Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Almachius Mchunguzi, tarehe 02 Septemba 2025, ametoa wito kwa wananchi kushirikiana kwa ukaribu na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa kuhusu wahalifu na matukio ya kihalifu yanayojitokeza katika maeneo yao.
Akizungumza kupitia 88.5 TK FM Radio, ACP Mchunguzi amesema kuwa usalama wa jamii ni jukumu la kila mmoja, na si la vyombo vya dola pekee.
Aidha, amesisitiza kuwa ushirikiano wa dhati kati ya wananchi na Jeshi la Polisi ni silaha madhubuti katika vita dhidi ya uhalifu.

0 Maoni