Safari ya kwanza ya treni ya kisasa ya Mchongoko (Electric Multiple Unit - EMU ) imeanza leo Novemba Mosi, 2024 kutoka Stesheni ya Magufuli mkoani Dar es Salaam hadi Stesheni Kuu ya Samia mkoani Dodoma.
Treni Mchongoko ( Electric Multiple Unit - EMU ) ina vichwa mbele na nyuma tofauti na treni zingine zenye kichwa kimoja, huku ikibeba jumla ya abiria 589 na inatembea kwa mwendokasi wa kilomita 160 kwa saa.


0 Maoni