Baada ya kuambiwa na wazazi wake warudi kijijini Isack hakuweza kukubalina na kauli ya wazazi wake kwa nia ya kurudi kijijini alikataa maana alitambua maisha ya kijijini ni magumu hivyo asingeweza kurejea kijijini kwa vile ingeshindikana kwake kukamilisha ndoto zake.
Kwa upande wa wazazi wa Isack walikuwa wanajihusisha na uuzaji wa pombe za kienyeji ambazo zilikuwa zinawasogeza kimaisha,Ndipo wazazi wake walipomuachia biashara hiyo ya kuuza pombe za kienyeji na kuyaendesha maisha yake akiwa na wadogo zake ambao aliachiwa na wazazi wake.
Ilikuwa ni hali ngumu sana kwa bwana Isack kuachiwa majukumu ya kuwa baba wa wadogo zake katika kuwaongoza kukabiliana na maisha,Lakini kwake ilimfanya apige magoti na kumuomba mungu,Maana majukumu yote ilikuwa kwake ya kuwalinda wadogo zake kwenye maradhi,njaa na hata katika kuwajenga kimaadili pia.
![]() |
| Isack Tangazi wa katika aliyeegemea mti akiwa na marafiki zake |
Maisha yake yalikuwa ni magumu hakua na kazi wala kibarua cha kuwaongoza wadogo zake pindi wasikiapo njaa,Kwa kijana yoyote ambaye ameachiwa mzigo mkubwa na wazazi wake ili kuyaendesha maisha yao bila wazazi wao huwa wanashindwa kufanya hivyo. Lakini kwa bwana Isack Tangazi ilikuwa tofauti japokuwa aliachiwa majukumu ya kuwaongoza wadogo zake mpaka pale watakapo maliza shule.
Pombe za kienyeji zilikuwa muhimili mkubwa sana katika kuyaendesha maisha yake ambapo biashara hiyo ilimpelekea kuwa katika mashaka na wasiwasi wa kutafutwa na polisi kila itwapo leo hali hiyo akuipenda lakini ilimbidi afanye biashara hiyo kutokana na hali ya maisha kuwa magumu alitamani kuicha lakini ilishindikana kutokana na majukumu makubwa kutoka kwa wadogo zake na miongoni mwa swali kubwa alilokuwa akijiuliza ni kwamba wataishi vipi pindi akiacha biashara hiyo kutokana na hakuwa na mbadala wa kazi tofauti na hiyo.
Minong’ono na majungu ilianza kusambaa kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki mara baada ya wazazi wake kumuachia jukumu la kusimamia familia yake ambalo waliona liko nje uwezo wake kutokana na kipato alichonacho kuwa duni hivyo isingeweza kutimiza mahitaji muhimu ya wadogo zake kama vile ada za shule, mavazi na chakula chenye kujitosheleza .
“Mbona wazazi wao wamewakimbia yani baada maisha kuwashinda wakaamua kuwaacha hawakufanya vizuri kabisa wataishije wasije wakawa vibaka tu mtaani hapa.”
Kauli hizo zilimuumiza na kumnyong’onyesha lakini kwa upande mwengine zilimtia nguvu na bidii ya kutafuta bila kuchoka na kuwasisitiza wadogo zake wasome kwa bidii ili kuokoa familia maana maneno na kauli za majirani walikuwa wanazisikia kuhusu sisi,Kwakuwa wadogo zangu walikuwa ni waelewa basi walishika maneno yangu.
Kutokana kipato kuwa cha chini ilipotimu 2007 aliamua kuaachana na biashara hiyo na kujiingiza moja kwa moja na biashara ya uuzaji wa samaki akiwatoa kilombero mkoani Morogoro na kuwasambaza katika maeneo mbalimbali katika jiji la Dar-es-salaam japokuwa alikuwa anatumia muda mwingi akiwa ametengana na familia yake katika kufuatilia mzigo huo hivyo pia faida ilikuwa ya kawaida kutokana na muda aliokuwa akipoteza akiwa mtoni huku wadogo zake wakitegemea mahitaji kutoka kwake .
Kutokana na kutokuwepo kwa takribani mwezi mmoja na nusu kuweza kuonana na familia yake pindi hawapo kwenye biashara ya samaki na faida yake kuwa ni kidogo na alitambua kuwa ana wadogo zake wanasoma shule wanamtegemea yeye,Ikambidi afanye uamuzi mgumu wa kuachana na biashara hiyo.
