwa msaidizi na vijana wake wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani. Walikuwa kama mchawi alierishwa usembe na kuropoka yote aliyoyafanya ya siri usiku wa giza katika imani zake za kishirikina.
Msaidizi na vijana wake awakupinga moja kwa moja walikubali kuwa walikuwa wezi wa pikipiki na bosi wao mkubwa ameshakufa ameuliwa na R.C.O mkuu wa upelelezi ngazi ya juu ili kupoteza ushahidi, waliendelea kutoa maelezo juu ya tukio la Imamu Shafii na mauaji ya dereva bodaboda ambae alikuwa mwizi mwenzao lakini aliuliwa na Scorpion mkuu wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani. Yote ilikuwa katika mpango wa kumshawishi Imamu Shafii kumtumia kusafirisha madawa ya kulevya kwa kutumia kivuli cha dini na mwisho wakamalizia kwa kusema daktari Mbaga kaingizwa katika kesi ya kutoa vipimo vya uongo na kupokea rushwa lengo kupoteza ushahidi wa mauaji ya dereva bodaboda lakini ukweli daktari Mbaga ahusiki na chochote hayo yote alishinikizwa kuyafanya baada ya kuhatarisha maisha ya familia yake.
Msaidizi na vijana wake wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani kutoka katika gereji ya scorpion wanamaliza kutoa maelezo yao.Watu wote waliopo hapo ndani ya mahakama hawakuweza kuamini kilichozungumzwa. Uliwadia muda ambao watu wote walikuwa wakisubili kwa shahuku kubwa ya kuongea mtu ambaye amefanana na daktari Mbaga. Alipopewa nafasi ya kuongea huyo mtu alikuwa kimya bila kuongea chochote kwa sababu hicho ni kivuli akiwezi kuongea chochote. Ukimya ulitawara kwa dakika kadhaa ndani ya mahakama kila mmoja akitaka kusikia ataongea nini ili kujitetea katika kesi nzito inayomuandama. Watu wote walikuwa kimya wakisubiri, aongee lakini kimya bila kuongea chochote, Hakimu alipaza sauti ya juu.
"Kutokana na watuhumiwa wameshathibitisha kuwa Fredy Mbaga kama daktari Mbaga amefosiwa kutoa vipimo vya uongo na katengenezewa kesi ya kupokea rushwa, maelezo ya watuhumiwa yamejitoshereza"
Watu wote walimgeukia hakimu na kumsikiliza juu ya kuongea kauli hiyo iliofanya mtu aliefanana na daktari Mbaga kumzuia kuongea. Hakimu alikohoa kidogo ili kuweka sawa koho lake, akavua miwani yake akaifuta vumbi kisha akaivaa tena na kumtazama daktari Mbaga aliyekuwa ametulia kizimbani, Akaendelea.
“Baada ya ya kusikiliza mwendo mzima wa kesi iliyokuwa inakukakabili Dokta Mbaga, mahakama imekukuta auna hatia kuanzia sasa hupo uhuru kinyume na sheria ya makosa ya jinai ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ilifanyiwa marekebisho mwaka 1977”
Ukumbi mzima walishangaa sana huku waandishi wa habari wakimpiga picha mtu ambaye amefanana na daktari Mbaga pamoja na mkewe akiwa sehemu aliokuwa amekaa machozi ya furaha yanamtiririrka.
R.C.O mkuu wa upelelezi ngazi ya juu alikuwa mwenye simanzi imani yake ilisadiki kesi inakwenda kwake, hakimu aligonga nyundo akawatuliza wapiga picha na minong’ono ya watu kuendelea.
“Mahakama inamtia hatiani ndugu Wilson Paul Makwaya kwa kosa la mauaji ya watu wawili, ndugu Marik Awadhi ambaye ni mmiliki wa kitengo cha wizi wa pikipiki mitaani na Yahaya Salum, pia kuchochea wizi mitaani na uhuzaji madawa ya kulevya"
Watu wote walishangaa kusikia kesi inakwenda kwa R.C.O mkuu wa upelelezi ngazi ya juu, waandishi wa habari kama kawaida yao walianza kumpiga picha R.C.O mkuu wa upelelezi ngazi ya juu, R.C.O mkuu wa upelelezi kwa aibu aliinamisha sura chini, hakimu aliendelea kutoa maelezo yake ya kuhitimisha kesi hiyo.
