Ingawa mvua kubwa sana ilinyesha mchana wa siku hiyo, bado haikutosha kubadili hali ya jiji la Dar es salaam. Joto lilikuwa kali kupita kiasi usiku wa siku hiyo, wakazi wa maeneo ya Tabata Kimanga walilazimika kulala nje ya nyumba zao! Yote hii ikiwa ni kulikimbia joto lililokuwemo ndani ya nyumba zao.
Hiyo
ndiyo ilikuwa hali ya Dar es salaam kwa usiku huo.Tayari ilishagonga saa kumi
na moja alfajiri, adhana za misikiti mbali mbali zilisikika kuwaamsha na
kuwaimiza waumini wa kiislamu kuwai katika nyumba za ibada kwa ajiri ya kufanya
ibada.
Miongoni
mwa msikiti uliokuwa unapiga adhana ni msikiti wa Almasjid Tidc wa Tabata
Mawenzi eneo la kituo cha chama, baada ya kupigwa adhana hiyo waumini walifika
na kuongezeka kadri muda ulivyozidi kusogea.
Lakini
chakushangaza Imamu Shafii wa kuongoza ibada alikuwa aonekani hapo
Msikitini. Waumini wa kiislamu walijipa Moyo yupo eneo hilo hilo la msikiti,
lakini hadi muda wa ibada unatimia Imamu Shafii alikuwa aonekani.
"Ni
nani aliepiga adhana?"
Ni
swali lililoulizwa na mmoja wa waumini wa kiislamu waliopo hapo msikitini,
lakini hakuna aliejitokeza katika kundi lao kuthibitisha yeye ndie alipiga
adhana.
Wakiwa
wanashauriana nani aongoze ibada kwakua muda wa ibada umeshatimia, mmoja wa
waumini anaona damu kibla anawaonesha wenzake, wanasogea na kuanza kuangalia
hizo damu.
“Damu
hii ya nini?”
Muumini
mmoja anauliza huku anawaonesha waumini wenzake hiyo damu, walipepesa macho
huku na huko labda wataona kiumbe chochote kilichokufa lakini wapi mara
inasikika sauti kutoka mlangoni.
“Mashekhee
njooni nje”
Walitoka
hadi nje, kama hatua kumi na tano kutoka mlango wa kuingia ndani ya msikitini.
“Ebu
angalieni”
Huyo
muumini aliwaonesha waumini waliotoka ndani ya msikiti, damu iliojaa sehemu
moja.
“Ndani
ya msikiti kibla kuna damu kama hii, dhaili kabisa inaonesha damu hii ya
binadamu lakini ni ya nani?”
"Swali
ilo! kila mtu anataka kujua”
“Aliepiga
adhana ni nani?”
“Tangu
tumefika atujamuona aliepiga adhana?”
“Wote
atujui?”
“Nani
wa kwanza alianza kufika msikitini?”
“Mimi
nimefika baada ya dakika kumi adhana ya kwanza kuisha kuadhiniwa ila aliepiga
adhana sijamuona”
“Nani
sasa kapiga adhana”
Kwa hakika hakuna aliejua aliepiga adhana wala kufahamu damu hiyo imetokana na nini. Lilikuwa fumbo lililotanda mawazoni mwao bila kulipatia ufumbuzi.
“Cha
umuhimu tufanye uchunguzi eneo lote la msikiti”
“Sijui
kama tutafahulu kwa hilo kwa sababu damu ipo sehemu mbili kibla na hapa nje”
Mmoja
wa waumini aliwaambia wenzake na kupinga wazo alilotoa muumini mwenzake la
kufanya uchunguzi ili kujua chanzo cha damu hiyo ni nini na ya nani.
“Sawa
damu ipo sehemu mbili, lakini itakua vizuri tukifanya uchunguzi tunaweza
kugundua chanzo cha damu na ya nani”
“Kweli!
kabisa!”
Baadhi
ya waumini walimuunga mkono muumini mwenzao anaetoa wazo la kufanya uchunguzi
eneo lote la msikiti. Hata muumini aliekuwa anapinga na kwenda kinyume na
waumini wenzake alikubaliana nao maana wengi wape. Walianza kufanya uchunguzi
eneo la msikiti, baadhi waliingia ndani ya vyoo na wengine walizunguruka nyuma
ya msikiti ambako kuna eneo kubwa la kupaki magari.
