Kamishna wa Operesheni na mafunzo ya Polisi (CP) Awadhi Haji amefanya ziara katika Kambi ya wakimbizi Nduta Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma ambapo alizungumza na askari wa kambi hiyo na kujadili hali ya usalama katika eneo hilo.
Katika kikao hicho kilichofanyika kambi hiyo Agosti16, 2025 , CP Awadhi Haji aliwataka askari kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa weledi, nidhamu na mshikamano wa hali ya juu hususani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
CP Awadhi alisisitiza kuwa Jeshi la Polisi lina wajibu mkubwa wa kuhakikisha wananchi wanabaki salama, wakitumia haki zao za kidemokrasia bila hofu wala vitisho.
Pia aliwataka askari kuzingatia maadili ya kazi zao, kuendelea kushirikiana na jamii na kuepuka vitendo vinavyoweza kudhoofisha taswira ya Jeshi la Polisi. Alieleza kuwa nidhamu, uadilifu na mshikamano ni silaha kuu za askari katika kulinda amani na mshikikano wa taifa.

0 Maoni