"Kutokana na ushahidi pande zote mbili wamethibitisha kwa asilimia mia moja wewe ndio mhusika”
Askari magereza na askari wa kawaida walisogea kizimbani alipokuwa R.C.O na kudumisha ulinzi.
“Kabla sijasoma hukumu, je ndugu mshtakiwa Wilson Paul Makwaya una chochote cha kujitetea?”
Watu wote waliokuwa mahakamani, walimgeukia mkuu wa upelelezi ndugu Wilson Paul Makwaya kizimbani alipokuwa amesimama, kila mtu akiwa na shauku kubwa ya kusikia atasema nini, R.C.O mkuu wa upelelezi ngazi ya juu anainua sura anawaangalia raia waliofurika ndani ya mahakama, anamwangalia daktari Mbaga akiwa katika muonekano wa Imamu Shafii, wanaangaliana uso kwa uso anaona aibu, anamwangalia daktari Mbaga anasikitika huku taratibu anageuza shingo kwa O.S.S mkuu wa upelelezi wa kituo ambae ni msaidizi wake ngazi ya chini ya upelelezi akiwa sambamba na mpelelezi wake anaemfuatia, anawaangalia kwa jicho kali. Mara hakimu anagonga nyundo tatu kumshtua R.C.O mkuu wa upelelezi ngazi juu ya kujitetea.
“Nafasi yako ya kujitetea”
R.C.O mkuu wa upelelezi ngazi ya juu anamgeukia hakimu.
“Kila chenye mwanzo kina mwisho wake”
Kauli hiyo kila mtu aliokuwa katika mahakamani hapo imani yake ilisadiki kesi imeshaisha kazi kwa hakimu, hakimu akupoteza muda wala kupepesa macho aligonga nyundo tatu akatoa hukumu,
“Mahakama imekukuta na hatia ya mauaji, kinyume na sheria ya makosa ya jinai ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ilifanyiwa marekebisho mwaka 1977, unahukumiwa kwenda jera miaka 30 na kuachishwa kazi moja kwa moja na mali zote ulizokuwa nazo zinachukuliwa na serikali”
Baada ya hakimu kutoa hukumu hiyo anagonga nyungo mara tatu, anaendelea kutoa hukumu anatoa hukumu kwa msaidizi na wezi wa pikipiki mitaani kutoka kitengo cha Scorpion gereji anawahukumu kila mmoja miaka kumi na tano jera kwa kosa la wizi wa pikipiki na kuua watu bila hatia. Anamalizia kutoa hukumu kwa daktari msaidizi wa daktari Mbaga kwa kosa la kutoa vipimo vya uongo. Baada ya kumaliza kutoa hukumu kwa watu wote waliohusika katika kesi hiyo hakimu anagonga nyundo anafunga mafaili yote muongoza kesi anasimama, inasikika sauti ya juu.
“Kooooorti”
Watu wote waliinuka na hakimu na jopo lake la majaji wanaondoka ndani ya mahakama. Askari wanamtoa R.C.O mkuu wa upelelezi kizimbani wanamfunga pingu, wanatolewa vijana wa kitengo cha wizi wa pikipiki wanafungwa pingu na daktari msaidizi wa daktari Mbaga nae anafungwa pingu wanatolewa ndani ya mahakama wanapelekwa sero iliopo hapo mahakamani. Wapiga picha walikuwa wanawapiga picha huku wakiwahoji maneno mawili matatu lakini watuhumiwa hawakuwa na hamu ya kuongea walikuwa wakali kutokana na hukumu walizopewa.
Wengi wao walikuwa na simanzi na majonzi huku hali ya majuto ikiwa imeshika kasi katika akili zao lakini ndio hivyo hakuna wa kumililia, waliokuwa na roho nyepesi walilia sana lakini hauwezi kugeuza jiwe ukawa mkate. Watu walianza kutoka ndani ya ukumbi wa mahakama huku minong’ono isioisha iliendelea katika vinywa vyao. Siku hiyo hiyo baadaye, gari la magereza lilifika likawabeba watuhumiwa wote na kuondoka kuelekea gerezani Segerea.
Daktari Mbaga akiwa katika umbo la Imamu Shafii, aliongozana na familia ya Imamu Shafii na waumini wa kiislamu na kuondoka eneo ilo la mahakama. Huku akimuacha mtu aliefanana nae ambaye ni kivuli chake kikiwa na mke wake.
