Na Mwandishi wetu.
Afisa mkuu wa Nyanda za Malisho katika Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Emmanuel Augustine Kato, amechukua fomu ya kuwania ubunge wa Jimbo la Missenyi katika Mkoa wa Kagera kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza baada ya kuchukua fomu hiyo, Kato alisisitiza dhamira yake ya kuwahudumia wananchi endapo atapewa ridhaa hiyo.
“Niwaombe wananchi wawe wavumilivu wakati chama kikiendelea na mchakato wake wa ndani,” alisema Kato, akiongeza kuwa akipata nafasi hiyo, atajitahidi kuendeleza maendeleo katika jimbo hilo.
Kato, ambaye ni mzaliwa wa Kata ya Bugandika, ameahidi kutumia uwezo wake kuleta mabadiliko yanayofaa na maendeleo chanya katika jamii.
Aidha, ameonyesha kufurahishwa na uwazi na haki vilivyomo ndani ya CCM, huku akivutiwa na kazi kubwa iliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine wa chama hicho.

0 Maoni