Kila kijana anapofikia hatua mfukoni hakuna kitu uchukua maamuzi magumu ya kwenda kukopa kwa mtu yoyote ili mradi maisha yake yaweze kusonga mbele,Hiyo ilimkuta bwana Isack Tangazi pale tu alipoona mfukoni hakuna kitu na familia inamuangalia yeye akachukua maamuzi magumu ya kwenda kwa mjomba wake bwana Isaya Mlenge ili aweze kumlaghai ili ampatie kiasi cha pesa ili aweze kufanya mambo yake.
Alipoweza kupewa kiasi cha laki tatu kwa miadi ya yeye kuenda kufanya biashara ya mbao kutoka kusini na kuleta jijini Dar-es-salaam na mjomba wake alimwambia kuwa wao watagawana faida atakayopata kwenye biashara ya mbao ilikuwa ngumu kwake kwasababu ya kiasi ambacho alichompatia kilikuwa ni kidogo kwa biashara hiyo lakini lengo lake kubwa ilikuwa ni kupata pesa na si kufanya biashara ya mbao,alipopata kiasi hiko cha pesa akakigawanya na kiasi kidogo akawapatia wadogo zake ili waweze kuwaindesha pindi yeye hayupo .
Aliweza kuwaachia wadogo zake kiasi cha laki moja na nusu na yeye kuanza kuondoka jiji la Dar-es-salaam.
Pindi maisha yalipozidi kuwa magumu Isack Tangazi akaamua kumpigia simu kaka yake Focusy Msambila na kumuambia kuwa nataka kuja Msumbiji, Lakini Focusy Msambila alimzuia kuenda nchini Msumbiji na kumuelezea kuwa nchi hiyo ina machafuko kutokana na vita za wenyewe kwa wenyewe,kwahiyo hutoweza kukabiliana na maisha ya huku na huwa watu wengi wanapokuja huku urudi majina kwahiyo usije , Isack Tangazi akukubaliana na kaka yake na kuamua kufunga safari nakuelekea nchini Msumbiji.
Huwa asilimia chache ya vijana wanaposhindwa na maisha ya Tanzania hufikiria kuenda kujaribu maisha ya nchi za nje kama south Africa na nchi zingine,Lakini kwa bwana Isack Tangazi ilikuwa tofauti kwake yeye alikuwa na mawazo tofauti na akili ya vijana wengine Isack Tangazi aliamua kuenda kujaribu maisha mengine nchini Msumbiji.
Safari ya kuenda nchini Msumbuji ikaanza lakini akuweza kumuaga mtu yeyeto zaidi ya wadogo zake huku akifikiria deni la shilingi laki tatu analodaiwa na mjomba wake,Ambalo anapaswa kulilipa pindi tu apatapo faida ya hiyo lakini akuweza kufanya biashara hiyo na kuamua kutumia pesa hiyo kama nauli ambayo itakayo msaidia kufika nchini hapo.kuenda nchini msumbiji kutokana na watu wakienda huko kurudi kwao inakuwaga ngumu,Ndipo alipoingia nchini msumbiji bila kujua Focusy Msambila kaka yake anaishi huko alikuwa atambui atalala wapi.
Lengo la kuenda nchini Msumbiji ilikuwa ni kufanya biashara ya madini lakini soko na uzoefu hakuweza kuwa nao wa shughuli hiyo,Maisha magumu na hali ngumu ya kimaisha umfanya kijana yoyote aweze kufanya shughuli yoyote hata kama ana uzoefu,Ndipo ilkuwa kwa bwana Isack Tangazi alipokuwa ana uzoefu wa biashara hiyo ndipo alipompata rafiki yake na kuanza kufanya biashara hiyo.
Mchoka ambaye ni rafiki wa Isack Tangazi,walikutana wilaya ya Mueda kijiji cha Chitope Mkoa wa cabdelgado nchini Msumbiji.
Mtihani wao wa kwanza kwenye biashara hiyo waliupata pale walipoweza kuwachimbisha watu madini na mfukoni mwao wakiwa na shilingi 50,000 kila mmoja,wachimbaji walipoweza kumaliza shughuli hiyo wakahitaji kulipwa pesa zao,Hapo ndipo ilipotokea mshike mshike ukaanza kutokea kwa bwana Isack Tangazi na Mchoka wakaanza kujiuliza maswali pesa watapata wapi ya kuwalipa wachimbaji hao na mfukoni mwao wana jumla ya shilingi 50,000 walipoanza kujiuliza maswali hayo nao wanakijiji wanapanga kuwadhuru bwana Isack na Mchoka.
Je wanakijiji watamdhuru Isack Tangazi au ataweza kuwakimbia na sehemu hiyo yeye hapafahamu vizuri na ni mgeni wa sehemu hiyo na yeye kashaonekana ni tapeli.
ITAENDELEA..........IJUMAA IJAYO




0 Maoni