**********
Daktari Mbaga akiwa katika umbo na muonekano wa Imamu Shafii alikosa amani ya nafsi kutokana na kesi kuisha lakini bado kivuli cha Imamu Shafii kimemtawara mwilini mwake. Waumini wa kiislamu walijua huyo ni Imamu Shafii maana maongezi yote anayoongea yanahusu dini na vitendo vyote vya Imamu Shafii. Mke wa Imamu Shafii muda wote alikuwa na furaha na daktari Mbaga akiamini ni Imamu Shafii hata walipofika nyumbani alimuandalia maji ya kuoga na kumpelekea bafuni. Daktari Mbaga aliekuwa katika umbo na muonekano wa Imamu Shafii, akuweza kuonesha utofauti wowote kama yeye ni daktari Mbaga na si Imamu Shafii anajiandaa anaenda bafuni kuoga huku waumini wakiwa wamejaa nyumbani kwake kila mmoja akitaka kujua mengi kutoka kwake.
Alitumia dakika thelathini kuoga, alitoka bafuni aliingia ndani akavaa kanzu safi vazi la kiislamu kwa waumini wanaume, alimuaga mke wake na kumwambia kuna sehemu anaenda, mke wake akuwa na kipingamizi moja kwa moja alijua mume wake anaelekea msikitini ili kukutana na waumuni wengine kuzungumza mengi yanayohusu dini na msikiti kiujumla.
Kwa pamoja na waumini wa kiislamu waliondoka hapo nyumbani kwa Imamu Shafii, safari yao hadi Kimanga mwisho katika duka la kuuza sanda za kuzikia. Walipofika hapo daktari Mbaga akiwa katika muonekano wa Imamu Shafii alinunua sanda. Waumini wa kiislamu walikuwa wanajiuliza sanda alionunua ya nani maana hakuna taarifa ya msiba kutoka sehemu yoyote, tangu alipotoka mahakamani akuonana wala kuongea na mtu hadi wanafika nyumbani kwake walikuwa watulivu ili waone mwisho wake. Daktari Mbaga alienda hadi wanapouza mbao alinunua mbao, waumini walishindwa kuelewa juu ya vitu hivyo vinavyonunuliwa.
Daktari Mbaga akiwa katika muonekano wa Imamu Shafii aliwaambia waumini wa kiislamu waelekee msikitini. Walitii kama walivyoambiwa, awakupanda daradara, walitembea kwa miguu njia nzima kila walipopita watu walikuwa wanamuonesha vidole daktari Mbaga akiwa katika muonekano wa Imamu Shafii wakiamini ni Imamu Shafii wakikumbuka tukio la darajani. Kama unavyojua msafara wa waumini wa kiislamu wakiwa katika safari, mwendo wa dakika ishirini wanafika msikitini Almasjid Tidc. Walipofika daktari Mbaga akiwa katika umbo na muonekano wa Imamu Shafii aliwaomba waumini wenzake wachukue vipimo vyake ili waandae sanda hiyo kwa ajiri ya mazishi, waumini wote walishangaa huku wakimzonga na maswali.
“Tukupime wewe kwa ajiri ya nani?'
"Msiba wa nani?"
“Mwisho wa vipimo na maandalizi atajulikana wa kuzikwa ila siku zote sanda kwa marehemu si kwa mtu hai”
Daktari Mbaga akiwa katika muonekano wa Imamu Shafii aliwajibu waumini wake. Waumini wakaanza kuiyandaa hiyo sanda mahususi kwa ajiri ya kwenda kumvalisha maiti lakini kila mmoja aliifikiria kauli yake kuwa sanda kwa marehemu si kwa mtu hai sasa vipi wachukue vipimo vya sanda kwake yeye mtu hai. Lilikuwa fumbo kwa kila muumini lakini hakuna alieweza kulifumbua fumbo hilo. Walimaliza kuiyandaa hiyo sanda, daktari Mbaga alizikusanya katika mfuko mmoja na akachukua na huo ubao akawaagaa aliondoka hapo msikitini. Waumini kila mmoja alishindwa kumuelewa juu ya mwenendo wake lakini walihisi labda anataka kujiua, amejiandalia vitu hivyo kama maandalizi ili ndugu zake wasipate shida. Baada ya kufikiria hayo katika akili zao waliamua kumfuata nyuma nyuma alipoelekea. Daktari Mbaga akiwa katika umbo na muonekano wa Imamu Shafii alielekea hadi nyumbani kwa Daktari Mbaga.
