WAHAMIAJI HARAMU WAKAMATWA DAR

‎Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es salaam imeendelea na Doria na misako katika maeneo mbalimbali ya Mkoa Dar es salaam. Zoezi hilo limepelekea kukamatwa kwa wahamiaji haramu wapatao 22 kutoka nchi za Burundi, Malawi, Ethiopia, Kenya, South Sudan na Uganda.

Aidha wahamiaji haramu hao wamekamatwa kutokana na makosa mbalimbali ya ki-Uhamiaji ikiwemo uingiaji nchini kinyume cha sheria za uhamiaji pamoja na wengine kukiuka sheria na tarabu za ukaazi wao hapa nchini, upelelezi unaendelea ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa

‎Wahamiaji haramu hao wamekuwa wakiishi pamoja na kujishughulisha na mambo mbalimbali kama jamii ya Watanzania kupitia Kampeni ya Uhamiaji ya Mjue Jirani Yako imepelekea kuwezesha kuwafichua Wahamiaji hao haramu.


‎Idara ya Uhamiaji inaendelea kutoa rai kwa watanzania kutosita kutoa taarifa ya uwepo wa wahamiaji haramu katika maeneo yao, sambamba na hilo Idara imeendelea na zoezi la utoaji wa elimu ya Ki-uhamiaji kwa jamii.


Chapisha Maoni

0 Maoni