**********
“INAL
LILLAH WAINA ILAIY RAJUUN”
Sauti
hiyo ilisikika kutoka umbali mrefu na kupenya masikioni mwa waumini wanaofanya
uchunguzi eneo la msikitini ili kujua chanzo cha damu na ya nani. Wote
waliacha kazi wanayofanya ya uchunguzi wanasikiliza kwa umakini sauti hiyo
inaposikika. Sauti ilizidi kusogea hapo msikitini kutokea kituo cha chama,
waumini wanaulizana.
"Sauti
ya nini?"
“Ebu
tusikilize kwa umakini”
Walitegesha masikio kama sungura aliehisi hatari, walisikiliza lakini ilikuwa ngumu kujua kwa sababu sauti ilikuwa inasikika kutoka umbali mrefu. Walitoka sehemu walipo walisogea eneo la mlangoni ili kujua sauti ya nini na nani.
“INAL
LILLAH WAINA ILAIY RAJUUN”
Sauti
ya Muumini mmoja ilisikika ikitamka kwa sauti baada ya kusikia sauti hiyo
ikitamkwa kutoka kwa mtu huyo anaekuja eneo ilo la Msikiti, anasababisha
wenzake kuwa katika mshangao baada ya kutamka.
“Inal
lillah waina ilaiy rajuun, ndio sauti ninayoisikia,”
Wote
walishangaa, muumini mmoja alirudia kutamka.
“INAL
LILLAH WAINA ILAIY RAJUUN!!"
"Ndio"
Muumini
huyo aliwaambia waumini wenzake watoke nje, walitoka hadi nje uso kwa uso na
muumini mwenzao akitamka kwa sauti ya juu.
“ INAL
LILLAH WAINA ILAIY RAJUUN”
Alifika
hadi kwa waumini wenzake akiwa anahema, jasho linamtiririka.
“ASALAM
ALEYKHUM”
"Waleykhum
mssalaam"
Nafsi
ya kila muumini ilikiri wazi kuwa na shahuku yakutaka kujua sababu ya kutamka
neno ilo zito la inal lillah waina ilaiy rajuun.
“Shekhee
kulikoni utokapo?”
Muumini
mmoja alimuuliza huyo muumini lakini bila kutoa jibu aliingia ndani ya msikiti.
“Nini
kimetokea juu yake?”
“Kimemkuta
nini muumini mwenzetu?”
“Itakuwa
umemfika msiba nyumbani kwake ndio maana yupo katika hali hiyo"
“Kwa
uhakika twende tukapate wasaha wake lakini hapa tutabuni kila jambo na
kusahau tatizo tulilokuwa nalo”
Walikubaliana
kwa pamoja walienda hadi ndani ya msikiti walimkuta muumini mwenzao akiwa
anasujudu huku akitamka maneno yale yale.
“INAL
LILLAH WAINA ILAIY RAJUUN”
Wanashangaa
kitendo anachokifanya muumini mwenzao, ndipo mmoja wa waumini anamsogerea hadi
sehemu alipo.
“Shekhee
unachokifanya unakufuru"
Huku
anamzuia, huyo muumini anaacha kusujudu, muumini mwenzake anamkarisha
kitako.
"Ebu
tuambie kimekukuta nini huko utokapo?”
Huyo
muumini huyo aliedelea kutamka kauli ile ile inallilah waina rajuun mara
alianza kuweweseka kama mtu alieingiwa na pepo mbaya. Waumini wenzake
wanamkamata wanammbeba juu juu hadi nje sehemu ya kutia hudhu wanamkarisha
kitako, muumini mmoja anachota maji anayasomea, alipomaliza kuyasomea
anammwagia kichwani huyo muumini.
Huyo
muumini alipiga kelele moja ya juu huku sura anaangalia mbingu, mara taratibu
anainamisha sura chini anaangalia ardhi anakuwa kimya kama dakika tatu,
inasikika sauti ya kihemo akipumua kama mtu aliekimbia umbari mrefu, mara
anaanza kulia kwa sauti ya chini.
“Shekhee
nini tatizo?”
Waumini
wenzake walimuuliza, huyo muumini anainuka akiwa na simanzi tele usoni kwake,
anamsogerea kila muumini anamshika mabega.
“Imamu
Shafii atunae duniani”
Kila
muumini anapopata taarifa hiyo akuweza kuamini anachoambiwa kwa wakati huo,
alikuwa anauliza ili kupata uhakika.
