Timu ya asasi za Haki ya Mwananchi na Mtanzania Foundation, waliopewa kibari na Tamisemi kutoa Elimu ya Mpiga Kura wameendelea kutoa Elimu kwa wananchi 373 vijiji Vya Naan na Njurai Kata ya Engusero katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro.
Mmoja wa mtoa Elimu hiyo , Sarah Toroge kutoka mradi wa MpigaKura255 wa Haki Mwananchi na Mtanzania Foundation tarehe 28 Oktoba 2024 , Ametoa Elimu ya Mpiga kura kwa wananachi 373, (wanaume 175, na wanawake 198).
Ikumbukwe , Tarehe 27 / 11 MWaka huu Kutakuwa na Uchaguzi wa Serikali za mitaa kumchagua Mwenyekiti Wa Mtaa na wajumbe , Hivyo Tamisemi imewapatia kibali Cha kutoa Elimu ya Mpiga Kura kwa Asasi ya Haki ya Mwananchi na Mtanzania Foundation kuwapatia Elimu Wananchi.



0 Maoni