Alipofika hapo alisimama alikuwa anaiyangalia nyumba kwa muda na taratibu alisogea na kuanza kuishika kama vile anaifananisha. Waumini walishangaa sana kwa vitendo alivyokuwa anavifanya na awakuweza kufahamu hapo kwa nani na kwanini amekwenda. Ghafla kilitoka nje Kivuli cha daktari Mbaga uso kwa uso na daktari Mbaga akiwa katika umbo na muonekano wa Imamu Shafii, daktari Mbaga akakipa hizo sanda na ubao kivuli na kuondoka bila kuongea chochote.
“Yule si Dokta aliokuwa anakabiliwa na kesi?”
Mmoja wa waumini aliwaambia wenzake.
“Ndiyo yeye”
“Sasa kampa huyo Dokta sanda na huo ubao wa nini?”
“Unauliza nini wakati wote tupo jera unaliza gari inayopita nje”
“Ila nimegundua kitu”
Mmoja wa waumini aliwaambia wenzake, waumini wote walimgeukia na kumsikiliza.
“Atakuwa amempa sanda na ule ubao kwa ajiri ya ile maiti iliokutwa sehemu mmoja na Imamu”
“Kweli”
Wote walimuunga mkono na walifarijika na jibu lao, waliamua kuondoka eneo ilo na kumfuata alipoelekea daktari Mbaga akiwa katika umbo na muonekano wa Imamu Shafii. Daktari Mbaga aliondoka hadi msikitini lakini alipofika msikitini akuweza kumkuta muumini hata mmoja. Aliingia chooni alijisaidia alipomaliza. Alienda hadi katika bomba la maji akatia hudhu, alipomaliza aliingia ndani ya msikiti akaanza kuswali. Waumini walifika walimkuta anaswali. Kila mmoaja alikaa pembeni hadi anamaliza kuswali. Alipomaliza kuswali aliwaita, waumini, waumili walisogea hadi sehemu alipo.
“Naomba tusome kisomo maalumu kwa ajiri ya kumuombea marehemu”
“Marehemu!”
Wote walishangaa sana.
“Ndiyo marehemu kwani amjui marehemu ni nani?”
“Ndiyo atujui ni nani?”
Mmoja wa waumini aliuliza kwa lengo la yeye na wenzake.
“Tusome kisomo marehemu atajulikana na msiba utatangazwa”
Baada ya jibu ilo awakuwa na swali la kuuliza zaidi waliungana na Imamu wakaanza kisomo maalumu cha kumuombea marehemu hadi giza linaingia na muda wa ibada unakuwa umewadia wanaingia katika sala ya saa mbili usiku wanaswali. Walipomaliza wanaagana kila mtu anaondoka kwake. Daktari Mbaga akiwa katika umbo na muonekano wa Imamu Shafii aliondoka hadi nyumbani kwa Imamu Shafii alikutana na mke wa Imamu Shafii, mke wa Imamu Shafii aliamini huyo ni Imamu Shafii. Wanakula chakula cha usiku, baada ya kumaliza kula chakula, daktari Mbaga akiwa katika umbo la Imamu Shafii aliongea mengi sana na mke wa Imamu Shafii. Yote aliyokuwa anaongea ni shinikizo la Kivuli cha Imamu Shafii. Mengi aliyokuwa anaongea juu ya kuishi vizuri na wanadamu wenzake, kuzingatia sala na kufuata yote yanayompendeza mungu.
Mke wa Imamu Shafii akushangaa hayo maongezi kwakuwa Imamu Shafii kama Imamu ni kawaida kutoa ushauri na kumuelekeza mtu yale yanayompendeza mungu lakini kauli ya mwisho ilimfanya mke kuwa katika njia panda.
“Imani ya kweli ndio itakuponya na kile kilichotokea kwa nabii musa ni cha kweli na ni maono ya mungu hivyo kinaweza kutokea kwako au kwangu pia kama imani ikiwepo na kupita katika njia sahihi ya kumpendeza mungu”
“Sijakuelewa unachomaanisha?”