“Nini?”
“Imamu
Shafii?”
“Amekufa?”
“Ndio
amekufa kwa ajari ya Pikipiki na Maiti yake ipo darajani”
“Inal
lillah waina ilaiy rajuun"
Ndio kauli iliosikika katika kila kinywa cha muumini aliopata taarifa ya kifo cha Imamu Shafii. Taarifa hiyo ya kifo Imamu Shafii ghafla unabadili msimamo wa kujua damu walizoziona hapo msikitini kama barafu juani.
Uzuni
inatawara miongoni kwa kila waumini wa msikiti wa Almasjid Tidc kutokana na
kifo cha Imamu Shafii.
Dakika
ishirini na tano, waumini waliungana kwa pamoja walielekea moja kwa moja hadi
darajani katikati ya kituo cha Chama na Dukani ndipo ilipo maiti ya Imamu
Shafii.
Ulikuwa
mwendo wa dakika tatu, kutoka msikitini hadi hapo darajani ilipo maiti ya Imamu
Shafii, kama unavyojua mwendo wa waislamu wakiwa katika msafara wao. Walifika
ilipo maiti ya Imamu Shafii wanathibitisha kweli amekufa kwa ajari ya
pikipiki.
Kila
muumini roho ilimuuma sana, wengine walishindwa kuvumilia machozi yaliwatiririrka
na wengine walijitenga pembeni huku wakitafakari ajari hiyo Imamu Shafii
alikuwa anatoka wapi hadi akapata ajari hiyo kwa sababu nyumbani kwake ni kituo
cha Shiba ukiwa unatoka mjini mkono wa kulia, ukiwa unatoka Tabata Kimanga
mkono wa kushoto katika mtaa unaelekea nyumba ya wageni J.M, nyumba ya
tatu baada ya kuivuka nyumba ya Mzee Mashindano na mtaa unaotokea katika Pub ya
Hassani Mbiligenda almaharufu MPOGORO PUB, nyumba hiyo anayokaa Imamu Shafii
almaharufu kwa Mzee Shobo.
Walitafakari
juu ya ajari hiyo Imamu Shafii alikuwa anatoka wapi, anaenda wapi na kwa muda
gani lakini bila majibu na wakikukmbuka damu walizoziona msikitini ndio kabisa,
lilikuwa fumbo waliloshindwa kulipatia ufumbuzi.
**********
Taarifa
za kifo cha Imamu Shafii zilienea kila kona ya Tabata Kimanga. Mke wa Imamu
Shafii nae alipata taarifa za kifo cha mume wake kutoka kwa waumini wa
kiislamu. Kutokana na umaarufu wa Imamu Shafii kila aliepata taarifa za kifo
chake alifika katika tukio ili kujishuhudia mwenyewe. Watu walitoka sehemu
mbali mbali za Tabata Kimanga na kuja katika tukio hilo la ajari. Kila muda
ulivyozidi kwenda watu walizidi kuongezeka katika tukio hilo la ajali maeneo ya
Darajani.
Karibu kila aliefika katika tukio hilo la ajali alisikitika baada ya kuona ajali hiyo, lakini kama unavyojua kwenye wengi kuna mengi, wengine wakiwa wanasikitika kutokana na ajali hiyo dereva pikipiki kuungua yeye na pikipiki yake huku Imamu Shafii kichwani akiwa ametapakaa damu ikiashiria amepasuka kichwani lakini wengine walikuwa na kazi ya kupiga picha na kurekodi video na kusambaza katika mitandao ya kijamii.
Waumini
wa kislamu awakupendezewa na kitendo hicho, wanawazuia watu kupiga picha
na kurekodi video lakini inakuwa ngumu kwa sababu watu wengi wanazuia huku kule
wanapiga picha na kurekodi video. Kama unavyojua tabia za wabongo kila tukio
kwao dili ilimradi kujipatia pesa katika mtandao wa youtube na kuchangamsha
katika magroup yao ya whatsApp.
**********
Askari
wa kibongo kama unavyowajua wao siku zote katika matukio wanakuwa wa mwisho
kufika na wa kwanza kutaka kujua chanzo cha tukio. Walifika katika tukio
walipima ajali na kupiga picha tukio zima la ajali na kuanza kuhoji watu wawili
watatu ili kujua chanzo cha ajali lakini kila waliemuhoji aelewi chochote juu
ya ajali ilivyotokea na chanzo chake, kila mmoja ameikuta kama ilivyo.
