Baraza la Wafanyakazi, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika kikao chake cha kwanza kilichofanyika Mei 11, 2025 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam limewachagua Bw. Frank Mhina Afisa Mambo ya Nje Mkuu kuwa Katibu wa Baraza hilo.
Bw. Mhina, anachukua nafasi iliyokuwa ikishikwa na Bi. Salma Baraka ambaye amemaliza muda wake
Naye Bi. Bertha Mturi, Afisa Mambo ya Nje amechaguliwa kuwa Naibu Katibu wa Baraza hilo na kuchukua nafasi iliyokuwa ikishikwa na Bw. Hassan Mnondwa Afisa Biashara ambaye pia amemaliza muda wake.
Katibu na Naibu Katibu wa Baraza hilo watahudumu kwa kipindi cha miaka mitatu
.jpeg)
0 Maoni