Watendaji wa Uchaguzi ngazi ya Kata wametakiwa kuviishi viapo vyao walivyoapa kabla ya kuanza mafunzo.
Wito huo umetolewa na Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama Kuu Asina Omari leo Agosti 05, 2025 alipotembelea na kukagua mafunzo kwa watendaji hao katika Halmashauri ya Mji wa Kondoa, Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa na Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, ambapo pia amewataka watendaji hao kuepuka kupokea maelekezo kwa wasiohusika.
"Lakini kuishi kiapo chako ni pamoja na kuepuka kupokea maelekezo...kwa wasiohusika, toka umepata barua yako ya uteuzi wewe kwa kwa sasa kwa muktadha tulionao ni Mtumishi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi" Ameeleza Jaji Asina.
Mafunzo hayo ya siku tatu ambayo yalianza mapema jana Agosti 04, 2025 yanatarajiwa kukamilika kesho Agosti 06, 2025 ikiwa ni sehemu ya kuwajengea uwezo watendaji hao kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, mwaka huu.



0 Maoni