Unakuwa
wakati mgumu kwa askari kujua ilivyotokea ajali hiyo wala chanzo cha ajali
hiyo kwa sababu hakuna alieshuhudia wala kuona ajali hiyo ilivyotokea.
"Bebeni
maiti zote tuzipeleke hospitali"
Ni
kauli ya mkuu wa kituo akiwaambia askari waliochini yake. Askari walitii amri
ya kiongozi wao walisogea zilipo maiti ili wazibebe lakini wakiwa wanaibeba
maiti ya Imamu Shafii ghafla waliibwaga chini.
“Mbona
mnaibwaga maiti?”
Mkuu
wa kituo anawauliza askari wake,askari wakiwa kimya wanaiyangalia maiti ya
Imamu Shafii huku wakiwa wametawariwa na hofu.
“Tatizo
nini?”
Mkuu
wa kituo aliuliza kwa mara ya pili ndipo askari bila kuongea chochote alionesha
kwa ishara katika mkono wa Imamu Shafii. Mkuu wa kituo alisogea hadi katika
maiti ya Imamu Shafii ili kuangalia anachooneshwa ndipo aliona katika mkono wa
Imamu Shafii katika mkono wa kulia, kidole cha shahada kinatoa shahada huku
mbele kikiwa na maneno yalioandikwa kiarabu yakisomeka.
"Ash
haduanlaa ilaha inlaalha waashhadu anaamuhammada rasuululhaa"
Kidole cha shahada kikigusa neno moja na lingine. Mkuu wa kituo alishtuka baada ya kuona tukio hilo, alibaki amekodoa macho kama panya kabanwa na mlango. Ilikuwa mara yake ya kwanza katika maisha kuona tukio kama hilo.
Hofu
ilimtawala, taratibu anarudi nyuma hatua tatu na kusimama bila kujua nini
afanye. Askari na wao wanarudi nyuma hadi sehemu aliposimama mkuu wao.
Raia
waliopo hapo waliona tukio hilo mwanzo hadi mwisho. Walisogea ili kuangalia
vizuri. Mtu mmoja alitoka nyuma ya kundi la watu huku alitoa simu mfukoni
alisogea hadi mbele karibu na maiti ya Imamu Shafii aliwasha kamera anapiga
picha lakini kabla frash ya simu aijatoa mwanga wa kamera inazibwa na mkono.
Huyo
mtu aliokuwa anapiga picha alishangaa anageuka kumuangalia alieziba kamera yake
ya simu uso kwa uso na mtu akiwa amevaa kanzu nyeupe kama mtu bara la Asia,
sura ya huyo mtu ilifanana na sura ya maiti ya Imamu Shafii alishtuka.
Huyo
mtu aliofanana na maiti ya Imamu Shafii ilimpa ishara huyo mtu aliekuwa anataka
kupiga picha ishara ya kumkataza kupiga picha. Huyo mtu aliokuwa anataka kupiga
picha alishindwa kujua ni pacha wa maiti ya Imamu Shafii au ni nani maana
wamefanana kila kitu. Huyo mtu alietaka kupiga picha alitaka kuongea.
“Shiiiiiiiiiiip”
Kwa
sauti ya chini mtu huyo aliefanana na maiti ya Imamu Shafii alimzuia kuongea
chochote. Huyo mtu alietaka kupiga picha alibaki kimya huku anatetemeka mwili
kwa uoga. Mtu huyo aliefanana na maiti ya Imamu Shafii alitoa mkono katika
kamera ya huyo mtu alietaka kupiga picha na alimwangalia kwa muda kama alitaka
kumwambia kitu, mara aligeuka alipiga hatua kutoka katika kundi la watu lakini
mbele alisimama anageuka anamnyooshea kidole cha shahada huku akiwa
anakichezesha kwa kukikunja na kukinyoosha na aliongea sauti ya chini
iliyopenya masikioni mwa huyo mtu alietaka kupiga picha maiti ya Imamu Shafii.
“Ondoka
haraka”
Huyo
mtu alietaka kupiga picha maiti ya Imamu Shafii anapita katikati ya kundi la
watu anaondoka eneo ilo la ajali. Huyo mtu aliefanana na maiti ya Imamu Shafii,
baada ya kuhakikisha huyo mtu alietaka kupiga picha katika maiti ya Imamu
Shafii kuondoka na yeye taratibu anapiga hatua anaondoka.