“Ilikuwa bado siku sasa bado masaa utaelewa ila kwasasa naomba tukalale”
Ndipo hapo mke alipobaki njia panda bila kuelewa alichomaanisha lakini akutaka kuendelea zaidi kuuliza aliamua kusubili huo muda ufike ili aelewe. Waliingia kulala lakini daktari Mbaga akiwa katika muonekano wa Imamu Shafii alikuwa anaumia kulala kitanda kimoja na mke wa Imamu Shafii ndipo aliinuka na kwenda kulala chini. Ilipofika saa saba usiku hali ya hewa ikwa imetulia Ghafla daktari Mbaga alijisikia nguvu zikimshukia, mwili wake ukawa dhaifu sana, alijisikia hali ya ubaridi kwenye mwili wake wa nyama, alitetemeka.
Upepo ulipuliza kuelekea alipo, akiwa amelala kitandani, aliona nuru nyeupe ikijaza chumba chote. Aliona shanga ndogondogo, nyeupe, za duara, zenye ukubwa wa kichwa cha pini. Shanga hizo zilikuwa zikianguka kama mvua inavyonyesha na zilipogusa ngozi yake, zilizama ndani. Zaidi ya hapo, aliona kama wingu linalofanana na ukungu mweupe likija kutokea juu. Nalo pia lilijaza chumba na likawa likizama kwenye ngozi yake kila lilipomgusa. Baada ya hapo, alimwona Imamu Shafii akitembea katikati ya lile wingu la ukungu kuelekea pale alipokuwa. Alikaa kwenye kiti chake pembeni hapo chini alipolala daktari Mbaga.
Alishindwa kuelewa kiti hicho kilitokea wapi. Ni kiti kizuri kilichotengenezwa kwa dhahabu. Umbo lake ni kama la viti vingine vinavyofahamika lakini kina sehemu ya kuegemeza mgongo. Kwenye kila mguu kuna nyota ya kung'aa, na nyota nyingine ya aina ileile, japo ni kubwa zaidi, iko kwenye sehemu ya kuegemea. Kivuli cha Imamu Shafii kilimsalimia na kikamnyooshea mkono wake na kumwambia amke maana muda unakimbia haraka sana. Alimvuta mkono wake daktari Mbaga aliinuka na kukaa kitandani, kisha akamwambia.
“Dokta Mbaga nataka uende nami ukairudishe nafsi yangu katika mwili wangu wa nyama”
Daktari Mbaga alikubali alisimama alimshika mkono wake kwa mkono wake wa kulia na walianza kutembea. Daktari Mbaga alifurahi sana kushikwa na Kivuli cha Imamu Shafii maana kwa namna alivyokuwa amemshikilia kwa nguvu, hofu yote ilitoweka. Lakini utembeaji wa safari hiyo ulikuwa tofauti na wanavyotembea watu kawaida. Japokuwa miguu ilikuwa inafanya kitendo cha kutembea lakini, ilikuwa kama vile wanaelea zaidi kuliko kutembea.
Muda wote walipokuwa njiani, walikuwa wanatembea wameshikana. Lakini mara tu walipofika nyumbani kwa daktari Mbaga waliachiana mara mlango wa nyumba ya daktari Mbaga ulifunguka kikatoka ndani kivuli cha daktari Mbaga viliungana kwa pamoja vikawa mwili mmoja na daktari Mbaga.
Baada ya uhungano huo daktari Mbaga na Kivuli cha Imamu Shafii waliondoka hadi mahali ambako ni pakavu sana, pakavu kuliko jangwa lolote unalojua binadamu, hakukuwa na dalili zozote za uhai. Hakukuwa hata na mti mmoja au hata jani au kiumbe chochote hai. Lilikuwa ni eneo linalofadhaisha sana. Lakini kulikuwa na jengo kubwa sana, na daktari Mbaga alipoliangalia vizuri hilo jengo aligundua ni msikiti. Kivuli cha Imamu Shafii kilimgeukia daktari Mbaga na kusema.
“Dokta tunaingia kupitia mlango ule ila fanya kila utakachoelekezwa maana mimi tukiingia ndani tunaachana.”
