JELA MAISHA KWA KUBAKA MTOTO WA MIAKA 7

 Mahakama ya Wilaya ya Nyasa imemuhukumu Samwel Edward Mpangala maarufu kwa jina la Babu Ndamanjo (71), Mkazi wa Kijiji cha Kihagara, Wilaya ya Nyasa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka 7.


Hukumu hiyo imetolewa Mei 27, 2025 na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Nyasa Mhe. Osmund Nsackhatu Ngatunga ambapo amesema mshtakiwa alitenda kosa hilo katikati ya Januari 3, 2025 na Machi 31, 2025 katika Kijiji cha Kihagara wilayani Nyasa kwa kumdanganya muhanga kwamba hataki kumuona na mwanaume mwingine.

Mshtakiwa alitenda kosa hilo katika kesi ya jinai namba 8493 ya mwaka 2025 kinyume na kifungu cha 130(1)(2)(e) na 131(1) vya Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 marejeo ya mwaka 2022.

Mbele ya Hakimu Ngatunga, Wakili wa Serikali Frank Sarwatt na mwendesha mashtaka wa Wilaya ya Nyasa Hope Milanzi wamesema kuwa mshatakiwa alifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani Aprili 10, 2025 na kusomewa shtaka hilo ambapo mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo.

Upande wa mashtaka ulileta mashahidi watano akiwamo mhanga pamoja na vielelezo vitatu. Mahakama ilijiridhisha kwamba upande wa mashtaka umethibitisha kosa hilo pasi na kuacha shaka dhidi ya mshtakiwa.

Mshtakiwa katika utetezi alidai kwamba yeye anasingiziwa tu kwa kuwa anaishi peke yake na hana mke, "Mheshimiwa hakimu, mimi ninasingiziwa tu kwa kuwa wanaona sina mke hivyo mwanamke yeyote akionekana kwangu wanaona ni mwanamke wangu" alijitetea Samwel - "Babu Damanjo".

Hata hivyo mahakama ilitupilia mbali utetezi huo kwa kukosa mashiko na kumuhukumu mshtakiwa kifungo cha maisha jela na fidia ya Shilingi milioni mbili na laki tano (2,500,000) kwa mhan

Chapisha Maoni

0 Maoni