EWURA YATANGAZA BEI YA KIKOMO CHA MAFUTA YA PETROLI

 

EWURA imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta aina ya petroli kwa mwezi Februari 2026, zikionesha kushuka kwa bei ya dizeli kwa mafuta yaliyopokelewa bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara.

‎Bei ya rejareja ya petroli dizeli imepungua kwa shilingi 90 Dar es Salaam, 25 Tanga, na 24 Mtwara, huku bei ya mafuta ya taa ikipungua kwa shilingi 17, 14, na 93 mtawalia ikilinganishwa na bei za Januari 2026.

‎Bei za reja reja za bidhaa za mafuta kwa mwezi huu ni shilingi 2,788 Dar es Salaam, 2,849 Tanga, na 2,881 Mtwara; bei ya dizeli ni shilingi 2,701 Dar es Salaam, 2,762 Tanga, na 2,807 Mtwara; bei ya mafuta ya taa ni shilingi 2,881 Dar es Salaam, 2,794 Tanga, na 2,838 Mtwara.

‎Gharama za kuagiza mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam ziliongezeka kwa wastani wa 1.88% kwa petroli na 1.65% kwa mafuta ya taa, huku dizeli ikipungua kwa wastani wa 5.10%.

‎Gharama za kuagiza mafuta katika bandari ya Tanga zimepungua kwa 1.62% kwa petroli na dizeli, na bandari ya Mtwara zimepungua kwa 9.24% kwa petroli.

‎Wastani wa gharama za kubadilisha fedha za kigeni umeongezeka kwa 1.86%.

‎EWURA inawahimiza wauzaji wa mafuta kutoa stakabadhi za mauzo zinazoonesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa, na bei kwa lita, na vituo vyote vya mafuta vichapishe bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana.

Chapisha Maoni

0 Maoni