Daktari Mbaga alipoambiwa alitawariwa na hofu na kuanza kutetemeka na kumwomba wawe pamoja muda wote. Kivuli cha Imamu Shafii kilisisitiza yale yale na kumwambia awe na amani hakuna baya lolote litakalo mkuta. Daktari Mbaga alikiambia Kivuli cha Imamu Shafii akutaka kuingia kwenye sehemu ile maana anaogopa kuwa peke yake. Kivuli cha Imamu Sahfii kiliendelea kumsisitiza lazima mlangoni waachane ili apate nafasi ya kukamilisha hiyo kazi ili awe uhuru na mwili wake wa nyama. Daktari Mbaga alikubali kishingo upande, waliingia kupitia mlangoni. Walipopita mlangoni na kuingia ndani Kivuli cha Imamu Shafii kiligeuka moshi na kupotea. Daktar Mbaga aliona mabadilika hayo alitawariwa na hofu baada ya kubaki peke yake.
Alipofika ndani ya huo msikiti alikuta watu kibao wanaswali kwa pamoja, alisogea taratibu huku akiwa anaogopa kila anaemwangalia yupo bize katika swala lakini alipofika mbele alimuona mtu anamuelekeza kulala juu ya maiti. Aliogopa sana na alisimama mwili wote ulikuwa unatetemeka. Huyo mtu alimsisitiza akalale, juu ya hiyo maiti daktari Mbaga alisimama kwa muda huku akitafakari kulala juu ya hiyo maiti. Akiwa hapo alikumbuka kauli ya Kivuli cha Imamu Shafii.
“Dokta tunaingia kupitia mlango ule ila fanya kila utakachoelekezwa maana mimi tukiingia ndani tunaachana.”
Baada ya kukumbuka kauli ya Kivuli cha Imamu Shafii taratibu huku mwenye wasi wasi alisogea hadi ilipo hiyo maiti. Alipofika hadi katika hiyo maiti, alipoiyangalia usoni aliiyona ikiwa katika sura ya Imamu Shafii alishtuka. Huyo mtu aliokuwa anampa maelekezo aliendelea kumsisitiza halale juu ya hiyo maiti, daktari Mbaga alilala juu ya hiyo maiti ya iliokuwa na sura ya Imamu Shafii ghafla kama mtu alievutwa na umeme akanasa na kupigwa shoti za umeme. Hapo hapo Kivuli cha Imamu Shafii kilianza kutoka katika mwili wa daktari Mbaga. Kivuli cha Imamu Shafii kilipomaliza kutoka mwilini kwa daktari Mbaga, daktari Mbaga alidondoka chini na kupoteza fahamu.
Fahamu zake za kawaida zilipomrudia alifungua macho yake na kujikuta kwenye mwili wake wa nyama, huku akiwa amelazwa kwenye hospitali ya Amana. Alikuwa ametundikiwa dripu kwenye mkono wake wa kushoto, alimwona mke wake, mwanawe kipenzi na ndugu zake wengine kwenye kona moja ya chumba, ambako walikuwa wakimuangalia kwa mshangao. Aliona kwenye uso wa mke wake kwamba alikuwa analia, alimwuliza nesi mmoja wapo kama alikuwa anafahamu tatizo lake lilikuwa nini lakini alimfanyia tu mzaha na kusema:
“Umezimia ndani ya miezi sita”
Nesi alikuwa anajaribu kuelezea kwa lugha nyepesi namna hali yake ilivyokuwa, lakini alibaini kuwa alikuwa anaogopa kumkaribia, alimwomba amuitie daktari aliyemuhudumia, Nesi huyo alimuita. Daktari alipofika, alisema kuwa hakujua kulikuwa na tatizo gani kwake. Mwanzoni, alidhani kuwa alikuwa na malaria lakini vipimo vilionyesha kuwa akuwa nayo. Aliendelea kumueleza kuwa joto lake, mapigo ya moyo, na shinikizo la damu vilikuwa chini sana kwa viwango vya hatari lakini hakuweza kujua sababu yake.
Alisema kuwa hakuwa na cha kufanya tena kwa ajili yake. Hakuweza hata kumuandikia kulazwa maana akuwa na ugonjwa. Dripu waliyomuwekea ilikuwa haifanyi kazi mwanzoni, lakini alipofungua tu macho yake, ikaanza kufanya kazi. Ndipo walipendekeza kuwa awekewe dripu nyingine mara ile ya kwanza itakapoisha ili aweze kupata nguvu za kutosha kwenda nyumbani. Hivyo baada ya kuwekewa ndipu ya pili alipata nguvu akaruhusiwa kurudi nyumbani,alikumbuka kilichotokea juu ya Kivuli cha Imamu Shafii ilitoka katika mwili wake lakini ilibaki siri yake na asingemweleza mtu yeyote juu ya kile alichoona maana ni nani angemuamini na watu watamuelewaje. Aliendelea kujiambia kuwa atomweleza kamwe mtu yeyote juu ya mambo hayo yote mwanzo hadi mwisho akahidi kuwa itakuwa siri yake ya maisha yake peke yake.
