Chama Cha Mapinduzi CCM kimesogeza mbele vikao vyake vya juu vya kamati kuu na halmashauri kuu hadi Julay 26 mwaka huu huku kikao cha mchujo wa wagombea kikitarajiwa kufanyika Julay 28 mwaka huu.
Katibu wa itikadi uenezi na mafunzo CPA Amos Makala akizungumza jijini Dodoma amesema hatua hiyo inatokana na chama kuamua kujipa muda wa kufanya mchujo wa wagombea hao vizuri zaidi.
Amesema baada ya majina hayo kutangazwa utaratibu wa hatua zinazofuata utatangazwa rasmi ikiwa ni pamoja na muda wa kampeni ndani ya chama na tarehe ya kura za maoni.

0 Maoni