Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi (IPCC), Dkt. Ladislaus Chang’a, kwa mwaliko wa Programu ya Umoja wa Mataifa uratibu wa Mazingira (UNEP) ameshiriki kikamilifu katika Mkutano wa 6 wa Mawaziri na Mamlaka za Mazingira wa Asia na Pasifiki (6th AP Forum) uliofanyika kuanzia tarehe 26–29 Agosti 2025 Jijini Nadi, Fiji.
Mkutano huo uliandaliwa kwa pamoja na Serikali ya Fiji na UNEP ukiwa na kaulimbiu “Kutafuta Suluhisho Endelevu katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi Duniani”.
Sambamba na mkutano huo, Dkt. Chang’a alikuwa na vikao mbalimbali na waheshimiwa na taasisi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kikao na Mhe. Rupa B. K., Waziri wa Serikali ya Nepal, Wizara ya Misitu na Mazingira, ambapo alimpatia taarifa kuhusu mpango kazi wa IPCC unaotekelezwa hadi mwaka 2029.
Mazungumzo hayo yalijikita katika kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kimataifa katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na kuboresha sera za mazingira. Mhe. Rupa alishukuru na kupongeza sana kazi kubwa inayofanywa na IPCC.
Kwa taarifa zaidi tembelea 👉www.meteo.go.tz





0 Maoni