VYAMA VYA USHIRIKA WA MAZAO WATAKIWA KUTUMIA MIZANI YA KIDIGITALI KUONDOA UDANGANYIFU KWA WAKULIMA

 

Mrajis wa Vyama vya Ushirika, Dkt. Benson Ndiege, amevitaka Vyama vya Ushirika vya Mazao kutumia mizani za kidigitali ili kuondoa udanganyifu na kulinda maslahi ya wakulima.

‎Maelekezo haya yametolewa kupitia barua ya tarehe 13 Machi, 2026, kwa Wenyeviti na Wajumbe wa Bodi wa Vyama vya Ushirika vya mazao Tanzania Bara.

‎ Vyama vitakavyobainika kuwa na mizani za kidijitali lakini havitumii ipasavyo vitachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria.

‎ Wakulima wanatakiwa kuhakikisha mazao yao yanapimwa kwa kutumia mizani zilizounganishwa na Mfumo wa Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (MUVU) ili kupata malipo stahiki.

‎ Dkt. Ndiege amevitaka Vyama vya Ushirika wa Mazao ambavyo havijatekeleza ununuzi wa mizani za kidijitali kuhakikisha vinanunua mizani hizo kufikia Juni 31, 2026.

‎Tume ya Maendeleo ya Ushirika inaendelea kuimarisha usimamizi wa Vyama vya Ushirika kwa kuratibu ununuzi na matumizi sahihi ya mizani za kidijitali.

Chapisha Maoni

0 Maoni