ONYO KALI LATOLEWA DHIDI YA UVUVI HARAMU KATIKA ZIWA TANGANYIKA

 Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya uvuvi kutoka mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma limefanya kikao kazi maalum katika Wilaya ya Nkasi kwa lengo la kupambana na uvuvi haramu katika Ziwa Tanganyika na Ziwa Rukwa.


Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Namanyere, Wilaya ya Nkasi, Mkoani Rukwa tarehe 29 Mei 2025 ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Mheshimiwa Dkt. Lazaro Komba.


Aidha katika hotuba yake Dkt. Komba alisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya serikali, vyombo vya ulinzi na usalama, na wananchi katika kulinda rasilimali za taifa, akibainisha kuwa uvuvi endelevu ni kichocheo muhimu cha uchumi wa wananchi, hususan waishio katika maeneo ya mwambao.

Vilevile, Naibu Kamishna wa Polisi (Oparesheni na Mafunzo), DCP Mihayo Msikhela, aliongoza kikao hicho alitoa onyo kali kwa wote wanaojihusisha na uvuvi haramu na kueleza kuwa Jeshi la Polisi limejipanga kuongeza doria, misako na oparesheni za mara kwa mara ili kuhakikisha sheria za uvuvi zinasimamiwa kikamilifu.


Vilevile DCP Mihayo Alisisitiza kuwa hatua kali zitachukuliwa dhidi ya watu wote watakaobainika kukiuka sheria hizo.

Nae Mkuu wa Polisi Wanamaji Tanzania, ACP Sokolo, alitoa shukrani na pongezi dhidi ya Serikali akieleza kuwa Serikali imetoa jumla ya boti 11 kwa Jeshi la Polisi Wanamaji kwa ajili ya kuimarisha doria katika maziwa Tanganyika.



Chapisha Maoni

0 Maoni