Jeshi la Polisi limeeleza kushangazwa na taarifa za kutekwa kwa Mchungaji Yanick Mbombo Cele raia wa Kongo jijini Dar es Salaam.
Mchungaji Yanick Mbombo alikamatwa Mei 15, 2025 mkoani Iringa kwa tuhuma za ubakaji na mauaji ya watoto wadogo, lakini ushahidi haukujitosheleza hivyo hakuandaliwa mashtaka.
Juni 17, 2025, Mchungaji na wenzake walifikishwa mahakamani kwa mashtaka ya kuendesha genge la uhalifu na kujipatia kesi kwa njia za udanganyifu, na walikiri kosa kwa njia ya Plea bargain.
Watuhumiwa walilipa faini ya shilingi milioni 20 na magari yao yakataifishwa, huku Mchungaji Yanick akiondolewa nchini na hakutakiwa kurudi tena.
Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi kuhusu taarifa za uwepo wa Mchungaji nchini na kutekwa kwake, na linaomba yeyote mwenye ushuhuda awasilishe kwenye kituo cha Polisi.


.webp)
.webp)
0 Maoni