Kutokana kwa ongezeko la baa katika makazi ya watu,Wakazi wa tabata wilaya ilala mkoa wa Dar-es-salaam wamelalamika kuwepo kwa wingi wa baa katika makazi yao na kusababisha kero nyakati za usiku.
Baa hizi zimejengwa karibu na maeneo ya mahospital,mashuleni,makanisani na misikiti kama ilivyo kawaida kwa baa yoyote athari zake ni kelele,ulevi na fujo katika eneo husika
Wakazi hao wameuomba uongozi wao kushughulikia kero hizo kwenye makazi yao,Pindi tu jua linapokuchwa wanashindwa kupumzisha akili zao kutokana na kero ya mziki wanazopiga Nyakati za usiku.
Sulemani Juma mkazi wa Tabata Barakuda, Amesema yani kwa sasa Tabata kumekuwa kama dampo la kuwepo kwa baa kila kona.
"Yani Tabata ya miaka mitano ilipita si Tabata ya miaka hii imekuwa na bar nyingi kila kona ukatizapo unakutana nazo yani kwangu mimi nachukia nawaomba serikali yetu iangalie hili ongezeko la kila kukicha baa inanipa kero kwangu"

0 Maoni