MKULIMA NA MCHUMI , KAMANGE NA NDOTO YA KUWATUMIKA WANANCHI WA JIMBO LA MISSENYI MKOANI KAGERA

Na Lydia Lugakila.

Ukiwatafuta vijana wenye mvuto kisiasa na waliojaa hoja na ushawishi heshima  nidhamu, utu na maadili lazima umtaje Kijana EVANCE KAMENGE ambaye umaarufu wake haujaanza leo bali miaka mingi hii ni kutokana na moyo wake wa huruma kwa mdogo na mkubwa.


EVANCE KAMENGE ni Mchumi na mkulima kutoka mkoani Kagera ambaye amejitosa kuwania ubunge wa Jimbo la Missenyi huku akitamani makubwa kwa Jimbo la Missenyi tofauti na wengine watamanivyo na moja ikiwa ni kuona anakamilisha ndoto zake za uongozi.

MCHUMI NA MKULIMA , EVANCE KAMANGE MTIA NIA WA UBUNGE JIMBO LA MISSENYI MKOANI KAGERA.

Akizungumza na waandishi wa habari, hivi karibuni Kamenge alielezea azma yake ya kuleta mabadiliko chanya katika jamii ya vijana kupitia kilimo, ufugaji, na uzalishaji.


Evance anasema kuwa ana ndoto ya kuwajengea wana Missenyi uwezo na kuwapa ujuzi mbalimbali ili waweze kujitegemea na kuondoa umaskini.


 Anatilia mkazo umuhimu wa vijana kuzingatia fursa za kilimo na ufugaji kama njia bora ya kujipatia kipato na kuboresha maisha yao. 


Aidha, anaahidi kuwa anatamani kuona mapori kadhaa katika eneo lake ambayo hayajendelezwa kuona yanaendelezwa kwa maslahi ya wananchi ili wayatumie vyema kwa ajili ya maendeleo ya jamii.

MCHUMI NA MKULIMA , EVANCE KAMANGE MTIA NIA WA UBUNGE JIMBO LA MISSENYI MKOANI KAGERA.

Kamenge pia anatoa wito wa kuimarisha mahusiano ya kimataifa ili kuongeza fursa za kiuchumi na kijamii kwa vijana. 


Aidha Anapendekeza kwamba badala ya kupeleka vijana kutembelea Bungeni, ni bora wakapelekwa Ulaya ili kujifunza na kufaidika na fursa za kilimo ambazo zitasaidia kuendeleza shughuli zao za uzalishaji.


Kamenge anatamani kuona kila mtu katika jamii yake anaweza kujikimu na kuondokana na umaskini, huku akiwataka wananchi wa Jimbo la Missenyi kumuunga mkono katika safari yake ya kutafuta kiti cha ubunge cha Missenyi katika uchaguzi wa mwaka 2025-2030.


Evance Kamenge amemuomba Mungu amjalie nguvu na hekima katika kipindi hiki muhimu, akitazamia kuleta mabadiliko endelevu kwa watu wa Missenyi.

Chapisha Maoni

0 Maoni