KAMISHNA BADRU ASISITIZA KUIMARISHWA KWA MIUNDOMBINU YA BARABARA NDANI YA HIFADHI YA NGORONGORO

 

Kamishna wa Uhifadhi Ngorongoro, Bw. Abdul-Razaq Badru, amesisitiza kuendelea kuimarisha miundombinu ya barabara ndani ya hifadhi ili kuboresha huduma kwa watalii, wawekezaji, na wananchi.

Barabara zinazohusishwa ni pamoja na Loduare hadi Golini (km 88), View Point hadi Naiyobi (km 76), Kimba, Edulen hadi makao (km 77), Endulen hadi Ndutu (km 52), Ndutu - Golini (km 23), Makumbusho Olduvai kwenda Nasera (km 54), na barabara za kreta ya Ngorongoro (km 110).

Kamishna Badru amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha barabara zinapitika wakati wote wa mwaka ili kuboresha viwango vya utoaji huduma.


Chapisha Maoni

0 Maoni