Jeshi la Polisi limeanza uchunguzi na kuwafuatilia watu wanaohusika na vitendo vya kikatili dhidi ya mtoto.
Polisi wanatoa wito kwa yeyote anayewafahamu watu hao au mtoto huyo kusaidia katika kumfikia na kuokoa afya ya mtoto.
Polisi wanatoa onyo kwa watu wenye tabia za unyanyasaji kwa watoto kwa lengo la kutafuta wafuasi kwenye mitandao ya kijamii, wakisema hawatasita kuwakamata.
Picha za mtoto akihamasishwa kuvuta sigara zinasambazwa mitandaoni, kitendo ambacho ni kinyume cha sheria na kanuni za kijamii na nchi.

0 Maoni