Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linatoa wito kwa wananchi kupuuza taarifa za upotoshaji zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu usalama wa Mkoa wa Mwanza.
Hali ya usalama katika Mkoa wa Mwanza ni shwari, na wananchi wanaendelea na shughuli zao za kila siku kwa amani na utulivu.
Askari Polisi wanaendelea kutimiza majukumu yao ya kulinda maisha ya watu na mali zao kwa ushirikiano na vyombo vingine vya usalama.
Taarifa zinazosambazwa zinalenga kuleta taharuki na kuchonganisha jamii, na Jeshi la Polisi linawasisitiza wananchi kuzipuuza na kutafuta taarifa sahihi kutoka mamlaka husika.
Jeshi la Polisi linaendelea kuwafuatilia watu wanaosambaza taarifa za uongo na zenye kupandikiza chuki, kwani ni kinyume cha sheria za nchi.

0 Maoni