Watoto waishio kwenye mazingira magumu mkoani Iringa wamekumbushwa umuhimu wa kuishi ndani ya familia ili kuepuka makundi ya kihalifu na tabia hatarishi zinazoweza kuathiri maisha yao ya baadaye.
Akizungumza na watoto hao Septemba 10, 2025 katika uwanja wa Mwembetogwa, Polisi Kata ya Makorongoni, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Magret Laizer amewaasa kuepuka kutembea usiku na kujihusisha na makundi ya kihalifu, huku akisisitiza athari za kuitwa watoto wa mitaani.
Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwatafutia watoto hao kituo cha makazi salama na wengine kupangiwa kujiunga na mafunzo katika Chuo cha Ufundi Stadi (VETA), ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwajengea mustakabali bora.

0 Maoni