Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa angalizo la mvua kubwa siku ya Leo Tarehe 28/10/2025 katika maeneo machache ya mikoa ya Tanga,Dar-Es-Salaam ,Pwani ( vikijumuisha Visiwa vya Mafia ) na Morogoro pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba.
Mamlaka hiyo imesema kuwa uwezekano wa kutokea kwa mvua hizo ni wa wastani, na kiwango cha athari zinazoweza kujitokeza pia ni cha wastani. Hata hivyo, TMA imetahadharisha kuwa baadhi ya makazi yanaweza kuzingirwa na maji kutokana na mvua hizo.


0 Maoni