Na Mwandishi wetu ,Kagera.
Mwanasheria na wakili wa kujitegemea hapa Nchini Salum Bagachwa ametia nia ya kugombea nafasi ya ubunge wa Jimbo la Missenyi mkoani Kagera huku kiu yake ikiwa ni kupambana na kumaliza changamoto zinazowakabili wananchi wa Missenyi ili kuwaletea maendeleo kwa haraka.
Akizungumza muda mfupi baada ya kuchukua fomu hiyo Juni 29, 2025 katika Ofisi za chama Cha mapinduzi Wilayani Missenyi Bagachwa amesema muda ukifika wa kuanza kutangaza sera atafanya hivyo ambapo msukumo wake ni kuwaleta maendeleo wananchi wa Missenyi na kuwapambania ili kutatua changamoto zinazo wakabili.
Bagachwa amesema kuwa yeye kama mzaliwa wa Kijiji cha Bugorora wilaya ya Missenyi anayajua matatizo yao na uwezo wa kuwawakilisha Wananchi Bungeni anao hivyo yupo tayari kuwasemea kwa chochote.
Aidha Bagachwa ametaja vipaumbele vyake kuwa ni kubuni miradi binafsi ambayo itaenda kuwanufaisha moja kwa moja wananchi wa wilaya ya Missenyi na kuwa muda ukifika na akafanikiwa atafanya kwa vitendo humu akiwaomba wana Missenyi kumuombea kwa mwenyezi Mungu wakati anapopita katika safari hiyo.

0 Maoni