Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imebatilisha uteuzi wa Luhaga Mpina kuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo, ikisema haukufuata taratibu za chama hicho, hivyo hastahili kuwa mgombea wa nafasi hiyo.
Uamuzi huo, unakuja baada ya ofisi hiyo
kuwakutanisha viongozi wa chama hicho na Katibu Mwenezi wa ACT Wazalendo Mkoa wa Dar es Salaam, Monalisa Ndala aliyelalamikia kupitishwa kwa Mpina, akidai kulivunja kanuni.
ACT kinakutana na kikwazo hicho siku moja kabla ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kufanya uteuzi wa wagombea udiwani, ubunge na urais watakaoshiri Uchaguzi Mkuu Oktoba 2025.



0 Maoni