**********
Muumini
mmoja katika ilo kundi la waumini waliokuwepo hapo katika hiyo ajali alienda
hadi katika maiti ya Imamu Shafii anaushika mkono wa Imamu Shafii na kuanza
kuusomea hadi hicho kidole cha shahada kinatulia kinaacha kutoa shahada.
Muumini huyo baada ya kufanikisha hilo anaangalia juu.
“Inshallah”
Baada
ya kutoa kutoa shukrani kwa mwenyezi mungu muumba mbingu na ardhi na mtawala wa
mbingu na ardhi na vyote vilivyopo ndani yake.
"Mnaweza
mkaubeba kwa sasa"
Mkuu wa
kituo aliwaamrisha askari wake wabebe maiti, askari walisogea ilipo maiti ya
Imamu Shafii wakiwa wametawariwa na hofu wanaubeba mwili wa Imamu Shafii
wanauingiza ndani ya gari walilokuja nalo na wanamalizia kubeba mwili wa dereva
bodaboda wanaondoka.
Zilibaki stori midomoni ilikuwaje na chanzo chake lakini kila mmoja akuweza kufumbua fumbo la ajali hiyo na dereva wa bodaboda akuweza kujulikana kutokana na kuungua moto mwili wote ila Imamu Shafii alijulikana kwa haraka, zilibaki simanzi na majonzi kwa waumini wa kiislamu Almasjid Tidc na watu wanaomfahamu.
**********
Saa
tatu juu ya alama, daktari Mbaga, daktari bingwa wa uchunguzi wa maiti katika
hospitali ya Amana alishuka katika bajaji anaingia ndani ya hospitali.
Alitembea mwendo wa haraka kuashiria kuna kitu anawahi, mkononi akiwa ameshika
begi jeusi.
Alipofika
geti kubwa la kuingia ndani ya hospitali ya Amana alisikia anaitwa anageuka,
uso kwa uso na mtu akiwa amevaa kama mtu bara la Asia akiwa amekaa chini.
Daktari Mbaga alimwangalia huyo mtu kama akimfananisha kuna sehemu aliwai
kumuona lakini mboni za macho yake yalimthibitishia akuwai kumuona sehemu
yeyote hapo ndio mara yake ya kwanza kumuona.
Mtu
huyo alisimama anasogea hadi alipo Daktari Mbaga kwa mwendo wa taratibu
kutokana na umri umeenda mwenye mvi kichwani zinazoonekana kwa mbali chini ya
mwisho wa kofia aliovaa. Huyo mtu alifika hadi alipo daktari Mbaga, daktari
Mbaga alitoa begi mkono wa kulia anashika mkono wa kushoto kwa ajiri ya
kusalimiana lakini huyo tu alinyoosha mkono wa kushoto.
“Asalam
Aleykhum”
Daktari
Mbaga ni mkatoliki tangu kuzaliwa kwake lakini dini ya kiislamu anaifahamu
kupitia eneo analokaa hata salamu zao waislamu anazifahamu kwa kuwaona
wakisalimiana lakini alishangaa salamu inayotoka kwa huyo mtu ni ya kiislamu
lakini alinyoosha mkono wa kushoto, wakati anajua ni mkono wa kulia, sio
waislamu tu salamu yeyote lazima utoe mkono wa kulia.
Akutaka kumuuliza lakini imani yake daktari Mbaga ilisadiki huyo mtu amechanganyikiwa uenda anauguliwa na mgonjwa wake imepelekea kuvurugwa hadi anatoa salamu kwa mkono wa kushoto. Akutaka kumjaji sana huyo mtu, aliitikia salamu kama waislamu wanavyoitikia na anamuamkia kama mkubwa kwake na alitulia kumsikiliza. Mtu huyo alikohoa kidogo kulainisha koo na anamwangalia kwa muda daktari Mbaga na anamshika bega alimwambia kwa sauti ya chini na ilioshiria utu uzima.
“Bila
shaka wewe ndio daktari bingwa wa uchunguzi wa maiti na muda huu unawai katika
chumba cha vipimo,sasa najua umesomea unachokwenda kukipima kwa hiyo kuna maiti
mbili zitafika muda huu, naomba hizo maiti utoe vipimo sahihi na usithubutu
kutoa vipimo vya uongo vitaghalimu maisha yako.”








0 Maoni