Mahakama ya Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu imemhukumu Jumanne Clement kwenda jela miaka 30 kwa kosa la kubaka mwanafunzi wa kidato Pili.
Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi Mhe. Enos Missana wa Mahakama ya Wilaya ya Maswa ambapo wakili wa Serikali Mwandamizi Violeth Mushumbusi na Mwendesha Mashtaka wa Wilaya ya Maswa Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Vedastus Mabu walieleza mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Aprili 4,2024.
Na hivyo mahakama imemtiahatiani mtuhumiwa huyo kutokana na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.

0 Maoni