Aliruhusiwa kurudi nyumbani, aliambatana na familia yake na watu zake wa karibu alirudi nyumbani. Alipofika kwake jambo la kwanza kulifanya alichukua kioo na kujiangalia paji la uso wake akaona sura yake halisi. Alifurahi sana na alipomuona mtoto wake akiwa katika ngozi safi ya kupendeza ile ngozi ya ukoma ilitoweka ghafla alizidi kufurahi.
Akiwa katika hali ya furaha alipokea taarifa kwa watu wasiojulikaana lakini kwa muonekano ni waumini wa kiislamu. Waumini hao walimpa taarifa ya msiba wa Imamu wa Almasjid Tidc Imamu Shafii alishtuka lakini alipokumbuka kilichotokea alifahamu Imamu Shafii alikufa tangu muda bali Kivuli ndicho kilichokuwa kinaishi ndani ya mwili wake. Akakumbuka kuwa alipewa sanda na ubao na Kivuli cha Imamu Shafii, akavichukua vitu hivyo akavipeleka hadi msikitini na kuwakabidhi waumini wakiislamu. Waumini walipoviona walivigundua hivyo vitu na walivipokea.
Msiba wa Imamu Shafii ulitangazwa kila kona ya Tabata Kimanga, watu wengi walifika katika msiba wa Imamu Shafii na Imamu Shafii alizikwa. Baada ya msiba kuisha waumini wa kiislamu wakamkabidhi barua daktari Mbaga ilioachwa na Kivuli cha Imamu Shafii, daktari Mbaga alipokea hiyo barua na kuanza kusoma. Barua hiyo ilimtaka daktari Mbaga abadilishe dini kutoka mkristo na kuwa muislamu.
Bila kipingamizi daktari Mbaga alikubali juu ya maombi ya husia ulioachwa na Kivuli cha Imamu Shafii. Daktari Mbaga akasilimu na kuwa muislmu. Kuanzia siku hiyo, daktari Mbaga alianza maisha mapya ya imani ya kiislamu kutoka katika imani ya kikristo alibadirisha dini na jina na kuitwa Ibrahimu. Taratibu watu walizoea jina hilo hata hospitali katika kazi yake ya uchunguzi wa maiti aliitwa daktari Ibrahimu. Baada ya miezi mitatu alipitishwa kama Imamu wa msikiti wa Tabata Mawenzi Almasjid Tidc na kuongoza msikiti. Japokuwa alikuwa ni mkristo wa roho mtakatifu asiyejua quran lakini alikuwa kama ameshushiwa kalama alijua qur-an, hadithi na sura zote hadi kutafsiri na kuisoma katika vitabu vya dini ya kiislamu kwa ufasaha. Hakukuwa na shaka juu yake aliwaongoza vyema waumini wa kiislamu katika msikiti wa Tabata Mawenzi Almasjid Tidc na kupendwa na kila muumini kutokana na upendo, ukarimu na utu wake.
Kazi yake ya udaktari ya uchunguzi wa maiti aliendelea nayo na alitenda kazi kwa haki kama imani yake inavyomruhusu alikataa rushwa na alikuwa aogopi chochote hata umpe vitisho vya aina gani Imani ilimtawara. Yalikuwa maisha mapya kwa daktari Mbaga lakini pia mwanzo mzuri wa mafanikio kwa askari mpelelezi Job na Muona wa kituo cha Tabata Shule. Baada ya watuhumiwa wote kuchaguliwa gereza, wanapandishwa cheo, O.S.S anachukua nafasi ya R.C.O mkuu wa upelelezi ngazi ya juu na Job mpelelezi na Muona wanachukua nafasi ya O.S.S lakini vituo tofauti.
MAWASILIANO ZAIDI TUCHEKI KUPITIA NAMBA HII KWA KUTUTUMIA HABARI +255682842818



0 Maoni