AKAMATWA KWA TUHUMA YA KUGHUSHI NYARAKA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limetoa ufafanuzi juu ya taarifa inayosambaa katika baadhi ya mitandao ya kijamii ikieleza kuwa Bw. Gasper Temba (30) ametekwa Jijini Arusha.



‎Akifafanua tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Justine Masejo amesema kuwa taarifa sahihi ni kwamba Bw. Gapser Temba ambaye ni mkazi wa Arusha hajatekwa, bali amekamatwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma zinazomkabili za kughushi Nyaraka.
‎SACP Masejo amebainisha kuwa tukio hilo llilifunguliwa huko Jijini Dar es Salaam na kueleza kuwa amekamatwa kwa mujibu wa sheria na taratibu nyingine za kisheria zinafuata.

‎Jeshi la Polisi mkoani Arusha limetoa onyo kwa watu wanaotumia mitandao ya kijamii kuacha kusambaza taarifa ambazo hawana uhakika zinazoweza kusababisha taharuki katika jamii.

Chapisha Maoni

0 Maoni